TAARIFA ya kuvuliwa uanachama CHADEMA kwa Juliana Shonza(M/Kiti), Mtela Mwampamba na Habibu Mchange

Taswira

JF-Expert Member
Sep 23, 2012
1,198
447
TAARIFA HII IMETOKA MOJA KWA MOJA KWENYE MIKONO YA BAADHI YA WAJUMBE WA KIKAO CHA KAMATI TENDAJI YA VIJANA (BAVICHA)


Ndugu Wanajukwaa,

Taarifa za kuvuliwa uanachama wa CHADEMA kwa Juliana Shonza (Makamu Mwenyekiti BAVICHA), Mtela Mwampamba na Habib Mchange ni za kweli!

Hatua hii ilifikiwa jana na kikao cha kamati tendaji ya BAVICHA iliyokutana pale Ukumbi wa Mbezi Garden majira ya Saa sita na nusu Mchana.

Kikao hiki kimsingi hakikuweka wazi ajenda za kwenda kujadili uanchama wa wahusika hapo juu (Pitia taarifa ya Tumaini Makene hapa JF kuhusu kikao hicho) licha ya wahusika hao hapo juu kualikwa kuhudhuria kikao hicho.

Wajumbe walioalikwa kwa ajili ya kikao hiki ni kama wafuatao: (Hawa wahusika si wajumbe wa kikao cha kamati tendaji BAVICHA)

1. Ben Saanane
2. Chacha Hatari
3. Habib Mchange
4. Mtela Mwampamba
5. Gwakisa Burton Mwakasendo.

Hao wajumbe hapo juu walihojiwa na kamati tendaji kila mmoja kwa nafasi yake na mashitaka yake mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la vijana Ndugu John Heche na katibu Deo Munishi.

Naomba kuyaweka mahojiano kama ifuatavyo, (mahojiano yalianza kufanyika saa tatu na nusu usiku).

Ben sanaane
alihojiwa kwanini ametoa shutuma kali mitandaoni kwa viongozi wake wa juu (Zitto)?

Majibu ya msingi ya Ben Saanane yalikuwa ni kwamba aliamua kufanya vile kwasabu ya kukilinda chama na viongozi wake wasihafuliwe mitandaoni na vijana aliowataja ni 'Masalia'.

Swali likaja; yeye haoni kama alikuwa anamchafua Zitto ambaye ni kiongozi wa chama? Jibu lake lilikuwa ni kuomba radhi amekosea.

Mtela mwampamba alihojiwa kwa kuulizwa mashitaka mawili. Moja ni kwanini anampinga Dr. Slaa kuwa anamiliki kadi ya CCM na pili kwanini alimkashifu Dr. Slaa hapa JF kwa kutumia 'Verified Account'

Majibu ya Mwampamba ni kama ifuatavyo:
Kwanza alianza kwa kuomba kubadilishiwa mwenyekiti wa kikao kwasababu hana imani naye. Kwanini hana imani naye? Ni kwa sababu wana 'conflict of interest' kwenye siasa (kuanzia kwenye uchaguzi wa BAVICHA) hawaelewani hivyo anaamini haki haitatendeka endapo Heche atasimamia mahojiano yale.

Mjumbe mmoja (mwenyekiti Arusha) akanyoosha mkono kwa kusema asiwasumbue wapo kazini. Mwampamba akajibu, hata mbunge wa Arusha Godbles Lema aliomba kubadilishiwa jaji kwenye kesi yake kwasababu alikuwa hana imani naye. Mwampamba akaongeza kwa kusema Ibara ya 18 na 19 ya katiba mama ya nchi inampa uhuru wa kuchagua nani wakusikiliza maoni yake na haki ikatendeka.

Mjumbe mwingineakasimama akasema kuwa yeye ameacha kata yake na kuja kusikiliza, Mwampamba unatusumbua. Mwampamba akamjibu mimi nimeacha wanachi 32,000 kule Mbozi jimboni (alikogombea ubunge mwaka 2010) wanaonitegemea nimekuja hapa, wewe unataka kusema ndio unajua sana kazi?

Kilichotokea: Bwan John Heche akagadhabika na kuamuru mabaunsa sita (6) wakiongozwa na Baunsa wa Mbowe anayejulikana kwa jina la 'Swai' wamtoe nje. Mwampamba alitolewa nje kwa nguvu, akatoka!

