Juliana Shonza aendelea kupiga kazi, ataka viongozi wa michezo kuboresha michezo


Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Messages
3,091
Likes
4,085
Points
280
Age
28
Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2014
3,091 4,085 280

Viongozi wa michezo ngazi za mikoa na wilaya wamehimizwa kuhamasisha na kusimamia mchezo wa riadha na michezo mingine katika maeneo yao ili taifa liweze kuwa na wanamichezo bora.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza wakati alipokuwa akifunga mshindano ya mbio za Rock City Marathoni yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Mwanza.

“Viongozi wa michezo ngazi ya mikoa na wilaya mnawajibu wa kuhamasisha mchezo wa riadha katika maeneo yenu ili taifa liweze kuwa na wanamichezo wengi zaidi na bora nchini,” alisema Naibu Waziri Shonza.

Naibu Waziri huyo amewapongeza waandaji wa mbio hizo ambao ni kampuni ya Capital-Plus International Ltd kwa kuwa wabunifu na kufanikisha mashindano hayo kila mwaka ambapo mwaka huu yamebeba dhima ya kujenga taifa kwa kuibua vipaji vya vijana haatua ambayo inatoa fursa ya vijana hao kujiajiri kupitia mchezo wa riadha.

Mashindano ya Rock City Marathon, yamnaendelea kutoa fursa ya kutambua vipaji vya wanariadha wengi zaidi ambao kupitia mashindano hayo wanapata fursa ya kujiajiri, kuinua vipato vyao na uchumi wa taifa pamoja na kuiweka Kanda ya Ziwa katika ramani ya michezo ndani na nje ya nchi.

Aidha, kuhusu ushiriki mdogo wa Watanzania katika mashindano hayo, Naibu Waziri Shonza amewahimiza waandaaji wa mashindano hayo kuyatangaza kwani inaonekana hayajatangazwa vya kutosha ili kupata washiriki wengi wengi zaidi.

“Wakati nakimbia mbio za kilometa tatu, njiani nimewasikia wananchi wakazi wa Mwanza wakisema, kumbe kuna mashindano, ningejua ningejiandikisha kushiriki ili kufanya mazoezi,” alisema Naibu Waziri Shonza.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Riadha nchini ambaye pia na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Athon Mtaka amesema kuwa mbio hizo ni za pili kwa ukubwa Tanzania na zinafanyika kwa mara ya nane mfululizo zikihusisha mbio za Kilometa 42, 21, 05, 03 na kilometa 2.5 ambazo zinawahusisha watoto wadogo.

“Tanzania hatuna wachezaji wengi sawa na Kenya, ili kufuzu kushiriki mashindano ya kimataifa ni lazima mwanariadha aliyeshiriki mashindano ya kimataifa anatakiwa kukaa siku 90 za kupumzika na kuendelea kufanya mazoezi bila kushiriki mashindano mengine,” alisema Mtaka.

Bw. Mtaka alitoa ufafanuzi huo kufuatia wananchi wengi waliokuwepo uwanjani hapo kuhoji na kutaka sababu za mwanariadha Alphonce Simbu kutokuwepo katika mashindano hayo.

Katika mbio za kilometa 42 kwa wanaume wanariadha kutoka nchini Kenya ndio walitawala mbio hizo wakiongozwa na Abraham Too mshindi wa kwaza hadi nafasi ya saba ambapo nafasi ya nane ilishikwa na Mtanzania Paschal Mombo huku upande wa wanawake katika mbio hizo Wakenya wakiongozwa na Gladness Otare.

Mshindano ya mbio za Rock City Marathoni mwaka huu yameongozwa na kaulimbiu inayobeba dhana ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika nchi yetu “Kutangaza vivutio vya utalii kwa njia ya michezo”. Kaulimbiu hii inauunga mkono juhudi za Serikali za kufikia chumi wa kati ifikapo 2025 na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.


Mo Dewji
 
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Messages
21,192
Likes
15,588
Points
280
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2010
21,192 15,588 280
Kwa budget ipi?
 
Dragoon

Dragoon

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2013
Messages
7,076
Likes
7,401
Points
280
Dragoon

Dragoon

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2013
7,076 7,401 280
Jiwe walilolikataa waashi.......
 
The Tomorrow People

The Tomorrow People

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2013
Messages
2,455
Likes
1,943
Points
280
The Tomorrow People

The Tomorrow People

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2013
2,455 1,943 280
Asante Juliana Daniel Shonza.... Chapa kazi.
 

Forum statistics

Threads 1,250,869
Members 481,514
Posts 29,748,969