Josephine Mushumbusi: Mwanamke aliyeota kuwa na asiye na hadhi ya kuwa First Lady

Status
Not open for further replies.
Hii Picha ina mwisho wake na mwisho wake wapo watakaofurahi na wapo watakaochukia,pia wapo watakaocheka na wapo wengine watalia na kusaga meno so tuvumilie tu,Zimebaki siku chache sana kuikuta october
 
Slaa: (huku amekodoa macho) Siamini kabisa mke wangu. Yaani,... basi tu..
Jose: Kwani tatizo nini baby?
Slaa: Eti nimelazimishwa nimpishe Lowasa kugombea urai...(kwi kwi kwi)
Jose: Nini?... hebu rudia tena. Umpishe nani?
Slaa: Eti... eti Lowasa.
Jose: Kwa hiyo umewakubalia?
Slaa: (nodding)
Jose: Kwa hiyo... inamaana ufirst lady nitausikia tu kwenye media? Haiwezekani!
Slaa: Lakini mke...
Jose: (interrupts) nyamaza, mke wako nani? Tena kuanzia leo... (itaendelea)

Wacha uongo, hapo ndio imeishia mwisho haiendelei
 
Wakuu,

Ninajua kuna wengine nitawakwaza kutokana na andishi hili, hasa makamanda wenzangu wa chadema kuhusu maoni yangu dhidi ya Josephine Mushumbusi.

Kama mnavyojua ni kwamba CC ya chadema ilikuwa na vikao vizito hivi karibuni kwa ajili ya uchaguzi mkuu. Moja ya agenda ilikuwa kumpata mgombea urais atakayeweza kupeperusha bendera ya chadema na ukawa.

Vikao vilikaa vikafikia maamuzi ya Eddo kupewa jukumu nzito ya kuipeperusha bendera, maamuzi yaliyoafikiwa na viongozi wote wa ukawa akiwemo Dr. Slaa.

Mara ya mwisho Dr. Slaa kushiriki vikao vya chama ilikuwa Jumapili, kikao ambacho kilichukua muda hadi saa nane usiku.

Ajabu ni kwamba siku ya Jumatatu Dr hakuweza kutokea ofisini, aliweza tu kuwasiliana na viongozi wenzie kwa simu kwa ajili ya kujipanga kwenda kwenye mkutano wa kumpokea Eddo. Siku ya J4 Dr hakuweza kushiriki mkutano wa Eddo, na hata alipotafutwa kwa simu hakuweza kupatikana hewani....

Zoezi likapita la kumkaribisha Eddo, ikabaki kumtafuta Dr kujua nini kilimpata, baadhi ya viongozi waliamua kwenda kwake, walipofika getini walizuiwa kuingia, taarifa za watchman zinasema mama (Josephine Mushumbusi) amefunga geti na ameondoka na funguo....

Hivi sasa tunavyoongea Dr. Slaa yupo kwenye unlawful detention kisa Mchumba wake Josephine Mushumbusi amechukizwa kuukosa u First Lady. Huyu mwanamke asiyeweza kujiheshimu, asiye na ustaarabu ndiye anayeleta makwazo kwa Mzee wetu pamoja na sisi wapambanaji.

Simu zote za Dr Slaa zipo kwa Josephine, taarifa zinasema mwanamke amechanganyikiwa kiasi cha kumshinikiza Dr ajiuzulu na kufanya propaganda kwenye media....

Kitendo cha kumweka kizuizini mtumishi wa chama chetu kwa tamaa ya madaraka siyo haki, nadhani sasa ni muda muafaka haki ikatafutwa iwe kiparoko, kishekhe, au kibabe

Umbeya ni sumu!
 
Slaa: (huku amekodoa macho) Siamini kabisa mke wangu. Yaani,... basi tu..
Jose: Kwani tatizo nini baby?
Slaa: Eti nimelazimishwa nimpishe Lowasa kugombea urai...(kwi kwi kwi)
Jose: Nini?... hebu rudia tena. Umpishe nani?
Slaa: Eti... eti Lowasa.
Jose: Kwa hiyo umewakubalia?
Slaa: (nodding)
Jose: Kwa hiyo... inamaana ufirst lady nitausikia tu kwenye media? Haiwezekani!
Slaa: Lakini mke...
Jose: (interrupts) nyamaza, mke wako nani? Tena kuanzia leo... (itaendelea)

hahahahahaha
 
By Florence MajaniDar es Salaam. Siku moja baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuzungumza na gazeti hili na kusema yupo salama, mke wake, Josephine Mushumbusi amekanusha tuhuma zilizozagaa kuwa ndiye aliyemshauri kiongozi huyo wa Chadema kujiuzulu na kumzuia kushiriki vikao muhimu vya chama.

Tetesi hizo zilivuma kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari baada ya Dk Slaa kutoonekana katika vikao muhimu vya Chadema na Ukawa, kuwa Mushumbusi hakupendezwa na kitendo cha Lowassa kupitishwa kuwania urais chini ya mwavuli wa Ukawa na badala yake alitaka Dk Slaa ndiye awe mpeperusha bendera.

Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo Mushumbusi amezikanusha, aliamua alimfungia ndani Dk Slaa kama moja ya mbinu za kumzuia asishiriki shughuli za kichama, tuhuma ambazo amezikanusha. "Bosi wako akija kukuomba ushauri utamsaidia, lakini akija akakuambia ameshafanya maamuzi unaweza kupingana naye?" alihoji Mushumbusi akianza kutoa maelezo yake na kuendelea: "Wakati wa vikao nilikuwa namwona (Dk Slaa) anachelewa kurudi kila siku, siku moja akaja akaniambia uamuzi aliouchukua na mimi sikuwa na la kusema, nikachukua shuka nikajifunika."

Katika mahojiano yake ya kwanza na Mwananchi baada ya kuzagaa kwa tetesi hizo, Mushumbusi pia alikana kumfungia Dk Slaa ndani ya nyumba, akisema wakati maneno hayo yalipokuwa yanazagaa, alikuwa nje ya nchi na wala hakujua kinachoendelea. "Mwenyewe najiuliza nini kinaendelea, siwezi kufanya kitu kama hicho. Nyumba yangu ina milango miwili, nawezaje kumfungia mtu, tena mwanamume, hata watoto siwezi kuwafungia. Kuna mambo mengine mwanamke huwezi kuyafanya kwa mwanamume. Mwanamume ni mwanamume tu," alisema.

Alisema viongozi wa Chadema, ndugu, jamaa na marafiki walikuwa wanafika nyumbani kwake na walikutana na Dk Slaa na kuzungumza naye... "Kama ningekuwa nimemfungia wangezungumza naye vipi?"

Mushumbusi alisema mwanamke anaweza kufanya chochote lakini kuna baadhi ya mambo ambayo mwanamume akiamua ni vigumu kumzuia. Akifafanua tuhuma za kumshinikiza Dk Slaa kujiuzulu Chadema, Mushumbusi alisema kiongozi huyo wa Chadema ana uamuzi wake na yeye ni msaidizi tu ambaye hana uamuzi wa mwisho kwenye familia. Hata hivyo, alisema endapo angeamua kumshawishi, uwezo wa kufanya hivyo anao lakini yeye ni mwanamke mwadilifu anayependa mafanikio ya mumewe."Kwani unanionaje? Mimi ni ‘strong' (nina nguvu), ningetaka ningefanya hivyo, nisingeshindwa," alisema.

Pamoja na hayo, Mushumbusi alilalamika kuwa tuhuma hizo dhidi yake zimesababisha asisikilizwe kama ilivyokuwa awali. Bila kufafanua kwa undani, alisema kuna kundi linalounda propaganda hizo ili abadili mtazamo kuhusu mumewe lakini jambo hilo haliwezi kutokea. "Nilisema nitampenda kama alivyo, sitajali chochote wala akiwa katika hali gani au chama gani. Kazi yangu ni kumtia moyo ili kile atakachofanya kifanikiwe," alisema.

Auza mkaa

Mbali na kukanusha vikali tuhuma hizo, Mushumbusi alisema alikwishajitoa kwenye masuala ya siasa kwa miaka miwili sasa na badala yake ameamua kufanya biashara ya kuuza mkaa. "Nimenyamaza kimya, nimekaa kando ninaendelea na biashara yangu ya kuuza mkaa, nipo mbali na siasa na sitaki kujua kinachoendelea, kwanza hata mchakato wenyewe siujui," alisema. Aliwashauri wanawake kuacha kushabikia masuala yanayotokea ndani ya ndoa yake na kuwataka wavae viatu anavyovivaa na wajue kuwa anapitia wakati mgumu.

Chanzo: Mwananchi Gazeti la Leo

My Take:

Soma kwa makini hasa sehemu nilizobold, then utoa maoni yako.
 
Wanajamvi naombeni msaada wa kupewa taarifa "HIVI NDOA YA DR SLAA NA HUYU MAMA ILIKUWA LINI VILE?"
 
Teh TehView attachment 274129 uploadfromtaptalk1438937843872.jpg
 
Hongera sana josephine kwa kuwa mkweli naomba tu umtie moyo dr slaa arudi tunampenda sana sana huu mwaka ni wamabadiliko lazima slaa awepo kwenye mabadiliko haya.
 
Nasikitika mke wa katibu mkuu wa chama amekuwa miongoni mwa watu wanao haribu mazingira na kujaza hewa ya ukaa ambayo hivi sasa dunia nzima inapiga vita uharibifu wa mazingira na hewa ya ukaa. Kama ni kweli anafanya hivyo, nashauri Sirikali imchukulie hatua zinazo stahili dhidi ya uharibifu wa mazingira.
 
