Juhudi za CCM kumbeba Magufuli zimezidi kugonga Mwamba

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
12,152
Reaction score
44,110
CCM iko kwenye wakati mgumu sana kisiasa baada ya kugundua kuwa mgombea wake wa Urais John Pombe Magufuli sio mtu mwenye nguvu na ushawishi mpana katika siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.

Habari za ndani ya CCM zinasema kuwa makada wengi wa CCM wana wasiwasi mkubwa sana kuhusu uwezo wa Magufuli kuweza Kuivusha CCM October kwa kuwa mpaka sasa Upepo wa kisiasa bado umeshindwa kuvumishwa ipasavyo na Magufuli.

Hatua hizi kadhaa zimeshafanyika ili kumpa Publicity Magufuli lakini hazijazaa matunda.
1/Kumtambulisha Magufuli katika mikoa mbalimbali.

2/Serikali nzima ya sasa ikiongozwa na Kikwete kumsindikiza kuchukua Fomu ya kugombea urais.

3/Vipindi vingi vya Television na Radio vyenye kuonyesha kazi na maisha ya Magufuli.

4/Ufunguzi wa ujenzi wa barabara mbalimbali nchini.

5/Hafla kubwa na wasanii wa Bongo katika ukumbi wa Mlimani City iliyogharamiwa kila kitu na serikali kupitia Ikulu.

CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA.
(A)Muingiliano wa ratiba ya Magufuli ya matukio ya kiserikali, kiCCM na kijamii. (Hakuna ratiba kamili, kila linalopangwa na CCM linakinzana na ratiba nyingine za Magufuli)

(B)Kukosekana kwa Timu maalum ya kuratibu hizo shughuri za kisiasa za Magufuli. Wakati CCM ina ratiba zake, January Makamba anataka apewe hilo jukumu binafsi la kusimamia kwa madai anauzoefu mkubwa katika hayo mambo. Bahati mbaya sana Magufuli hapendi kabisa mfumo wa Makamba.

(C)Ubishi binafsi wa Magufuli. Magufuli amekuwa akipinga utaratibu wa kupangiwa ratiba ya matukio pasipo kuulizwa kwanza.(mfano ni lile tukio la kususia kwenda kufungua michuano ya Kagame, na badala yake aliamua kwenda Mwanza)

(D)Mlolongo wa kiitifaki uliopo sasa katika maisha ya Magufuli
(Kwa sasa anaongozwa na kulindwa na maafisa usalama wa serikali na hivyo utaratibu wa kupanga ratiba zake za kisiasa unataka uchunguzi wa kiinteligensia, kitu ambacho kinachukua muda kidogo)

(E)Baadhi ya wagombea wa CCM waliokatwa kwenye mbio za urais kususa, kukaa kimya au kuonyesha kutoridhishwa na mchakato(Hapa wanatajwa Lowassa(Huyo ameshahamia UKAWA lakini hakuwahi kuonyesha kukubali uteuzi wa CCM Dodoma), Mizengo Pinda, Samweli Sitta, Mark Mwandosya nk. Hii imepelekea Kikwete ndio awe mstari wa mbele kumshika Magufuli mkono na kumtembeza mitaani.
 
Huu ni mwanzo tu, Tunasubiri tarehe 25 Oct, Asubuhi.
 
Ndani ya ccm kuna vijana na wazee wetu watiifu kupita maelezo! CCM pisheni njia, mtanyooka tu!
 
Lowasa ni babu katika siyasa lakini nayeye aliyojuwa huko kujifunza nayeye magufuli a
 
Mzee magufuli ni mchapa kazi ila kama nilivowahi kusema 2013 ....magufuli anafaa kuwa waziri mkuu ..urais hapana!!
 
Hauziki Magufuli....he is not marketable...!!!

CCM hata sura zao zinaonyesha washashindwa....

Lowassa, Ukawa ni mpango wa Mungu..."!!!

Magufuli, CCM wataanguka vibaya sana sanaaa, hawana jinsi....jaribuni kupita pita mitaani, vijijini, mijini, kwa waalimu, wafugaji, wana vyuo, machinga, bodaboda, wakulima, wafanyakazi, wakristo, waislam, Zanzibar, UVCCM, BAVICHA, CCM, UKAWA, UWT, yaani 85% kura ni Lowassa, ukawa tu...ulizieni...

Sioni CCM pa kuponea... sioni...Magufuli hajui SIASA....as well wananchi washapoteza Imani sana na CCM, na JK, so kumuuza Magufuli ni ngumu mnoooo...

Hali ni mbaya CCM kuliko tujuavyo....!!
 
kiukweli makufuri amekosa support kutoka kwa watia nia wenzie kutoka ccm km tulivyozoea baada ya kura za maoni wote waliungana kumsaidia aliyeteuliwa na chama
 
Hauziki Magufuli....he is not marketable...!!!

Angekuwa hauziki UKAWA wasingewakata Dr. Slaa na Lipumba.

