Mama Maria Nyerere yupo New York,pamoja na mambo mengine atakutana na kusalimiana na Wafanyakazi wa Ubalozi wetu New York,atakutana na Mama Migiro (Naibu Katibu Mkuu) na baadaye ataonana na Bw. Miguel Brockman,ambaye ni Rais wa Baraza kuu la 63 la Umoja huo,Bw.Miguel ni raia wa Nchi ya Nicaragua,rais huyo wa Baraza kuu la UN ni mpenzi mkubwa wa Marehemu Nyerere,pamoja na kuwa na mazungumzo na Mama Nyerere,Bw. Miguel atamtunukia nishani Mama Nyerere kama kumbukumbu na ishara ya kumkumbuka Mwalimu kwa mchango wake katika Jamii.