HABIB MCHANGE:
Yeye alikuwa na shitaka la kuwakashifu viongozi mitandaoni. Habib Mchange akahoji kwa mwenyekiti wa kikao. Kwanza alihoji uhalali wa kikao, kwasababu kile kikao kikatiba hakipo kwasababu hakuna makatibu wa baraza la vijana ni kikao cha wenyeviti tu? Pia, akaomba aelezwe ameitwa kama nani kwenye kikao kile? Pia akaomba apewe mashitaka yake yenye uthibitisho wa yeye kuhusika na hayo wanayo yasema.

Mwenyekiti kwa hasira akaamuru mabaunsa wamtoe Mchange nje! Mchange kwa ustaarabu akatoka nje.

Gwakisa Burton:
Yeye alikuwa na mashitaka mawili la kumpinga Dr. Slaa kuwa na kadi mbili ya CHADEMA na CCM pamoja na kumpinga Sugu Mbunge wa Mbeya mjini (CHADEMA).

Bila kuchelea Gwakisa akakili kweli alimpinga Dr. Slaa kwa kumiliki kadi mbili, Pia alikili alimpinga Sugu kwasababu wanatofautiana kimawazo (ikumbukwe Gwakisa alitolewa kwenye kura za maoni jimbo la Mbeya Mjini ili Sugu apitishwe kuwa mgombea). Alichokifanya mwenyekiti John Heche palepale akaamuru kumsamehe Gwakisa na kupewa onyo kali la kutorudia tena kuwapinga viongozi wake.

Ndugu wana JF,
Kikao kilimalizika mnano saa 5 na dakika 46 usiku. Maazimio ya kikao kile ni kuwavua uanachama wahusika watatu hapo juu.

UTATA ULIPOJITOKEZA:
Kimsingi katiba hairuhusu kabisa na haiwapi mamlaka BAVICHA kufukuza uanachama mtu yeyote. Kwenye katiba hakuna sehemu kamati tendaji inapewa nafasi ya kuhoji na kufukuza wanchama ndani ya chama.

Pia, Juliana Shonza atavuliwajwe uongozi na kamati tendaji wakati katiba inaeleza wazi kuwa mkutano mkuu utaitishwa lilikumvua uongozi kwa sababu yeye alichaguliwa na mkutano mkuu?

HATUA ALIYOICHUKUA FREEMAN MBOWE:
Nimetoka makao makuu ya CHADEMA muda huu pale Kinondoni, wameandaa toka asubuhi eneo, ambapo palitakiwa pafanyike Press Conference na vyombo vya habari kuhusu maazimio ya jana kwenye kikao. Freeman Mbowe amezuia hatua hiyo ya kutangaza maazimio hayo kwa sababu BAVICHA hawana mamlaka ya kumuwajibisha mwanachama yeyote, Kinachotakiwa BAVICHA kukifanya ni kupeleka mapendekezo yao kamati kuu ya CHADEMA taifa ndiko maamuzi yote yatafanyika.

Kwa maana hiyo John Heche na Mbowe wapo kwenye msuguano mkali kutokana na kwamba hili swala likifika kamati kuu litakwend akinyume na wanavyotaka. Wajumbe wengi wa kamati kuu wanaendesha mamuzi yao kiutu-uzima, bila hisia na kikatiba. Pia uzito wa makosa haya haupelekei kupoteza vijana hawa wenye umuhimu mkubwa kwenye majimbo yao na kwenye chama.

KUHUSU JULIANA SHONZA:
Yeye hakufika kwenye kikao kile kutokana na kutokuwepo jijini Dar es Salaam na taarifa kuchelewa kumfikia. Hivyo walishindwa kufanya mahojiano naye na kumpatia mashitaka yake.

HALI NDANI YA KIKAO ILIVYOKUWA:
Wajumbe walionekana kuandaliwa ipasavyo kisaikolojia kwaajili ya kuwakabili Mwampamba na Mchange. Kwa sababu walipoingizwa kwenye ukumbi wa kikao kila mmoja alitengewa kiti chake na kukabishiwa mabaunsa 6 kwa ulinzi. Muda wote Mwampamba na Mchange walikuwa kwenye ulinzi mkali sana.

Waalikwa wengine kama Saanane na Gwakisa na hatari walikwa hawana ulinzi, wapo free.

MWISHO:
Hii ndio CHADEMA, kuna uwezekano wa wanachama wengi wakafukuzwa kwa kupigiwa simu tu bila katiba kufuatwa. Pia kufukuza wanachama ndio last solution kwa kulea vijana?

UPDATES:
Press conference ipo confirmed inafanyika majira ya sa tano asubuhi ya leo Tar:7/01/2013 makao makuu ya chadema.

