MLUMENDAGU
Senior Member
- Oct 31, 2014
- 183
- 31
Mimi Joseph Mungai sijawahi kuyasema maneno hayo ambayo yanapotosha ukweli. Mimi nilikuwa Waziri wa Elimu kwa miaka mitano (5) 2000-2005; na SIYO kwa miaka minane (8). Mipango muhimu niliyoisimamia ni MMEM (Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi) 2002-2007) & MMES (Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Sekondari) 2004-2009.
MMEM ililenga ELIMU BORA YA MSINGI KWA WOTE katoka 56% wa miaka 7-13 waliokuwa Shuleni Mwaka 2000!! Mafanikio uandikishaji ulifika ZAIDI ya 98%; na kufaulu Darasa la VII kuliongezeka kutoka 19% Mwaka 1999 hadi 62% mwaka 2005.
MMES ulikenga kupanua Elimu ya Sekondari iweze kupokea 50% ya wahitimu wa Darasa la Saba. Kwa hiyo MMES niliyoisimamia Mimi chini ya Rais Mkapa haikuwa na mkakati wa Sekondari za Kata. Mafanikio yalikuwa ongezeko la wanafunzi wa Sekondari zaidi ya maradufu 2005 na Aidha ongezeko la zaidi ya 30% kufaullu Div I-III Kitova 10%.
Msukumo wa Sekondar za Kata ulianzishwa na Serikali ya Awmu ya Nne ambamo Mimi nilikuwa kwanza Waziri wa Kilimo na baadaye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Aidha Chuo Kikuu cha Dodoma kimeanzishwa na Serikali ya Awamu us Nne.
Ni ukweli usiokwepeka kwamba msukumo wa Sekondari za Kata na Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma ULIONGOZWA kwa juhuhudi kubwa sana na Waziri Mkuu wa wakati huo Mhe Edward Liwassa. Haifai kupingana na ukweli ambao tuliuona na wengine tulishiriki. Sipendi mtu yeyote kunisemea wakati Mimi mwenyewe bado nipo
J J Mungai
Wazir wa Elimu (2000-2005)