Judge Warioba ateuliwa kuwa Mwenyekiti Tume ya Katiba

JK is not NOT an angel. Kajitahidi kwa kuunda tume ila namshauri asichakachue mapendekezo yao.
 
Great Thinkers,

Ni mshangao ilioje kwa baadhi yetu kushindwa hapa kuona hoja ya msingi zaidi vile! Heshima ya Jaji Warioba wala haina maswali LAKINI ukweli wa mambo ni kwamba uteuzi wake ni wa kisheria na utendaji wake kazi vile vile utafuata mkondo huo huo.

La kujiuliza hapa ni kwamba NANI huyo anayempa mwongozo wa kazi katika tume ile? Naam, swala hapa si IMANI TU na mtu gani atakayekalia kiti hicho bali swala zima la kukodolea ma ni je
HADIDU ZA REJEA atakazotumia kama mwongozo wake wa kazi zinapatikana kutoka kwa nani?

Ni kutoka kwa SISI WANANCHI au ni kutoka kwa SERIKALI kwa maana ya CCM?

kama tuna imani na WARIOBA kwa nini tusiwe na imani na aliemteua?.uteuzi wa tume hii nzuri ni ushahidi tosha kuwa mteuzi anayo nia SAFI na NJEMA.Sidhani kama RAIS kaunda tume hii ili kesho imletee mapendekezo ayachakachue yy na mama salma na riz.tuache hisia mbovu tutakonda kwa hisia za ajabu.kikwete hongera sana kwani unazidi kututendea mema.
 
Kwa upendeleo huu wa KIDINI JK atarajie upinzani kwa wakristo.

Mkuu wangu hakuna upendeleo.Sheria inasema Zanzibar iteue wajumbe 15 na bara 15.Sasa mkuu kwa Zanzibar ni lazima wote wawe waislam.Tuache visingizio tumpongeze kwa hili.
 
not so good ....not so bad .... lets wait ... hapo kuna manguli wa constitutional Law
 
Kwa upendeleo huu wa KIDINI JK atarajie upinzani kwa wakristo.

Mkuu wangu hakuna upendeleo.Sheria inasema Zanzibar iteue wajumbe 15 na bara 15.Sasa mkuu kwa Zanzibar ni lazima wote wawe waislam.Tuache visingizio tumpongeze kwa hili.
 
Jmushi1,

Issa Shivji kwa weledi wake asingestahili kuachwa. Jenerali Ulimwengu, Kibamba kutoka asasi za kiraia na Prof. Abdala Safari wasingeachwa. Labda tuungane nao nje ya Tume ili tuunde parallel commission ya kuikosoa tume iliyoteuliwa

Mkuu Ben,
Hoja nzito sana hii Mkuu!
 
Sasa mbona wazee tupu?

tena ndio wale wale waliotufikisha hapa tulipo..
 
Daaah JK mbona umenipa raha sana.yaaani kwa mara yakwanza nimekupenda JK..warioba,mwesiga,mvungi,salim!!! Daaah mungu atupe nini sasa ..
 
Wapi prof Safari, Shivji, Jenerali Ulimwengu, Ananilea Nkya kidogo hawa hawana nidhamu ya woga ila sio mbaya is a good begining... Na je waislamu tutapata haki yetu? Kwa tume sidhani! Ila sijui

Haki gani tena mnayotaka waislamu jamani? Hapa tunachotaka ni maslahi ya nchi kwa wananchi wote bila kujali dini ya mtu. Assumption ni kuwa nchi haina dini ila wananchi wake wana dini zao. Waachwe wapange mipango yako wenyewe, waabudu kwa uhuru bila kubughudhiwa ila wasivunje sheria, na dini za mashetani zenye kuhatarisha amani na usalama wa raia zisiruhusiwe.
 
Kuuvunja muungano!
 
Sasa mbona wazee tupu?

tena ndio wale wale waliotufikisha hapa tulipo..

Mkuu hapo ni kweli. Hii katiba inatakiwa itupeleke miaka 50 mbele kama alivyosema Rais lakini mbona imesheheni wazee ambao sina hakika kama wana miaka 10 mbele!
 
Wapi prof Safari, Shivji, Jenerali Ulimwengu, Ananilea Nkya kidogo hawa hawana nidhamu ya woga ila sio mbaya is a good begining... Na je waislamu tutapata haki yetu? Kwa tume sidhani! Ila sijui

Mkuu kwa Prof. Safari ni bora hayumo. Huyu ni mojawapo wa wasomi wa kiislamu wenye misimamo mikali (radical islams) na inaitaka sana makahakama ya kadhi, so ni bora hayumo.
 
Well done your excellency president Kikwete, in support of private candidate for the presidential election 2015!!
 
, naona amewapiga plasta za mdomo akina butiku maana hivi vibabu vimefulia kinoma so ameamua avipe shavu walau vilambe per diem ya trip za mikoani viache kutema povu,JK alishasema haiwezekani kila mnaemtaka akawemo akina Shivji,ulimwengu,Nkya,kisimba, wanaweza kuwa wabunge wa bunge la katiba,kweli JK ni messi wa siasa za kibongo as tulipinga sana yeye kuteua hii timu lakin leo tunakenua baada ya uteuzi huu! Naona wajumbe wengi ni mawakala wa CCM!
 
Yes, team ya juu ya kigoda cha mwl nyerere bado na heshima, hata jaji agustino naye jembe pia, hope they stay undefiled

Kigoda cha mwalimu sawa lakini hawa ni wahafidhina ingebidi wachanganywe na waliberali ili kuleta uwiano. Namkubali Waryoba pia wajumbe wengine ila sasa huo mchanganyiko sijaona kijana wa miaka 18; sijui kama kuna Mkulima humo; walemavu wa ngozi udhani wana Rais wao manake kila sehemu ni huyo huyo; sijaona uwakilishi wa wafugaji wala wanywa gongo. Tume imesheheni wanasheria. Wanasheria wangekuwepo lakini wengi wangekuwa kwenye sekretariati ili kuyaweka mawazo ya wavuvi, wakwezi na walima bangi kwenye lugha ya kisheria.
 
Back
Top Bottom