Jukumu la nani kulipia mahari?

Jukumu la nani kulipia mahari?

mmp

Member
Joined
Sep 10, 2014
Posts
33
Reaction score
2
Habari wa kuu, samahan mm nina maswali yafuatayo ninaomba nielimishwe hivi ni yupi anaepaswa kulipia gharama(mahari,pete ya uchumba,nauli ya kwenda na kurudi kama wanaishi mbali,na huduma ndogo ndogo) zote mpk kufikia ndoa baina ya wachumba wawili wenye malengo ya kuoana, namanisha msichana na mvulana?
 
mvulana ndie mwenye jukumu hilo (kwa imani yangu mimi)
 
Kwa Wahindi Mwanamke Ndo Hutoa Mahari Kwa Mwanaume Pindi Anapohitaji Kuolewa Ila Kwa Tamaduni Za Watu Wengine Mwanaume Ndo Anasimamia Kila Kitu
 
Show ya mwanaume mwanzo mwisho. Onyesha uanaume
 
Asanten Wakuu Lakin Yeye Hawez Kukusaidia Hata Kanauli Ili Muonane?
 
Asanteni Kwa Kunipa Mwanga.Mfano Yeye Anakazi Na Anadai Ni Mtumie Vocha Je Nihaki Kwel??
 
Mahari ni zawadi kutoka Kwa mume anamzawadia mkewe haijalishi ni kitu gani, inaweza kua dhahabu pesa au vyote, kuhusu usafiri inategemea huyo mkeo mtarajiwa wakoje kimshiko, mnaweza mkakaa pamoja mkasaidiana gharama lakini kwakua wewe ndio unaenda kumchukua mkeo itabidi utoe...
 
asante mkuu,mfn Yy Anakaz Na Anaomba Nimtumie Vocha Je Nihaki Kumtumia?
 
Jukumu ni la anayeoa..kama unataka kusaidiwa mapema hii inakuwa ni aibu kwako..jikaze mtoto wa kiume...majukumu madogo sana yanaanza kukushinda..niliwahi kumwambia rafiki yangu mmoja kwamba...wazee wetu walioweka utaratibu wa mahari walifikiria mbali sana...kama kijana mahari yatamshinda basi hawezi kuoa..nikimaanisha kwamba hawezi kumtunza/kumgharamia mwanamke..hivyo basi asiyeweza/anayehitaji kusaidiwa kulipa mahari..atahitaji pia kusaidiwa kumtunza mke wake...angalia usije ukawa mzigo kwa mke wako..
 
komaa kaka...!
hilo hilo ni jukum lako mwanzo mwisho mpaka chombo kimefika ndani..!
 
Asante Anrango, Hapa Nimekua Mwelewa Sasa Kumbe Nisiuonyeshe Udhaifu Wangu
 
Asante Anrango, Hapa Nimekua Mwelewa Sasa Kumbe Nisiuonyeshe Udhaifu Wangu

Sawa..na kwa mahari pamoja na logistics za siku hizi kuanzia engagement mpaka kuoa ..jipange uwe na minimum cash Tsh 3.5m
 
Habari wa kuu, samahan mm nina maswali yafuatayo ninaomba nielimishwe hivi ni yupi anaepaswa kulipia gharama(mahari,pete ya uchumba,nauli ya kwenda na kurudi kama wanaishi mbali,na huduma ndogo ndogo) zote mpk kufikia ndoa baina ya wachumba wawili wenye malengo ya kuoana, namanisha msichana na mvulana?

Jukumu la kutoa MAHALI ni la MWANAUME na sio mvulana au msichana.
 
Back
Top Bottom