Joseph Senga umempelekea salamu Mwangosi?

Joseph Senga umempelekea salamu Mwangosi?

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
10,737
Reaction score
14,894
Tutakukumbuka kwa mengi Sana JOSEPH SENGA hasa kwa umahili wako mkubwa wa kupiga picha katika mazingira magumu ikiwemo kupishana na silaha hatari hasa mabomu. umetuachia simanzi kubwa sana SENGA pengo uliloliacha litabaki kuwa kubwa na pengine inahitajika jitihada sana kuliziba.
IMG_1244.jpg

umahili wako mkubwa uliouonyesha hasa baada ya kuutambulisha ulimwengu juu ya unyama aliofanyiwa muandishi DAUDI MWANGOSI, ambaye aliuawa kinyama kwa kulipuliwa na bomu. bila wewe SENGA leo hii tusingejua na waliofanya hicho kitendo wasingejutia kukifanya kitendo kama walichomfanyia MWANGOSI. kwa kifupi Wakati Mwangosi akiwa anashambuliwa, Joseph Senga, naye alikuwa katika wakati mgumu baada ya askari kumdhibiti na kuanza kumpekua mifukoni, huku mwenyewe akijitahidi kujinasua mikononi mwao.
img.php
l
SENGA mpe salamu MWANGOSI mwambie japo haki aikutendeka katika kesi yake lakini tunaamini damu yake haikumwagika bure, naifananisha kesi ya MWANGOSI na kesi iliyomtia hatiani Aliyekuwa Kaimu Kamishina wa polisi mkoa wa Dar es Salaam, Abdalah Zombe ambaye kikosi chake kilitumiwa kuwaua wafanyabiashara wa madini, sheria ilimgusa hadi yeye ZOMBE ambaye pengine tukio hilo lilipokuwa linatendeka alikuwa ofisini lakini yeye kama mkuu wa kikosi aliwajibishwa japo mwanzo alishinda kesi lakini baadae wapenda haki wasiotetereshwa na tamaa ya mali walitoa hukumu inayostahili.
zombe.JPG

lakini imekuwa tofauti kwa mauaji ya MWANGOSI askari zaidi ya watano wanaonekana walikuwa wanamshambulia ila aliepatikana na hatia ni mmoja hii ata mtoto mdogo hawezi kuielewa, yule askari aleyepatikana na hatia si alikuwa anatekeleza majukumu aliyoagizwa hadi kufikia kumuua MWANGOSI. sasa inakuaje ahukumiwe peke yake pasipo kutolewa hukumu na yule aliye muagiza kutenda hilo kosa..? kazi za kijeshi zinajurikana kuwa ni za kupokea amri hivyo msumeno wa sheria ulitakiwa uwaguse wote ata yule aliyetoa amri. ila kwakuwa sheria kwa wengine sio msumeno umemkata asiehusika wanaohusika wamepandishwa vyeo hii inawezekana TANZANIA tu.
523247_200245940106924_552813434_n.jpg

SENGA mwambie MWANGOSI tunamkumbuka sana na tunatambua mchango wake mkubwa aliokuwa anautoa kwenye tasinia nzima ya habari. mwambie jinsi tulivyomlilia lakini kwakuwa sheria imepinda machozi yetu yameenda na maji kama machozi ya samaki yanavyopelekwa na maji baharini, mwambie watanzania siku hizi atuna tena mahala pa kukimbilia, unapigwa aliyekupiga akakuumiza anawahi kukushitaki, unakamatwa tena kwa kipigo kizito kisha unashitakiwa tena kwa kubambikiwa kesi,

TULIWAPENDA SANA SENGA NA MWANGOSI ILA MUNGU ALIPENDA MJE DUNIANI KUFICHUA MLIYOYAFICHUA, MUNGU ALIWATUMA MJE KUTUANGAZA KUTUONYESHA MABAYA WANAYOFANYA WANAUSALAMA TULIOWAAMINI NA KUWAPA MAISHA YETU WATULINDIE, TUNAAMINI MLIIFANYA VYEMA KAZI YENU NA TUNAAMINI MMEPOKELEWA VYEMA UKO MLIPO TUTAZIDI KUWAOMBEA NA TUNAOMBA NA SISI MTUWEKEE NAFASI UKO MLIPO.
 
Huwa nakaa nawaza na kuwazua sipati majibu,naamini kwa dhati kuwa MUNGU yupo.lkn napata taabu kukubali kuwa baadhi ya watawala na viongozi pamoja na Hawa wanausalama kuwa Wanaamini uwepo wa MUNGU,he kweli kutakua na hukumu siku ya mwisho?kama kweli sheria duniani haki mbinguni basis mwangosi na sisi wengineo wengi tusubiri kupata haki zetu siku ya mwisho mbinguni
 
Back
Top Bottom