Juma kaseja alistahili kuwa mwanasoka bora wa mwezi january?

AljuniorTz

JF-Expert Member
Jan 6, 2009
544
17
Mnamo siku ya Ijumaa ya tarehe 20 mwezi huu wa pili, chama cha waandishi wa habari za michezo (TASWA) walimchagua mwanasoka bora wa mwezi Januari; uchaguzi huo ulimuangukia Juma Kaseja, golikipa wa Yanga FC kama alivyomtangaza Katibu Msaidizi wa TASWA Amir Mhando.

Mwanasoka bora huyo wa mwezi wa TASWA, alijinyakulia jumla ya shilingi za kitanzania 500,000/=. Kigezo??? kikubwa walichokitumia ni mechi ya ligi ya mabingwa wa Afrika, Yanga dhidi ya Etoile ambayo Yanga walishinda goli 14 -1.

Tukumbuke kuwa vyma au taasisi nyingi za michezo huwa wanachagua mwanamichezo bora kwa vigezo kadhaa alivyonavyo mchezaji, ikiwemo mchango wake kwa klabu yake,na timu ya taifa, nidhamu yake uwanjani na kambini, ushirikiano wake na wachezaji wenzake uwanjani na kambini.

Tukirudi ktk uteuzi wa kaseja, ndani yake kuna mizengwe kadhaa ilitokea lakini kubwa hasa huo mkutano wa uteuzi ulifanyika kienyeji mno. Waandishi wengi wa habari za michezo ambao ndio wanachama wa TASWA, hawakupewa taarifa mapema. Walioshiriki wengi wao walikwenda kuripoti michuano ya mashindano ya wachezaji wa vikosi vya pili vya klabu zinazoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara, wakaitwa ndani ya ukumbi wa mikutano ktk ofisi za TFF, wale waliochelewa kdg tu walikuta matokeo yanatangazwa.

Kuna wachezaji km Mrisho Ngasa, Haroub Cannavaro, Ally Shamte (karibuni ameitwa Stars) hawa wote walistahili kuwa wachezaji bora wa mwezi uliopita. Kaseja amepewa heshma ambayo hakustahili, ili hali wale waliostahili na ambao walitoa mchango mkubwa isiohitaji kufanyiwa utafiti wameachwa.

January mwaka huu ilifanyika michuano ya CECAFA na mechi za mzunguko wa pili wa ligi kuu ya bara.
Tukianzia CECAFA, Kaseja hakushiriki kabisa, lakini Ngasa na Cannavaro walishiriki na wakatoa ushirikiano mkubwa kwa Kilimanjaro Stars (Ngasa) na znz Heroes(Cannavaro)

Katika mechi za mzunguko wa ligi kuu ilizocheza Yanga FC kuanzia Januari 17, Kaseja alicheza mechi moja tu dhidi ya JKT Ruvu ambapo Yanga ilishinda 1-0. Mechi dhidi ya Prisons iliyofanyika Mbeya, Kaseja hakucheza lakini Ngassa ndie alisababisha goli lililoipa ushindi Yanga (Ally Shamte mfungaji). Mechi ya Mtibwa Sugar na Yanga alidaka Mzungu, Yanga walishindamechi hiyo.

TASWA walitumia vigezo gani hasa ktk uchaguzi wa Kaseja kuwa Mwanasoka mwazi Januari?

Labda nyie wadau mnajua

Thnx
 
Nami nimeshangaa sana kwa kigezo kipi sasa au kulikuwa hakuna activities zozozte wakaamua kuangalia nani hajawahi kupata???maana mm sijasikia Kaseja amefanya nini mwa mwezi Jan...
 
I dont dispute credibility ya TASWA, lakini zawadi hizi za TASWA hazina vigezo ambavyo ni clear. Nadhani Kaseja hana kosa kwa hili pia kwani yeye ametajwa tu. Ushauri kwa TASWA next time wakitaka waonekane zawadi zao ni za maana (credible) aidha washirikishe wadau au wawe na vigezo. Tumeyaona haya kwenye u-miss n.k.
 
Back
Top Bottom