Katika maadhimio hayo,Bwana John Heche ameridhia kauli ya mwenyekiti Freeman Mbowe ya kufuta na kutupilia mbali swala la kufuta unachama wa chadema kwa wahusika tajwa hapo juu.

Kwa maana hiyo John Heche atatangaza kuwafuta uanachama wa bavicha na sio Chadema.Jambo la kushangaza bavicha inawafuta uanachama watu ndani ya chadema,Kuna fomu au kadi yoyote ya uanachama wa bavicha?.

Pia nitakuja kuleta draft aliyoichora ben saanane namna ya kucheza na huu mchezo wa kufuta wanachama watu kwa mfumo wa "sikutambui" ni fomula iliyotumia south Africa.

Kuna taarifa nitakuwa niki-update hapa kile kinachoendelea,hasa kuhusu tamko la Bw.John heche kuhusu maadhimio mengine yaliyobakia.

Wana JF,

Naomba kuweka kumbukumbu sahihi kuhusu haya yaliyoandikwa na yenye sura ya upotoshaji wa makusudi kabisa. Sikupenda kuongelea mambo haya ila naomba kidogo nijielekeze kwa mambo yanayonihusu na mengine ambayo yanagusa mamlaka fulani nitaiachia mamlaka husika ijibu kwa muda wake (kama inaona kuna ulazima wa kufanya hivyo).

Ni kweli nilialikwa kwenye kikao. Ikumbukwe kwamba kuna kamati ndogo iliyoundwa na kamati tendaji kuchunguza na kutafuta ufumbuzi wa migogoro iliyoanza kujitokeza ndani ya baraza la Vijana. Mimi ni miongoni mwa wale waliohojiwa na kamati hiyo ndogo ambayo kimsingi ilitakiwa kupeleka ripoti yake kwa kamati tendaji . Pamoja na kwamba nilihojiwa lakini hivi karibuni kuna mambo mengi ambayo yameibuka kwa hiyo wale tuliohojiwa tulipewa fursa nyingine ya kusikilizwa tena mbele ya kamati tendaji. Niliitwa kwa njia ya barua, Nilialikwa/tulialikwa! Sikuona ukiukaji wa kanuni, Katiba wala itifaki katika mualiko huo.

Suala la kwamba kuna mgogoro kati ya mwenyekiti wa vijana na Mwenyekiti wa chama hilo silijui lakini nitoe angalizo kwenu wanaJF, Jaribuni kufuatilia historia ya huyu mleta mada kupitia post zake zote za nyuma na mtagundua kwa haraka sana lengo lake ni nini na nilishasema malengo yao hapa ni kutenganisha viongozi ndani ya CHADEMA. Ninamfahamu huyu na yupo kwenye lilie kundi. Nabanwa tu na sheria za JF vinginevyo ningemuanika hapa, wengi wenu mnamjua.

Mambo yaliyopotoshwa:

1: Hakuna mahali popote nilikoomba msamaha kwamba nimemchafua Ndugu Zitto. Sitaingia kwa undani kuhusu mjadala uliofanyika kwenye kikao , nitaiachia mamlaka husika itoe kauli kwa mujibu wa katiba, kanuni na taratibu pamoja na kuzingatia itifaki. Hoja hii imewekwa kwa ajili ya kufanya upotoshaji wa makusudi kwa malengo ambayo wanayajua wao. Narudia tena, sikuwahi kuomba msamaha mahali popote kwamba nimemchafua ndugu Zitto Kabwe. Kuna malalamiko na Maelezo ambayo nilishayapeleka kwa Katibu Mkuu na yapo kwenye mamalaka husika kuhusu jambo hili na nisingependa kulijadili hapa na sitalijadili kwenye kikao chochote kwani mamalaka nyingine tofauti na hiyo ikiwemo ya Vijana inakosa jurisdiction ya kujadili hilo. Namshangaa aliyetunga hadithi hii amekusudia nini hasa!

2: Kuhusu suala la Ulinzi: Ninachofahamu na ninachoelewa ni kwamba pale Mbezi Garden nilikuwa huru na hata wenzangu walikua huru. Huu upotoshaji kwamba kuna watu waliolindwa na wengine kuachwa huru ni muendelezo wa siasa za ghiliba tu. Nilikuwa nimekaa nje karibu na Meza ya akina Mchange, Mwampamba na Gwakisa ambapo baadaye alikuja dereva wa Mh. Zitto Kabwe akajumuika nao na baada ya kuhojiwa waliondoka pamoja huku wakimuacha Gwakisa akiendelea kuhojiwa.