Ni kweli Mwanaume akiamua ameamua..hata Regina Lowassa alishindwa kumshawishi mumewake kubaki CCM, ingawa ulikuwa ushauri wa busara kutoka kwa mkewe.
Josephine pia nimependa busara na hekima uliyojaliwa....endelea kumtia moyo Dr kwenye maamuzi sahihi aliyofanya...hakika mmechagua kukaa upande sahihi wa historia
 
1438942628205.jpg

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuzungumza na gazeti hili na kusema yupo salama, mke wake, Josephine Mushumbusi amekanusha tuhuma zilizozagaa kuwa ndiye aliyemshauri kiongozi huyo wa Chadema kujiuzulu na kumzuia kushiriki vikao muhimu vya chama.

Tetesi hizo zilivuma kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari baada ya Dk Slaa kutoonekana katika vikao muhimu vya Chadema na Ukawa, kuwa Mushumbusi hakupendezwa na kitendo cha Lowassa kupitishwa kuwania urais chini ya mwavuli wa Ukawa na badala yake alitaka Dk Slaa ndiye awe mpeperusha bendera.

Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo Mushumbusi amezikanusha, aliamua alimfungia ndani Dk Slaa kama moja ya mbinu za kumzuia asishiriki shughuli za kichama, tuhuma ambazo amezikanusha.

“Bosi wako akija kukuomba ushauri utamsaidia, lakini akija akakuambia ameshafanya maamuzi unaweza kupingana naye?” alihoji Mushumbusi akianza kutoa maelezo yake na kuendelea:

“Wakati wa vikao nilikuwa namwona (Dk Slaa) anachelewa kurudi kila siku, siku moja akaja akaniambia uamuzi aliouchukua na mimi sikuwa na la kusema, nikachukua shuka nikajifunika.”

Katika mahojiano yake ya kwanza na Mwananchi baada ya kuzagaa kwa tetesi hizo, Mushumbusi pia alikana kumfungia Dk Slaa ndani ya nyumba, akisema wakati maneno hayo yalipokuwa yanazagaa, alikuwa nje ya nchi na wala hakujua kinachoendelea.

“Mwenyewe najiuliza nini kinaendelea, siwezi kufanya kitu kama hicho. Nyumba yangu ina milango miwili, nawezaje kumfungia mtu, tena mwanamume, hata watoto siwezi kuwafungia. Kuna mambo mengine mwanamke huwezi kuyafanya kwa mwanamume. Mwanamume ni mwanamume tu,” alisema.

Alisema viongozi wa Chadema, ndugu, jamaa na marafiki walikuwa wanafika nyumbani kwake na walikutana na Dk Slaa na kuzungumza naye... “Kama ningekuwa nimemfungia wangezungumza naye vipi?”

Mushumbusi alisema mwanamke anaweza kufanya chochote lakini kuna baadhi ya mambo ambayo mwanamume akiamua ni vigumu kumzuia.

Akifafanua tuhuma za kumshinikiza Dk Slaa kujiuzulu Chadema, Mushumbusi alisema kiongozi huyo wa Chadema ana uamuzi wake na yeye ni msaidizi tu ambaye hana uamuzi wa mwisho kwenye familia.

Hata hivyo, alisema endapo angeamua kumshawishi, uwezo wa kufanya hivyo anao lakini yeye ni mwanamke mwadilifu anayependa mafanikio ya mumewe.

“Kwani unanionaje? Mimi ni ‘strong’ (nina nguvu), ningetaka ningefanya hivyo, nisingeshindwa,” alisema.

Pamoja na hayo, Mushumbusi alilalamika kuwa tuhuma hizo dhidi yake zimesababisha asisikilizwe kama ilivyokuwa awali.

Bila kufafanua kwa undani, alisema kuna kundi linalounda propaganda hizo ili abadili mtazamo kuhusu mumewe lakini jambo hilo haliwezi kutokea.

“Nilisema nitampenda kama alivyo, sitajali chochote wala akiwa katika hali gani au chama gani. Kazi yangu ni kumtia moyo ili kile atakachofanya kifanikiwe,” alisema.

Auza mkaa

Mbali na kukanusha vikali tuhuma hizo, Mushumbusi alisema alikwishajitoa kwenye masuala ya siasa kwa miaka miwili sasa na badala yake ameamua kufanya biashara ya kuuza mkaa.

“Nimenyamaza kimya, nimekaa kando ninaendelea na biashara yangu ya kuuza mkaa, nipo mbali na siasa na sitaki kujua kinachoendelea, kwanza hata mchakato wenyewe siujui,” alisema.

Aliwashauri wanawake kuacha kushabikia masuala yanayotokea ndani ya ndoa yake na kuwataka wavae viatu anavyovivaa na wajue kuwa anapitia wakati mgumu.

Chanzo;mwananchi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom