G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Kama Juliana Shonza yule wa UDSM niliyekuwa nikimfahamu angeendelea kuwa Chadema basi leo tungekuwa tunaongea mengine.Juliana alikuwa kwa kasi kiwango ambacho hata Halima Mdee hakuanza nacho.
Juliana alikuwa akisimama jukwaani unabaki kuwaza mbali.Juliana alijiamini na kujisimamia.
Tatizo la Juliana Shonza ni moja tu, kukosa uvumilivu kwenye shida. Juliana alianza kuweweseka na vijisenti vya kudanganywa na wanaccm. Alidhani kuwa kwa kufanya hivyo angetengeneza msingi wa kuiua Chadema na yeye kuneemeka kama 'alivyodanganywa'
Majuzi nilikutana na kijana mmoja tuliyesoma wote UDSM ambaye alikuwa rafiki kipenzi wa Juliana. Alinieleza jinsi Juliana anavyojutia kudanganyika.Anajua fika kuwa leo angekuwa mbali sana mithili ya akina Halima Mdee! Anajua jinsi alivyojikosesha nafasi muhimu kwenye jamii. Hilo anajutia na zaidi anavyoiona Chadema ilivyo sasa. Juliana analia jinsi alivyotumika vibaya. Rafiki yake anasema kuwa Juliana anadai kuwa yupo katika njia isiyo na malengo, zaidi isiyoeleweka. Sasa anajiuliza nini afanye? Hiyo nawaachia wana-jf wamjibu.
Mtella Mwampamba naye bila shaka anajilaumu maana huwa tunasema a=b=c. Kwa hiyo bila shaka hilo nalo analo. Tena huyu ndo katelekezwa kabisa. Hana tena nyuma wala mbele.Aliyokuwa akitarajia kwa Chadema ili aneemeke yote yamebuma
Huyu bado sijasikia kutoka upande wake ingawa ni dhahiri ndivyo ilivyo!