Jukwaa la Wahariri lalaani kufungiwa kwa Radio 5 na Magic FM

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
IMG-20160830-WA0044.jpg
Hayo wamesema leo Fwatilia

=======

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limetoa tamko na kusema kuwa limeshtushwa na kusononeshwa kutokana na hatua ya Serikali kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuvifungia kwa muda usiojulikana vituo viwili vya redio.

Vituo vilivyofungiwa ni Radio 5 ya Arusha na Magic FM ya Dar es Salaam, uamuzi ambao ulitangazwa juzi.

Tamko hilo la TEF lilitolewa jana Dar es Salaam na Katibu wa jukwaa hilo, Neville Meena.

Alisema kwa muda wa miezi takriban kumi tangu alipoteuliwa kuwa waziri, Nape amejitokeza mara nne na kutangaza kufuta na kufungia vyombo vya habari.

“Alianza kulifuta Gazeti la Mawio, baadaye alitangaza kufuta mamia ya magazeti na majarida ambayo hayajachapishwa kwa muda mrefu, ikafuata adhabu ya kulifungia kwa miaka mitatu Gazeti la Mseto na sasa vituo viwili vya redio.

“Katika tukio la kufutwa kwa Mawio, tulihoji ukubwa wa kosa la gazeti hilo kiasi cha kufutwa. Leo hii tunahoji tena ukubwa wa makosa na pengine historia ya redio husika siku zilizopita. Ndiyo maana tunasema hili la sasa ni mwendelezo wa ukandamizaji wa uhuru wa habari.

“TEF inachukulia hatua hii kama mwendelezo wa ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari nchini na tunashindwa kuelewa dhamira ya Serikali ya awamu ya tano kwa sekta ya habari nchini. Kinachoonekana ni kutumia kila aina ya sheria iliyopo kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Kimsingi TEF hatuoni nia (spirit) ya malezi katika uamuzi wa waziri huyo,” alisema Meena.

Kutokana na hali hiyo, alisema msimamo wa TEF, unasikitishwa na utaratibu uliotumiwa na waziri kufikia uamuzi huo, umekuwa wa makosa yaleyale ya siku zote.

“Pamoja na kwamba vyombo vya habari hufanya makosa, lakini hata pale makosa yanapotokea taratibu za kuyashughulikia lazima zizingatie misingi ya utawala bora, haki na demokrasia.

“Mfumo wa kushughulikia matatizo au kasoro za kitaaluma katika vyombo vya habari ni kandamizi kwani unamfanya waziri kuwa na mamlaka ya kutoa adhabu kwa kuzingatia mtizamo wake, hata kama mtizamo huo unakinzana na misingi ya taaluma,” alisema.

Meena alisema kuwa uamuzi wa Waziri Nape unaonekana hauna nia njema ndani yake kwani kifungu cha 28 cha sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) alichotumia kutoa adhabu hiyo, hakimlazimishi kufungia vituo vya redio kama alivyofanya.

“Kosa la vituo hivyo kwa mujibu wa waziri ni uchochezi, lakini hakuweka bayana maudhui ya vipindi au habari ambazo zilivifanya vituo hivyo ‘kutiwa hatiani’ na baadaye kufungwa kwake kwa muda usiojulikana. Kwa sababu hiyo si rahisi kwa waandishi wengine wa habari kujifunza kwa makosa ya wenzao kwa kuwa mchakato uliotumika kushughulikia suala hilo umebaki kuwa siri ya waziri.

“Tunapinga uamuzi wa Serikali kuvifungia vituo hivyo bila sababu na tunatoa mwito kwa Waziri Nape kutafakari upya suala hili na kuachana kabisa na dhamira hiyo isiyokuwa na tija kwa nchi yetu,” alisema Meena.


Chanzo: Mtanzania
 
Hivi nini hua kinafuata baada ya tamko la kulaani?
Yaani baada ya jukwaa la wahariri kulaani, je nini hua kina fuata baada ya laana hiyo?
Nawakilisha
 
basi mmeshia hapo tu hakuna hatua yoyote ya maana zaidi ya hayo matamko,chukueni hatua zaidi ya hizo mnaweza lakini kwa vile hamna umoja zaidi ya matamko ni sawa na nyoka wa kibisa tu
 
Nasikia walikosoa bila kutaja vifungu vya sheria wala katiba...naona waziri kawa'kongoli' kimya kimya bila...maji ya kunywa.
==============
Andikeni na Tangazeni kwa weledi ili muepuke adha hizi. Kama unaona kiwango chako hakiridhishi katika fani ongeza ujuzi. Kuna Mhariri wa Gazeti la Jamhuri aliona kazi yake inahitaji elimu ya sheria aliamua kujiunga chuo kikuu cha Dar es Salaam na kupata ujuzi huo....sidhani kama Mhariri huyo kashawahi kuiingiza Jamhuri kwenye mikasa kama ya hawa wa Magic FM
 
Na mimi natumia ule msamiati wa UKUTA fam ...njaa mbaya.
Hawa nao...Kila siku tunalaani tunalaani,Laana kila siku kwani wamekuwa Wazee.Chukueni hatua dhidi ya hao Mabwana achaneni na matamko.Watakufungieni mpaka ninyi sasa.......
 
Baada ya kukemea nini kitatokea? Kila mara huwa wanakemea halafu basi, serikali imezoea makemeo yao. Hawa ni sawa na wale wa haki za binadamu wanaishia kukemea kwenye vyombo vya habari basi na mambo ya kijinga yanaendelea kutokea.
 
At least wameonesha msimamo wao kwenye hilo sakata.. Huu ni uonevu wa wazi wazi
Msimamo wa kiuoga namna hii hausaidii chochote. Hii ni hadithi ya mtu anakuja anachukuwa mali zako na wewe badala ya kuchukua hatua unabaki kulaani. Laana haipati wanasiasi. Wangekuwa wanapata laana basi mtu kama Shein anayepora kura mchana kweupe asingekuwa na kidole hata kimoja. Vyote vingekuwa vimekatika kwa laana.
 
INGEKUWA VYEMA KAMA WANGECHUKUA HATUA NA SIYO KUTOA MATAMKO.

TUMESHACHOKA NA MATAMKO YA KILA MARA.
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!​
 
Wanabodi
Salaam;

Nimeona tamko la jukwaa la wahariri nchini waki-laani kitendo cha waziri wa habari utamaduni na michezo kuvifungia vituo vya Radio magic fm na Radio 5.

Sioni maantiki ya tamko lao km hawachukui hatua za kupigania uhuru wao. Kwa hali ilivyo,huyu jamaa ataendelea kufungia vyombo vya habari vyote vinavyokinzana na serikali.

Nawashauri wasusie kuandika habari zote zinazohusu wizara hiyo. Na si kumsusia tu,ili habari ziweze kuripotiwa tena,apewe masharti ya kufungulia magazeti na radio zote alizofungia.

Naamini hili linawezekana,na Nape afungiwe maisha kuandikwa habari zake kwenye media. Nakumbuka Omary Ramadhan Mapuri aliwahi kususiwa na wanahabari na mpaka leo hakuna ajuaye alipo huyu mzee.

Vinginevyo waandishi mkubali kuandika habari wanazotaka wao. Kifupi mkubali kutumika..!

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom