Joshua nassari anatisha kwa mistari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Joshua nassari anatisha kwa mistari

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by ExpertBroker, Apr 2, 2012.

 1. E

  ExpertBroker JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Jun 1, 2009
  Messages: 454
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  [h=6]“Ninawashukuru sana watu wa Arumeru Mashariki ambao hawakujali umri wangu, uwezo wangu kifedha, historia ya familia yangu katika siasa, na mapungufu niliyokuwa nayo lakini wakakubali kunichagua!
  Najua walikuja wengi na fedha nyingi,
  Najua walikuja wengi na majina makubwa,
  Najua walikuja wengi na kila aina ya mbwembwe,
  Najua walikuja wengi na bendi nyingi na wakahonga sana,
  Najua walikuja wengi wakanitukana na kunisema sana! Lakini hatimaye sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, na lile alilolipanga mwenyezi Mungu limekwenda kutimilika!

  Walipoambiwa mimi ni mdogo kiumri, walisema siendi bungeni kupeleka mvi au miaka, na wakasema wanahitaji dogo janga na si kubwa jinga,
  Walipoambiwa mimi sijaoa, wakasema mimi siendi bungeni kusuluhisha ndoa,
  Walipoambiwa mimi ni masikini, walisema wanahitaji masikini mwenzao,
  Walipoambiwa sina kitambi, walisema bungeni siendi kucheza mieleka…” MBUNGE MTEULE, ARUMERU MASHARIKI, JOSHUA NASSARI, BAADA YA USHINDI!
  [/h]
   
 2. d

  david2010 JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  People Power!!!!!####$$$$$$$ Kijana huyo hyoo!!!!!!!!! bungeni hapo ametoa mistari michache na si hilo lazima ahadi itekelezeke. Ahsanteni Watu wote na hasa Makamanda wote waliojitolea kwa hali na mali n muda kuhakikisha watu wanashinda. Ahsante Mungu
   
 3. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hotuba hii nimeipenda
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Bungeni kutawaka moto!
  Nadhani Anna Makinda anazidi kuchanganyikiwa huko aliko, maana anaona wazi balaa liko mlangoni laja!
   
 5. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  This is another chapter in our country! The Youngest MB in our parliamentary House!! Hope 2015 will have more young MBs via CDM.
  Its M4C.
   
 6. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,069
  Likes Received: 419
  Trophy Points: 180
  edit hapo juu. kasema dogo janja sio janga
   
 7. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160

  The young man is good kuliko wengi wanavyomuelewa jukwaani....he is real vocal tangu alipokuwa chuo, he has content na ability kubwa ya kusoma in between lines..............na fani aliyosomea iko direct linked na kazi aliyoomba kuifanya......alikolelewa kisiasa ni furnace per se

  So he is just too good to be........he deserves and he is capable
   
 8. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Movement for CHANGE,
  Movement for CHADEMA.
   
 9. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Nasali kwanza jamani kutoa shukrani kwa Mungu..
   
 10. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kichwa kingine kutka Arusha......
  Kama kuna mtu amepata nafasi ya kusoma maandiko ya Mh. Lema (huwa anaandika mara chache sana), mtakubaliana nami kwamba Lema ni hatari sana.

  Nimeona huyu kijana anaweza kuwa balaa katika kuwasilisha ujumbe wake kwa maandishi.........Safi sana.
   
 11. M

  Mr Emmy JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,201
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Shahada/Degree yake amesomea nini Mkuu?
   
Loading...