Jukwaa la Wahariri(TEF), lataka majeruhi ajali ya moto Morogoro washitakiwe

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kushtushwa na taarifa za vifo vya Watanzania zaidi ya 60 walioungua moto wakati wakichota mafuta kutoka katika lori lililopata ajali eneo la Msamvu, Morogoro, jana Agosti 10, 2019 likitaka waliojeruhia kushitakiwa watakapopona majeraha yao.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana usiku Jumamosi na Kaimu Mwenyekiti Jukwaa hilo, Deodatus Balile ilisema vifo hivyo vimetokana na tabia mbaya iliyojengeka kwa baadhi ya watu kuchukulia ajali kama fursa ya kujipatia mali kwa njia haramu iliyoanza miaka ya hivi karibuni.

“Tumeshuhudia picha za watu waliofariki kwa kuungua moto zikirushwa kwenye mitandao ya kijamii kinyume cha maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na upashanaji habari. Tunakemea tabia hii na kuitaka jamii iache mara moja tabia hii ya kinyama isiyo ya utu,” alisema Balile.

Balile pia alizungumzia watu zaidi ya 70 waliojeruhiwa katika ajali hiyo akisema wakipona wajiepushe na tabia hii ya uporaji.

“Ikilazimu, wote watakaopona katika ajali hii washitakiwe kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwao na wengine kuwa ikitokea ajali tunapaswa kusaidia majeruhi na kuokoa mali zao badala ya kupora,” alisema.

“Tunaomba viongozi wa dini, wazazi, viongozi wa kisiasa na jamii kwa ujumla itumie ajali hii kufundisha watoto na vijana maadili mema ya kuwa watu wa msaada mtu anapopata ajali kwa kusaidia majeruhi na kuokoa mali za waliopata ajali badala ya kuwapora,” aliongeza.

Hadi jana usiku, watu 64 walikuwa wameripotiwa kufariki huku 70 wakijeruhiwa ambapo baadhi ya majeruhi wamelazwa Hospitali ya Morogoro na wengine wakihamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Chanzo: Mwananchi
 
......nyie TEF, ni mapema sana kutoa kauli kama hizi.
Na msiishie tu katika kusema washitakiwe majeruhi, semeni pia na suala la kukosekana kwa vifaa vya kutosha vya zimamoto, madereva kutotoa nafasi ili ambulance ipite.

Umaskini (usifikirie ukosefu wa chakula na ajira tu, bali umaskini kwa maana ya kukosa taarifa muhimu kwa mtu mmoja mmoja na umma wote).

.....hili janga halitakuwa la mwisho na likitokea tena, watu wataenda 'kuokota' mafuta. Kama mkate hunapatikana kwa shida, wachache watatafuta makombo
 
Vipi kuhusu waandishi wanaodai/wanaopewa bahasha ili waripoti/wasiripoti matukio kasemaje? Nyani asiyeona nyuma yake.
 
Sidhani kama walioiba mafuta wamepona.
Hao ni wale wa pembeni wapita njia au walikwenda kuangalia na inawezekana walikuwa wamekaa mbali
 
ila wangesubr kwanza wauguze majeraha then km sheria inasema hvyo basi sawa,

serikali iwajibike nao wawajibike(ila ijulikane sio wote walikua wanachota hayo mafuta),

kuna mabo manne au zaid kunapotokea janga km hili, na henda kwa mtitririko

sheria,
je sheria inasemaje mtu akifanya kosa km hilo?

haki,
haki za mtu aliepata majanga km haya pasipokujali amejitakia mwenyewe au laa!

wajibu,
wajibu wa serikali katika kuzuia, kusaidi na kupambana na majanga km haya pasipo kujali chanzo,

huruma na ubinadamu,
huruma na ubinadamu kumsaidia bila manyanyaso kwa mtu aliepatwa na tatzo km hili pasipo kuangalia kisababishi kwanza.

Usiruhusu chochote kati ya hivyo kimzidi mwenzakee, na haviwezi kufanyika vyote kwa wakati mmoja,
 
Mmmh!!! Mimi napingana nao. Hao majeruhi wengine ni wapita njia. Wezi ni hao waliofariki maana ndio waliokuwa karibu na mlipuko.

Majeruhi ni watu waliokua mbali na mlipuko kwa jina lingine naweza waita mashuhuda.
Wasiwafanye wajinga na kujiona wao ndo welevu. Badala ya kuwapa pole wao wanaleta upumbavu
 
Sijaona mtu yeyote alohoji kwa nn police hawakuenda kuwatawanya watu wanaochota mafuta.
Moto haujalipuka tu baada y lori kuanguka, kulikua na muda mwingi tu. Kuna baadhi walirudia hadi tripu ya pili kuchota ndio moto umezuka sasa muda wote police wa pale msamvu walikua wapi?.
Kuna kipindi nilishuhudia askari wakiwatawanya watu kweny ajari ya gari la bia yaan ilikua risasi mbili tu za hewani hakuna raia ilebaki pale.
Police wangewahi ingewezekana kupunguza athari au kuzuia kabisa
 
Back
Top Bottom