Joto kuongezeka Moshi je volcano inatukutia?

samakinchanga

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2014
Posts
2,024
Reaction score
1,237
Kwa sasa bora hata dar jamani joto la mji wa Moshi linaongezeka sana.labda huko chini ya mlima kuna ule ujiuji mzito jina magma umekasirika nini?wataalam wa miamba tujuzeni
 
Moshi pana jota sana kwani ni bondeni na maeneo ya KIA pengine ndio ndipo penye joto kali zaidi Tz
 
Ni ishara za nyakati.Kiama kimekaribia.Watu watubu dhambi
 
Kwa sasa bora hata dar jamani joto la mji wa Moshi linaongezeka sana.labda huko chini ya mlima kuna ule ujiuji mzito jina magma umekasirika nini?wataalam wa miamba tujuzeni
Volkano ya mlima Kilimanjaro ni ''volkano iliyokufa''. Joto linasababishwa na uzembe wetu binadamu. Watu wanakata miti na kuacha nchi kama jangwa! Mji wa Moshi hauna miti ya kutosha japo ardhi ina rutuba! Na ndicho kinachoikumba Dar! Wakoloni wali-plan miji vizuri sana wakaacha sehemu za wazi, bustani na miti. Mwafrika ''alipojitawala'' akaona mkoloni ni mjinga. Akaingilia kujenga kila sehemu yenye nafasi huku akikata miti hovyo! Tunacheza muziki tulioomba sisi wenyewe!
 
Kuna mwaka nilikuwa na safari ya Moshi nikajikoki na nguo nzito, nilichokipata dah!
 
Volkano ya mlima Kilimanjaro ni ''volkano iliyokufa''. Joto linasababishwa na uzembe wetu binadamu. Watu wanakata miti na kuacha nchi kama jangwa! Mji wa Moshi hauna miti ya kutosha japo ardhi ina rutuba! Na ndicho kinachoikumba Dar! Wakoloni wali-plan miji vizuri sana wakaacha sehemu za wazi, bustani na miti. Mwafrika ''alipojitawala'' akaona mkoloni ni mjinga. Akaingilia kujenga kila sehemu yenye nafasi huku akikata miti hovyo! Tunacheza muziki tulioomba sisi wenyewe!
Volcano ya kilimanjaro ni volcano iliyokufa?????????

Kunanhaja ya kumsue mwl wa geograpghy

Watunzi wa Vitabu vya geography pamoja na wizara ya elimu.....
 
Mwaka 2050(kama sijakosea) wanasayansi walisema barafu yote itakuwa imeisha na itachukua miaka 150 kwa barafu kuonekana juu ya kilele cha mlima.Nadhani wako right
 
Volcano ya kilimanjaro ni volcano iliyokufa?????????

Kunanhaja ya kumsue mwl wa geograpghy

Watunzi wa Vitabu vya geography pamoja na wizara ya elimu.....
Pale kuna volkano tatu. Mawenzi, Shira na Kibo. Shira na Mawenzi zimekufa ila Kibo imelala fofofo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom