tyc
JF-Expert Member
- Feb 25, 2014
- 1,178
- 2,977
Taarifa ni kuwa Juma Haji Duni, mgombea mwenza wa Lowassa kampeni zake zimesimamishwa kutokana na chama chake cha Chadema kupungukiwa pesa ya kufanyia kampeni, hivyo imeonelewa kuwa ni bora wabaki na mgombea mmoja ili kuendana na hali halisi ya mfuko. Wengi wenu mtakuwa mnakumbuka majuzi juzi Chadema walizindua harambee ya kukusanya michango ili kuwezesha mipango ya kampeni iende sawia, sasa mambo bado hayajawa vyema hivyo kamati kuu ya chadema ikaonelea ni bora kusitisha ratiba ya mgombea mwenza kama ilivyokuwa imepangwa tangu awali.