Magna Carta
JF-Expert Member
- Jul 14, 2014
- 4,335
- 6,617
Nasikia kuna ajali.nyingine ya lori la mafuta Kilimanjaro, raia wametimuliwa na polisi
Kilema cha kudumu!Kwa mawazo yangu hakuna haja ya kushtakiwa kwa kua adhabu ya moto imetosha
Leo lori la mafuta,kesho utapinduka na bus badala ya kusaidia watakuja kukuibia na kukuacha ufe.Balile anajipendekeza, bila shaka anatafuta uteuzi. Kwa umaskini wa watanzania uliopo ktk awamu hii alitegemea wananchi wafanye nn?
Ama kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa!
We uko na majonzi gani saa hizi? Au umepoteza nini mpaka washtakiwe?Ni sahihi kabisa kwani wameingiza taifa na familia zao kwenye majonzi yasiyokuwa ya ulazima!
Kuna mengi sana ya kusema ambayo ni ya wazi. Wamefanya uvivu wa kufikiri kuandika jambo linaloweza kuitwa "blaming the victim".......nyie TEF, ni mapema sana kutoa kauli kama hizi.
Na msiishie tu katika kusema washitakiwe majeruhi, semeni pia na suala la kukosekana kwa vifaa vya kutosha vya zimamoto, madereva kutotoa nafasi ili ambulance ipite.
Umaskini (usifikirie ukosefu wa chakula na ajira tu, bali umaskini kwa maana ya kukosa taarifa muhimu kwa mtu mmoja mmoja na umma wote).
.....hili janga halitakuwa la mwisho na likitokea tena, watu wataenda 'kuokota' mafuta. Kama mkate hunapatikana kwa shida, wachache watatafuta makombo
Una kipimo cha kupimia majonzi? Walichokuwa wanakifanya kilikuwa halali? Roho zilizopotea zilihitajika sana kwenye nyuvu kazi ya taifa! Majeruhi wanapaswa kuwajibishwa hata kama hawakujua kwamba walichokua wakikifanya ni uhalifu!We uko na majonzi gani saa hizi? Au umepoteza nini mpaka washtakiwe?
Vipi waliokuwa wanawaokoa waliokuwa ndani ya cabin? vp wapita njia?Una kipimo cha kupimia majonzi? Walichokuwa wanakifanya kilikuwa halali? Roho zilizopotea zilihitajika sana kwenye nyuvu kazi ya taifa! Majeruhi wanapaswa kuwajibishwa hata kama hawakujua kwamba walichokua wakikifanya ni uhalifu!
walienda kuangalia Nini? Hawakujua madhara ya petroli? Walitakiwa wakimbie mbali sio kusogea kushuhudiaSidhani kama walioiba mafuta wamepona.
Hao ni wale wa pembeni wapita njia au walikwenda kuangalia na inawezekana walikuwa wamekaa mbali
Huo ndoukweli tubadilikeJukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kushtushwa na taarifa za vifo vya Watanzania zaidi ya 60 walioungua moto wakati wakichota mafuta kutoka katika lori lililopata ajali eneo la Msamvu, Morogoro, jana Agosti 10, 2019 likitaka waliojeruhia kushitakiwa watakapopona majeraha yao.
Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana usiku Jumamosi na Kaimu Mwenyekiti Jukwaa hilo, Deodatus Balile ilisema vifo hivyo vimetokana na tabia mbaya iliyojengeka kwa baadhi ya watu kuchukulia ajali kama fursa ya kujipatia mali kwa njia haramu iliyoanza miaka ya hivi karibuni.
“Tumeshuhudia picha za watu waliofariki kwa kuungua moto zikirushwa kwenye mitandao ya kijamii kinyume cha maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na upashanaji habari. Tunakemea tabia hii na kuitaka jamii iache mara moja tabia hii ya kinyama isiyo ya utu,” alisema Balile.
Balile pia alizungumzia watu zaidi ya 70 waliojeruhiwa katika ajali hiyo akisema wakipona wajiepushe na tabia hii ya uporaji.
“Ikilazimu, wote watakaopona katika ajali hii washitakiwe kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwao na wengine kuwa ikitokea ajali tunapaswa kusaidia majeruhi na kuokoa mali zao badala ya kupora,” alisema.
“Tunaomba viongozi wa dini, wazazi, viongozi wa kisiasa na jamii kwa ujumla itumie ajali hii kufundisha watoto na vijana maadili mema ya kuwa watu wa msaada mtu anapopata ajali kwa kusaidia majeruhi na kuokoa mali za waliopata ajali badala ya kuwapora,” aliongeza.
Hadi jana usiku, watu 64 walikuwa wameripotiwa kufariki huku 70 wakijeruhiwa ambapo baadhi ya majeruhi wamelazwa Hospitali ya Morogoro na wengine wakihamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Chanzo: Mwananchi