INGAWAJE MABADILIKO YA KWELI NDANI YA NCHI HII KITOVU CHAKE A-TAUNI, TSUNAMI LA KISIASA LITAKALOLIFUNIKA KABISA CCM NA MAFISADI WAKE SASA MIKONDO YAKE KUKUTANIA IDODOMYA
Wanabodi bado nakumbuka; Wanaharakati tulipoanza wengine walitubeza, CHADEMA ilipoanza kuwakabili sana MAFISADI kwingineko chama chetu hiki kikapata kubatizwa jina 'Vyama vya Msimu',
na hivi sasa, kwa kuwa CHADEMA imebadilika na kuwa zaidi ya msumari wa moto kwa MAFISADI hao hao na kwa jinsi hiki chama cha Rostam Aziz kinavyoendelea kuzama fasta ajabu kwa Kimbunga Cha Lema wenzetu sasa wanatukaba kwa kuua wanachama wetu.
Hebu mwenzenu mwachieni Mh Nassari akahimize kitu Utaifa mbeeeele kama tai LAKINI katika kweli, heshima kwa utu wa Mtanzania katika mazingira ya HAKI na HAKI tu na wala si kwa kutegemea tabasamu katika uso wa rais wa nchi na viongozi maswahiba wake!!
Naam, japo ni kweli mabadiliko ya kuikomboa nchi hii yalianza rasmi na ule umwagaji damu kule A-Town lakini hivi sasa Tsunami ya kisiasa yaja kutoka kanda ya Ziwa (Bukoba, Mwanza, Mara na Shinyanga) ...
... na hivyo kuja kukutana na ule mkondo wa Kanda ya Juu Kusini (Njombe, Mbeya, Iringa, Songea) na siku zitakapokutania pale katika Jiji la Idodomya basi hapo hapo ndipo CCM pamoja na MAFISADI wooote watakapoDIDIMIA kimoja na kusahaulika na historia hata kabla ya 2015.
Habari ndio hiyo wanabodi kwa wale waliodhania kwamba kimbunga CHADEMA ni kule kaskazini tu.