Jumaa Aweso: Hali ya upatikanaji wa maji mjini yafikia asilimia 88

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,818
4,569
1683787273612.png

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Maji kwa Mwaka 2023/2024 ambapo amesema hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Mijini imeongezeka kutoka wastani wa asilimia 86.5 mwezi December, 2021 hadi wastani wa asilimia 88 mwezi Desemba, 2022.

Aweso amesema “Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa Wakazi waishio Mijini imeendelea kuimarika kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa maendeleo, jitihada hizo ni pamoja na Serikali kukamilisha utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo mbalimbali ya Mijini”

“Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Mijini imeongezeka kutoka wastani wa asilimia 86.5 mwezi Desemba, 2021 hadi wastani wa asilimia 88 mwezi Desemba, 2022, ongezeko hilo limetokana na kukamilika kwa miradi ya maji Mjini 40 inayohudumia Wakazi 2,345,537 wa maeneo ya Mijini”

“Serikali imeendelea pia kuboresha huduma ya uondoshaji wa majitaka katika maeneo ya Mijini ambayo hutolewa kwa njia ya mfumo wa mabomba na magari ya majitaka, katika kuboresha huduma utekelezaji wa miradi ya uondoshaji majitaka umeendelea katika maeneo mbalimbali nchini”

“Utekelezaji huo, umeongeza mtandao wa majitaka kutoka kilomita 1,385.8 mwezi Aprili 2022 hadi kilomita 1,416.93 mwezi Aprili 2023, pia maunganisho yameongezeka kutoka Wateja 53,428 mwezi Aprili 2022 hadi Wateja 56,923 mwezi Aprili 20230

“Aidha, katika Miji ya Geita, Kahama, Magu, Misungwi, Lindi, Kigoma, Sumbawanga, Bukoba na Lamadi huduma ya majitaka inatolewa kwa mfumo wa magari na mabwawa ya kutibu majitaka”
 
Back
Top Bottom