JOSHUA NASSARI nakufananisha na Joshua Myahudi aliyetumwa na Mussa kwenda kuchunguza nchi ya maziwa na asali. Mungu amekuinua wewe kwenda kuwasemea na kuwawakilisha wana arumeru wote pasipo kujali itikadi zao.
Kumbuka siku ulipotangazwa kuwa mshindi mvua kubwa ilinyesha kama ishara ya baraka na kukubalika kwako mbele za Mungu. Watu waliomba Mungu awape kiongozi Arumeru....wamama na bibi zetu wanaoteseka hasa katika suala la ukosefu wa huduma nzuri za afya, maji, ardhi waliomba sana, Mungu amewajibu.
Kumbuka Mungu aliwaambia wana wa Israeli...utakapofika uko..ukafanikiwa na kondoo, mbuzi, ngamia, ngombe zako wakaongezeka...usimsahau Mungu aliyekuweka hapo. ULIANZA NA MUNGU...USIMWACHE KABISA. MAJITU(CCM) yasikuogopeshe kwa lolote..saaa ya ukombozi ndio hii. ushindi huu umeleta mwangwi mkubwa wa furaha kwa Watanzania wengi wapenda mabadiliko na maendeleo...YOUNG MAN NEVER EVER GIVE UP....