Juliana Shonza, Mtella Mwampamba wangekuwa mbali sana kisiasa!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
10,590
2,000
Kama Juliana Shonza yule wa UDSM niliyekuwa nikimfahamu angeendelea kuwa Chadema basi leo tungekuwa tunaongea mengine.Juliana alikuwa kwa kasi kiwango ambacho hata Halima Mdee hakuanza nacho.

Juliana alikuwa akisimama jukwaani unabaki kuwaza mbali.Juliana alijiamini na kujisimamia.

Tatizo la Juliana Shonza ni moja tu, kukosa uvumilivu kwenye shida. Juliana alianza kuweweseka na vijisenti vya kudanganywa na wanaccm. Alidhani kuwa kwa kufanya hivyo angetengeneza msingi wa kuiua Chadema na yeye kuneemeka kama 'alivyodanganywa'

Majuzi nilikutana na kijana mmoja tuliyesoma wote UDSM ambaye alikuwa rafiki kipenzi wa Juliana. Alinieleza jinsi Juliana anavyojutia kudanganyika.Anajua fika kuwa leo angekuwa mbali sana mithili ya akina Halima Mdee! Anajua jinsi alivyojikosesha nafasi muhimu kwenye jamii. Hilo anajutia na zaidi anavyoiona Chadema ilivyo sasa. Juliana analia jinsi alivyotumika vibaya. Rafiki yake anasema kuwa Juliana anadai kuwa yupo katika njia isiyo na malengo, zaidi isiyoeleweka. Sasa anajiuliza nini afanye? Hiyo nawaachia wana-jf wamjibu.

Mtella Mwampamba naye bila shaka anajilaumu maana huwa tunasema a=b=c. Kwa hiyo bila shaka hilo nalo analo. Tena huyu ndo katelekezwa kabisa. Hana tena nyuma wala mbele.Aliyokuwa akitarajia kwa Chadema ili aneemeke yote yamebuma
Huyu bado sijasikia kutoka upande wake ingawa ni dhahiri ndivyo ilivyo!
 

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Kwani wewe umefika wapi kisiasa pamoja na kuwa wakala wa kumwagia watu tindikali.
 

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Yericko Nyerere na Ben Saanane wamefaidika nini na Chadema? Mbona hawana mbele wala nyuma Chadema ina wenyewe kama Mbowe hakupendi huna chako utaishia kuwa msukule daima dumu.
Wamebakia na jambo moja kuwinda kuuwa watu basi.
 

lyinga

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
2,498
0
huu ni mfano mzuri kwa vijana, tutulie sehemu moja tujenge nchi!!!!!! Kabwe mwenyewe anasita kuiacha Chadema sasa nashangaa mtu anaiacha kirahisi, kilishakuw chama kikubwa.
Waambie mdau huwezi kula muwa bila kukuta fundo na maisha ni safari ndefu yenye milima na mabonde.
 

Magwira

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
286
225
Yericko Nyerere na Ben Saanane wamefaidika nini na Chadema? Mbona hawana mbele wala nyuma Chadema ina wenyewe kama Mbowe hakupendi huna chako utaishia kuwa msukule daima dumu.
Vp we dodoki ulishatembea uchi baada ya CHADEMA kujizoolea vijiji, mitaa, vitongoji na wajumbe kibao hadi kwenye eneo lako?
 

magode

JF-Expert Member
Oct 2, 2014
2,123
2,000
Yericko Nyerere na Ben Saanane wamefaidika nini na Chadema? Mbona hawana mbele wala nyuma Chadema ina wenyewe kama Mbowe hakupendi huna chako utaishia kuwa msukule daima dumu.
Mwanaume kuwa mbea unatudhalilisha wanaume wenzio! Ukiendelea na hii tabia ya umbea usishangae kutumiwa pm ukiombwa 0713.....!!!!
 

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
9,692
2,000
Nadhani ni wakati mwafaka wa Hawa wadau kukubali kuwa waliteleza na warudi kundini.
Stella Mapamba siyo rahisi kupewa Airtime kwa maana Makada wanapendelea zaidi Sketi..
Kutenda kosa siyo kosa, bali kurudia kosa. Na ninavyompenda huyu Juliana sasa :confused2:
 

gefa

Member
Apr 4, 2014
88
70
dah! huyo habib mchange pale udom alikua moto mbaya, dizain jamaa alipostpone hadi degree yake, nasikia jamaa aliahidiwa kupelekwa akasome ujerumani, duh huyu zitto ameua wanasiasa chipukizi jamani.
 

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,720
2,000
Yericko Nyerere na Ben Saanane wamefaidika nini na Chadema? Mbona hawana mbele wala nyuma Chadema ina wenyewe kama Mbowe hakupendi huna chako utaishia kuwa msukule daima dumu.
Usiguse hizo namba kabisa ni hatari sana,na kama unataka mafanikio yao futilia matoke ya kura za juzi jumapili
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom