galimoshi
Member
- Aug 5, 2023
- 13
- 8
Na Mwandishi Wetu-Momba
JOTO kisiasa katika majimbo yaliyopo mkoani Songwe limeamza kupanda baada ya Mbunge wa Tunduma, David Silinde kudaiwa kuandaa vijana kumzuia mbunge wa Momba, Condester Sichalwe asihudhurie mkutano wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Momba.
Tukio la kuzuiliwa Condester lilitokea Jumamosi (Aprili 19, 2025) wakati wa mkutano wa Baraza la UVCCM uliofanyika katika Shule ya Sekondari Tunduma na kuhudhuriwa na viongozi wa CCM na UVCCM wa Wilaya ya Momba.
Silinde ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo alipopigiwa simu mara kadhaa ilikuwa inaita tu bila kupokelewa lakini alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) hakukataa wala kukubali kama alihusika kupanga vijana wa kumzuia mbunge Sichalwe kuingia kwenye kikao badala yake alimtaka mwandishi kuwasiliana na Mwenyekiti ama Katibu wa UVCCM Wilaya ya Momba.
"Mpigie mwenyekiti au katibu wa vijana wa Wilaya ya Momba nadhani ndio watu sahihi kukupa majibu ya maswali yako maana mengine ndio nasikia kwako," alisema Silinde baada ya kuandikiwa sms na mwandishi kwamba anadaiwa kuhusika kuandaa vijana kumzuia mbunge wa Momba asiingie kwenye kikao hicho.
Katibu wa UVCCM Wilaya Momba, Thomas Warioba, alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema ni kweli vijana wa 'green guard' walimzuia Sichalwe asiingie, hata hivyo hakueleza sababu za vijana hao kufanya kitendo hicho.
"Waliomzuia mbunge Sichalwe asiingie kwenye kikao cha UVCCM Wilaya walikuwa vijana wa green guard na sio kweli kwamba waliandaliwa na mbunge wa Tunduma Silinde wale ni vijana wa hamasa wa UVCCM," alisema.
Naye Mwenyekiti wa UVCCM ya Momba, Mandela Mtaki, alipoulizwa kuhusu tukio hilo alikiri kutokea lakini akasema hawezi kulizungumzia kwa undani kwasababu limeshafikishwa kwa Katibu wa CCM Wilaya ndiye anayeshughulika nalo.
"Suala hili mimi siwezi kulizungumzia lilivyotokea nakuomba muulize Katibu wa CCM wa Wilaya yeye ndiye ana mamlaka ya kuzungumzia suala hilo na sio sisi viongozi wa UVCCM," alisema.
Katibu wa CCM Wilaya ya Momba,Kataba Sukulu, alipoulizwa kwa njia ya simu alisema baada ya tukio kutokea alitoa maelekezo na kukemea kitendo alichofanyiwa mbunge Sichalwe.
"Tamko gani tena la chama unataka nitoe wewe sikiliza ile 'clip' hadi mwisho utasikia maelezo niliyoyatoa baada ya tukio hilo kutokea," alisema katibu huyo na kukata simu.
Mbunge wa Momba,Condester Sichalwe, alipoulizwa alisema ni kweli alizuiliwa kuingia kwenye mkutano wa UVCCM Wilaya ambao mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Tunduma, David Silinde licha ya kwamba na yeye alialikwa.
Alisema vituko vilianza kwa kuzuia gari lake kwa kupanga magari ili asiweze kupita baada kutoka kwenye kikao cha Mfuko wa Jimbo lakini baadaye alimua kushuka kwenye gari lake na kuanza kwenda ukumbini.
Sichalwe alisema baada ya kufika karibu na lango la kuingilia ukumbini vijana wa green guard walimzuia na alipohoji alielezwa kuwa wamepewa maelekezo na viongozi kwamba yeye (Sichalwe) asiingie kwenye mkutano huo.
Taarifa za ndani kutoka katika kikao hicho zinaeleza kuwa mbunge huyo baada ya kuzuiliwa Katibu wa CCM wa Wilaya alipewa taarifa na kuingilia kati ambapo alikemea kitendo kilichofanywa na vijana wa green guard na Sichalwe aliingia ukumbini na kuendelea na kikao.
Mbunge Sichalwe licha ya kupata msukosuko wa kuzuwiliwa, baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza kwenye mkutano huo alitekeleza ahadi yake ya kutoa Sh.milioni moja kwa ajili ya kusaidia UVCCM lakini katika hali ya kushangaza Mwenyekiti wa UVCCM alikataa kuipokea.
Katika Group la Whatsaap liitwalo MAENDELEO MOMBA tarehe 26 April 26, 2025 mmoja wa wana group hilo Kapwa Mwilang’ombe aliandika ujumbe unaomtuhumu Mhe. David Silinde Mbunge wa Tunduma kumpatia mtu mmoja pesa za kugombea ubunge Jimbo la Momba, na mtu huyo anaitwa Martin, hata hivyo baada ya tuhuma hiyo Mbunge Silinde alijibu ujumbe huo hivi “Sinaga tabia za kujibu watu mitandaoni, ila kwa hili umenikwaza!! Acha tabia za kutengeneza chuki kwa stori za kutunga. Sina mgombea yoyote niliyemtuma Momba na pili sina hela ya kumpa mtu aje kugombea Momba. Mwisho kabisa … Siku nikitaka kugombea Momba nitakuja mwenyewe na sio kumtuma mtu ….huwa sipigani vita mbili kwa wakati mmoja” mwisho wa kunukuu.
MWISHO