Mwenyekiti wa Chadema amekiri hadharani kuwa hawana mgombea wa kushindana na Magufuli.

Kitendo cha kumchukua Lowassa kimelenga kupata pesa za kampeni tu kwa sababu Mbowe hataki kitumia pesa zake kwenye mradi anaojua utafeli...
 
CCM iko kwenye wakati mgumu sana kisiasa baada ya kugundua kuwa mgombea wake wa Urais John Pombe Magufuli sio mtu mwenye nguvu na ushawishi mpana katika siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.

Habari za ndani ya CCM zinasema kuwa makada wengi wa CCM wana wasiwasi mkubwa sana kuhusu uwezo wa Magufuli kuweza Kuivusha CCM October kwa kuwa mpaka sasa Upepo wa kisiasa bado umeshindwa kuvumishwa ipasavyo na Magufuli.

Hatua hizi kadhaa zimeshafanyika ili kumpa Publicity Magufuli lakini hazijazaa matunda.
1/Kumtambulisha Magufuli katika mikoa mbalimbali.

2/Serikali nzima ya sasa ikiongozwa na Kikwete kumsindikiza kuchukua Fomu ya kugombea urais.

3/Vipindi vingi vya Television na Radio vyenye kuonyesha kazi na maisha ya Magufuli.

4/Ufunguzi wa ujenzi wa barabara mbalimbali nchini.

5/Hafla kubwa na wasanii wa Bongo katika ukumbi wa Mlimani City iliyogharamiwa kila kitu na serikali kupitia Ikulu.

CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA.
(A)Muingiliano wa ratiba ya Magufuli ya matukio ya kiserikali, kiCCM na kijamii. (Hakuna ratiba kamili, kila linalopangwa na CCM linakinzana na ratiba nyingine za Magufuli)

(B)Kukosekana kwa Timu maalum ya kuratibu hizo shughuri za kisiasa za Magufuli. Wakati CCM ina ratiba zake, January Makamba anataka apewe hilo jukumu binafsi la kusimamia kwa madai anauzoefu mkubwa katika hayo mambo. Bahati mbaya sana Magufuli hapendi kabisa mfumo wa Makamba.

(C)Ubishi binafsi wa Magufuli. Magufuli amekuwa akipinga utaratibu wa kupangiwa ratiba ya matukio pasipo kuulizwa kwanza.(mfano ni lile tukio la kususia kwenda kufungua michuano ya Kagame, na badala yake aliamua kwenda Mwanza)

(D)Mlolongo wa kiitifaki uliopo sasa katika maisha ya Magufuli
(Kwa sasa anaongozwa na kulindwa na maafisa usalama wa serikali na hivyo utaratibu wa kupanga ratiba zake za kisiasa unataka uchunguzi wa kiinteligensia, kitu ambacho kinachukua muda kidogo)

(E)Baadhi ya wagombea wa CCM waliokatwa kwenye mbio za urais kususa, kukaa kimya au kuonyesha kutoridhishwa na mchakato(Hapa wanatajwa Lowassa(Huyo ameshahamia UKAWA lakini hakuwahi kuonyesha kukubali uteuzi wa CCM Dodoma), Mizengo Pinda, Samweli Sitta, Mark Mwandosya nk. Hii imepelekea Kikwete ndio awe mstari wa mbele kumshika Magufuli mkono na kumtembeza mitaani.

Ni kweli kabisa
 
Hauziki Magufuli....he is not marketable...!!!

CCM hata sura zao zinaonyesha washashindwa....

Lowassa, Ukawa ni mpango wa Mungu..."!!!

Magufuli, CCM wataanguka vibaya sana sanaaa, hawana jinsi....jaribuni kupita pita mitaani, vijijini, mijini, kwa waalimu, wafugaji, wana vyuo, machinga, bodaboda, wakulima, wafanyakazi, wakristo, waislam, Zanzibar, UVCCM, BAVICHA, CCM, UKAWA, UWT, yaani 85% kura ni Lowassa, ukawa tu...ulizieni...

Sioni CCM pa kuponea... sioni...Magufuli hajui SIASA....as well wananchi washapoteza Imani sana na CCM, na JK, so kumuuza Magufuli ni ngumu mnoooo...

Hali ni mbaya CCM kuliko tujuavyo....!!
Magufuli ni mwanasiasa aliyefilisika kifikra
 
Ccm omelet a watu kwa huruma kama huyu shekhe kwa ni wapi??😷kama sikosei ni comoro au lamu mombasa sasa hapa tz ameingiya amejiridhisha yeye ni mzaliwa wa hap 'tutaacha kutukanwa?huruma ikizidi mbaya sana
 
na leo yuko Lindi saa mbili alikua anapokelewa ofisi za chama
 
Naweza kusema mpk Ccm ikikaribia uchaguzi so chama was Kikwete mifuko itakua mikavu. Kutokana na nguvu kubwa watakayoitumia
 
Back
Top Bottom