Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,056
- 23,506
Na Julius Mtatiro
Najulishwa kwamba, mtu aliyetoa BASTOLA wakati wa uvamizi wa mkutano wa CUF kwenye hotel ya Vina, Mabibo - Dar leo hii ni Ofisa wa Usalama wa Taifa.
Watu waliolifuatilia gari mojawapo kati ya yale yaliyowabeba MUNGIKI wa Lipumba (na kuwaondoa Vina Hotel baada ya kupiga, kuumiza na kupora waandishi na viongozi wa CUF), wamenipa ushahidi unaoonesha kuwa mtu huyo ni Askari wa vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama.
Natoa wito kwa waandishi wote wa habari waliokuwepo kwenye eneo la tukio watukabidhi picha zote za video na mnato ili tumsake mhusika na kuiweka picha yake hadharani.
UOVU hauwezi kudumu na kamwe hatuwezi kuukalia kimya. Leo nimekaa na kujiuliza, hivi kwa mfano njama za kuisambaratisha CUF zinazoongozwa na dola zikishafanikiwa, Tanzania itakuwa na viwanda? Ajira zitapatikana? Kina mama wataacha kujitwisha ndoo za maji vijijini? Kilo ya Unga itashuka bei?
Kwamba kuna uhusiano gani kati ya dola kutumia nguvu kubwa sana kukisambaratisha chama kimoja badala ya kutumia nguvu hizo kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja?
Too shameful!
Imeandikwa na Julius Mtatiro katika ukurasa wake wa Facebook
•INGELIKUWA VYEMA ANGETOA REASONS WHY IS TISS...
au mtu siku hizi akishatoa bastola tu anakuwa ni tiss?
***