3: Ninachojua ni kwamba kila mtu alihojiwa kwa muda wake. Hadi ninapoandika muda huu sijapokea maamuzi ya kikao hicho! Nilikuwa mtu wa pili kutoka mwisho kati ya wale waliohojiwa.

4: Kikao kiliisha around saa 2: 30 A.M (Saa 8 na nusu usiku) na sio saa sita kama anavyopotosha mleta mada. Huu ni uongo na uzushi wenye muelekeo wa dhamira ovu.

5: ID iliyotumika ningeweza kuiweka wazi hapa lakini kwa kuwa nina wajibu wa kulinda kanuni na sheria za JF ambazo niliridhia kabla sijajiunga, naomba niendeleze ustaarabu huu wa kutotaja aliyeandika haya. Ila kwa muhtasari naomba niwakumbushe kwamba:
ID yenye Jina Taswira ilisajiliwa tarehe 23 December, 2012 baada tuhuma zilizorushwa hapa. Na kila mmoja anajua jitihada za TASWIRA katika kulitetea kundi la MASALIA/PM-7 na harakati za kundi hili. Upotoshaji huu unafanywa kwa makusudi kabisa. Kuna mengi hapa yamepotoshwa lakini nitaachia mamlak
Kutokana na maswali yanayojitokeza humu jamvini nimeona niwawekee video ya Mwenyekiti wa BAVICHA Mh. John Heche akitoa maamuzi ya Kamati Tendaji ya BAVICHA Taifa iliyokutana tarehe 05/01/2013 katika Hotel ya Mbezi Garden iliyopo jijini Dar es Salaam.
BAVICHA yawafukuza Uanachama Watovu wa Nidhamu - YouTube

Heche anadai wakibisha na kujifanya wajuaji atatuwekea video, sauti na mawasiliano yao ya simu.
 
Safi sana cdm endeleeni kufagia uchafu ndani ya chama masalia baibai
 
Nachojua chadema ni chama chenye kujali na pia kina umoja hivyo hili swala likiwa na ukweli au uongo mambo yatakuwa poa tu
 
Angalau umeeleza bila matusi , manake zamani ungetanguliza kutukana Katibu mkuu wa chama na kadhalika mukienda hivyo munaweza kuyamaliza na kusonga mbele na ujenzi wa chama matusi kwa watu wazima na viongozi hata kama hamuwapendi yanatuudhi wapenda mabadiriko huo ndio uwe uamuzi wa 2013 jadili hoja sio watu elezzea mantiki sio matusi elezea ukweli sio uzushi tunasubiri wenzio waje watueleze nao
 
Wengine tutasema kuwa wamekata matawi,mzizi mkuu wameuacha.
 
Ngoja nisubiri upande wa pili maana naona kama umeegemea sana upande mmoja ( Mwampamba na Mchange ).
 
Mi ninavyoelwa ngoma bado nzito kwani watalazimika kuitwa tena kwenye kikao cha kamati kuu kuwajadili kabla ya kutoa hukumu.
 
Kama mbowe ameingilia naamini katiba itafuatwa kama ni wa kufukuzwa watafukuzwa tu!!!
 
Hatari! hatari! kwenye hivi vikao wanaweza hata kukung'oa meno kwa koleo kama si kukuminya sehemu za siri.
 
Umeandika kiushabiki shabiki sana... kama hao masalia wamefukuzwa safi sana....
 
Hadithi yako ni nzuri ila kama ungetumia muda huo kufikiria namna ya kuondoa UMASKINI wa Watanzania na hoja yako ukaipeleka mbele zaidi kwenye vikao vya maamuzi ungeitendea haki sana nchi yako
 
Kwanza kabisa nikupongeze kwa kujitaid kupangilia mawazo yako vizur bwana mwampamba.
Ingekua ni vema ungekuja na id yako coz unaonekana umejikita sana katika kutathmini uovu na haki ktokutendeka katika kikao,ukweli utajulikana tu hata iweje.huwezi ukaniambia umeona uonevu na wewe ulikuwemo humo ukafanya nini.inaonekana wazi wewe unataka kuonesha uma mmeonewa na umesahau unaowadanganya wamekuzidi akili
 
Gwakisa Burton.yeye alikuwa na shitaka moja la kumpinga Dr.slaa kuwa na kadi mbili ya chadema na CCM.
Bila kuchelea Gwakisa kakili kweli alimpinga Dr.slaa,mwenyekiti John heche palepale akaamulu kumsamehe Gwakisa.nakupewa onyo kali la kutorudia tena kuwapinga viongozi wake.

- hillarious1 ha! ha! ha! ha! ha!

le mutuz
 
Back
Top Bottom