Jua furaha yako iko wapi, itafute

Jua furaha yako iko wapi, itafute

Ishmael

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
15,039
Reaction score
6,018
Tofauti ya binadamu na viumbe wenzake wote, iko katika ufahamu. Binadamu anaweza kutumia ubongo wake vizuri zaidi na hivyo kujitofautisha na "wanyama" wenzake wasiojua wanakotoka na wanakoelekea.

Anao uwezo wa kujua anataka nini na afanyaje kukipata. Wenzake wote, pamoja na Sokwe mwenye Di Eni Ei zinazokaribia kufanana na zake, na hata wengine tukadhani wanachangia babu wa babu, hawana kingine wanachokitafuta zaidi ya uzazi. Wao, kuzaa kuna maana ya kufikia kiwango cha juu cha mafanikio katika kipindi cha maisha yao. Wakishazaa basi, hata wakifa, kwao kifo hicho hakitahesabika kuwa cha hasara.

Nini kusudi la binadamu kuzaliwa? Je, binadamu huyu anatafuta kitu gani katika kipindi cha maisha yake ambacho akikipata hicho basi anaridhika? Anataka nini ambacho akiisha kukipata basi, kwake hayo ndiyo mafanikio katika kilele chake?

Je, ni kuzaa kama ilivyo kwa ndugu zetu wanyama? Je, ni kuwa na mke mrembo kuliko wote (kama kweli yupo)? Ni kuwa bilionea nambari moja Bongo yote? Ama ni kuzawadiwa usomi kwa wingi wa shahada? Kwanza inasemekana kadiri binadamu anavyosoma ndivyo anavyokuwa mjinga, kwa sababu anazidi "kusoma mambo machache" mpaka unakuta anageuka mjinga anayejua kitu kimoja!

Kusudi ni nini? Ama ni furaha? kwamba binadamu anapigana vikumbo kutafuta furaha (utoshelevu) wa moyo wake? Kwamba awe Raisi afurahi. Awe na mke mzuri afurahi. Ajulikane. Afurahi. Je, ndivyo ilivyo?

Ukamilifu wa maisha ni kitu gani? Umezaliwa iliiweje? Ule, uzae, ufe? Wote tunajua kamwe hiyo haiwezi kuwa kweli.

 
Furaha! ni rahisi kutamka wala si kuipata.

wengi wetu huwa tuna mihemko ya muda mfupi nayo huwa tunaiita furaha.

Mkuu kuijua furaha yako ilipo ni safari yaweza kuwa ndefu ama fupi kutegemea na malezi.

Huwezi ukapata furaha kama haujitambui wewe ni nani,nini kusudi la aliyekuumba kukufanya uwe kama ulivyo na ujiulize na kupata jibu kwanini wewe ni tofauti na viumbe wengine wote? Yaani mimi au wewe ni wa kipekee hakuna aliyewai kuwa kama mimi auwewe wala atakayekuja kufanana na mimi au wewe hadi mwisho wa dunia.

Je umewai kujiuliza wewe ni nani?

Pengine ukiwa na jibu la uhakika la swali hilo ndo unaweza ukaijua furaha yako ilipo.
 
Najaribu kuifikiria dunia yenye watu wote wenye furaha siku zote za maisha yao.ninawaza huenda ndio ile ambayo Adam na hawa walifukuzwa.huku tulipo ni kama tunaishi ndani ya matokeo ya uovu ule.

Furaha ya mtu unakuja kwa muda na inaondoka bila hata mtu mwenyewe kugundua imesababishwa na nini.

Ukitaka kuamini hili kumbuka siku yoyote ambayo ulifurahi mazingira na vitu ulovyokuwa navyo siku hiyo then fanya kuirudia siku ile uone kama itakusisimua.

Binadam anatafuta amani ili imretee furaha bila kujua kuwa vitu vyote hiyo ni nje ya uwezo wake yeye.haijatokea dunia yenye maisha yenye furaha kama ambavyo wanadamu tunafikiri ni kuonjeshwa tu.
 
Furaha huja pale unapokuwa na amani na watu wote, uwe na uwezo wa kutumia maneno haya: Pole, samahani, asante, karibu na mengineyo yanayoonyesha hali ya kujishusha. Alafu kuwa mbunifu ili kuongeza kipato chako alaf tambua mahitaj ya wanaokuzunguka na wakihitaj msaada wapatie kadri ya uwezo wako. Mwisho mtangulize Mwenyezi - MUNGU kwa kila jambo.
 
be who your are, love your self and what ur doing , love others as u love ur self. jifunze kushukuru kwa kila jambo
 
kuna nchi sijui Finland, ndio watu wenye furaha kuliko wote duniani!
 
Maisha ni matamu na furaha inaweza kupatikana iwapo kila mtu atafanya yake.
Mijitu sasa kupenda kuingilia maisha ya watu wakishindwa na yao. Pesa unatafuta ila ukitumia unasakamwa.
Muacheni kila mtu afurahie maisha ili mradi havunji sheria.
 
daaahhh Furaha ya Kweli itatoka kwako Mwenyewe japokuwa kuna siku ya kucheka na siku ya kulia
 
Kuishi maisha yako ni furaha tosha.....Haijalishi unakula nini na unalala wapi.......Kufanya kile wanachokiogopa wenzako ndio unajenga ulimwengu wako....kuwa wewe na sio yule au wale....
 
Furaha huja pale unapokuwa na amani na watu wote, uwe na uwezo wa kutumia maneno haya: Pole, samahani, asante, karibu na mengineyo yanayoonyesha hali ya kujishusha. Alafu kuwa mbunifu ili kuongeza kipato chako alaf tambua mahitaj ya wanaokuzunguka na wakihitaj msaada wapatie kadri ya uwezo wako. Mwisho mtangulize Mwenyezi - MUNGU kwa kila jambo.
Kuna watu wamepoteza Furaha baada kuwatendea mema wengine...yaani wema wao uligeuka majuto....
 
Furaha ni kutimiza ndoto zako zote..ili kufanikisha malengo yako hapa duniani..chukua paper orodhesha ndoto zote ulizonazo tick moja baada ya nyingine ukimaliza kuachieve zote hence ur happy kuanzia hapo usikubali mtu mwingine akuletee stress.alafu kuwa mcha Mungu pia akuepushe na majaribu ndo yanaondoa furaha
 
Kuna watu wamepoteza Furaha baada kuwatendea mema wengine...yaani wema wao uligeuka majuto....

LIFE IS NOT JUST HAPPENING TO YOU ,, IT RESPONDING TO YOU...The way you face life,
determines how it shall respond to you!
Stop just existing and start living in order to experience life like you have never done before
 
LIFE IS NOT JUST HAPPENING TO YOU ,, IT RESPONDING TO YOU...The way you face life,
determines how it shall respond to you!
Stop just existing and start living in order to experience life like you have never done before
Easier said than done
 
Kuna watu wamepoteza Furaha baada kuwatendea mema wengine...yaani wema wao uligeuka majuto....

Kweli mkuu mimi pia ni muathirika wa hillo. Nimesamehe lakini nimehuta majuto ya firaoun.na athar zake bado ninaishi nazo.
 
Kweli mkuu mimi pia ni muathirika wa hillo. Nimesamehe lakini nimehuta majuto ya firaoun.na athar zake bado ninaishi nazo.
Nimeongea hii sio kwa kumtolea MTU mfano nami nimuathilika wa jambo hili unafanya jambo jema kwa mtu kwa lengo la kuShare nae furaha yako lkn yy anakuwa unaemsaidia anakuwa Tanzi kwako....so..kuwa au kutokuwa na furaha kwa MTU kunachangiwa na mengi mwingine umaskini unamfanya akose furaha mwingine utajiri unaweza kumfanya mtu aikose so MTU kuwa na Furaha nizaidi yakupata kitu
 
Back
Top Bottom