Umslopagazi
JF-Expert Member
- May 16, 2013
- 1,737
- 935
Nauliza tu maana sijamsikia kitambo sasa na kampeni zinayoyoma.
Jibu kwa hekima.
========================
Updates; 01 Oct 2015
Jibu kwa hekima.
JUMA DUNI KAPOTELEA WAPI?
Mgombea mwenza Ukawa Babu Duni amekata tamaa kabisa ya kutoendelea na mikutano ya kampeni kutokana na zomeazomea kuendelea kuikabili Ukawa.
Hata hivo kuna uwezekano Babu Duni akawa amesoma upepo mapema hivo kuamua kijiondoa ili kupunguza upotevu wa gharama.
Mbali na hivyo kwa taarifa za ndani kutoka CUF inasemekana anatakiwa arudi CUF kwasababu Ukawa wamekiuka makubaliano yaliyoafikiwa juu ya usawa wa vyama shiriki ukawa hivyo anatakiwa kujiondoa haraka Chadema arudi CUF na huo ndio utakua mwisho wa Ukawa
========================
Updates; 01 Oct 2015
Mgombea mwenza wa urais wa tanzania kupitia chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA ),anayeungwa mkono na vyama washirika vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi ( UKAWA ),Mh.Juma Duni Haji amesema kuwa mji wa utete wilayani rufiji ambao ulianzishwa mwaka 1899, zaidi ya karne moja iliyopita haukupaswa kudumaa kimaendeleo kutokana na kuwa na bonde la mto rufiji lenye rutuba kwa kilimo,pori la akiba la Serou pamoja na maporomoko ya maji ambayo yangetumika kuzalisha umeme.
Mh. Juma Duni Haji amehutubia mkutano wa hadhara wa kampeni katika mji wa Utete na kueleza kusikitishwa kwake na hali ya maendeleo ilivyo kwa kipindi cha miaka 53 tangu nchi ipate uhuru toka kwa wakoloni wa kiingereza.
Aidha, mgombea mwenza huyo wa Chadema akiongea kwa uchungu mkubwa amewahakikishia huduma bora za kujifungua akinamama wajawazito ambao wamekuwa wakipoteza maisha yao njiani wakati wakivuka mto rufiji kwenda kujifungua katika vituo vya afya na zahanati.
John Guninita,miaka 25 iliyopita aliwahi kuhudumu kama mkuu wa wilaya ya rufiji anaeleza hali ilivyokuwa wakati huo na sasa,huku makamu mwenyekiti wa chadema taifa kutoka Zanzibar Said Issa Mohammed akihoji kitendo cha uongozi wa serikali wilayani humo kuzuia madawati zaidi ya 100 yaliyotengenezwa kwa maelekezo ya waziri mkuu mstaafu Mh.Edward Lowassa yasitumiwe na wanafunzi wanaoendelea kukaa chini sakafuni.
Last edited by a moderator: