Joseph Selasini, viongozi wa CHADEMA hawako hivyo... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Joseph Selasini, viongozi wa CHADEMA hawako hivyo...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Oct 20, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kwanza nikupongeze kwa kuufukua huo uozo huko Kondoa;;

  KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imependekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Isdori Mwalongo ambaye kwa sasa amesimamishwa kazi arejeshwe kazini mara moja kutokana na kamati kubaini kuwa sababu za mkurugenzi huyo kusimamishwa kazi ni za kupikwa.

  Mwenyekiti wa kamati ya LAAC iliyofika Kondoa, Joseph Selasini alisema kamati yake pamoja na Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) wameona ya kuwa mkurugenzi huyo ameonewa kutokana na ukweli kwamba kabla ya kusimamishwa kwake, alibaini wizi waSh72 milioni na alipochukua hatua dhidi ya mwizi husika naye akajikuta akisimamishwa kazi.

  Kabla kamati ilibaini kuwa mkurugenzi aliyesimamishwa alibaini wizi uliokuwa ukifanywa na aliyekuwa mhasibu wa wilaya hiyo (DT), ambaye kwa kushirikiana na mkandarasi aliyepewa kandarasi ya ujenzi wa madarasa wilayani hapo walifanya njama za kuiba fedha kwa njia ya kufanya malipo mara mbili ambapo badala ya malipo ya Sh36 milioni zililipwa Sh72milioni ambazo ni mara mbili ya fedha halali kwa mujibu wa mkataba.

  Baada ya Mwalongo kubaini wizi huo, alimfikisha mweka hazina wa halmashauri (DT) husika mbele ya Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo na baraza liliamua DT asimamishwe kazi na mkandarasi arejeshe fedha alizoiba, mkandarasi alirejesha Sh21 milioni tu.

  Hata hivyo ilielezwa kuwa mara baada ya DT kusimamishwa kazi aliapa kumshughulikia mkurugenzi wake na akajitapa kuwa anafahamiana na wakubwa ndani ya ofisi ya waziri mkuu ambao ilidaiwa anawatumia kumhujumu mkurugenzi aliyesimamishwa kazi.

  “Hatutaki kumtaja mtu, lakini tunafahamu ya kuwa kuna kiongozi mkubwa Tamisemi ambaye anatumiwa vibaya, inashangaza mwizi kupandishwa cheo na kuendelea kutesa mitaani huku huyu aliyegundua kuwapo wizi akiteseka yeye na familia yake, kiongozi huyo wa Tamisemi asitumike vibaya, leo hatumtaji lakini kama hakutokuwapo na utekelezwaji wa maagizo haya kamati itachukua hatua ikiwa ni pamoja na kuliweka bayana jina la kiongozi huyo anayetumika vibaya,”alisema Selasini.


  Tatizo langu bwana Selasini, ni kuwa CHADEMA haifanyi kazi kwa kuogopa watu. Kwa taarifa yako huyo anayemhujumu Bw Mwalongo baada ya kujua amefahamika, atatumia mbinu mbaya zaidi kuuficha uozo wake. Wewe ulutakiwa umtaje, tena kwa jina lake na la ukoo, tumchambue hapa, tumzomee aache huo ujinga, na Bw Mwalingo arudi kazini.

  Usidhani wewe mwenyewe unaweza kumshinikiza huyo mhalifu, bali sauti za watu mbalimbali na vyombo vya habari zingesaidia, na kama ungamtaja jina ingetia hamasa zaidi...
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa hata mimi ningetarajia huyo kiongozi aliyepo tamisemi atajwe ili afahamike kwa watanzania na hususan wanakondoa wamfahamu mtu anayemlinda mwizi wao.

  Hili la kuficha jina la huyo kigogo wa tamisemi si jambo zuri hata kidogo kwani linarudisha nyuma jitihada za kupambana na ufisadi.
   
 3. l

  luhwege Member

  #3
  Oct 20, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mimi binafsi ningependa hao wote waliohusika na ubadhilifu wa pesa na wamepatikana hadi kufikia maamuzi ya kuzirudisha wafunguliwe mashtaka siyo kuachwa wakiwanyanyasa wenye haki, mpaka hapo ushahidi wa kuwatia hatiani tayari upo sasa iweje warudishe na wasifunguliwe mashtaka au wezi wa kuku tu ndiyo wenye haki ya kuingia magerezani tu? Imefika mahali wenye pesa hawashikiki jamani mnatupeleka wapi.
   
 4. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Selasini vipi bana mbona unatuangusha? Kazi ya kutetea haki katika mfumo uliioza kama huu wa magamba ni ngumu sana, wewe weka mambo hadharani ili kila mtu amfahamu na nguvu ya umma ndio itoe hukumu. Bila nguvu ya umma kwa hawa magamba ukombozi wa hii nchi utabakia historia
   
 5. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Aisee Selasini na wewe umeanza ya Mwakyembe eeeeh!!! ........... hiyo nayo ni aina ya wizi
   
 6. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi mnamlaumu kwa lipi?
   
 7. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Failed
   
 8. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Failed
   
 9. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Failed
   
 10. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Passed
   
 11. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kichaa kakutana na Mwendawazimu
   
 12. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  lakini ilitakiwa atajwe huyo kiongozi ili awajibishwe
   
 13. M

  MIRIJA IKATWE Senior Member

  #13
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh. Huna Kosa ila lazima atajwe mpe tu muda wa kujifikiria ,tunataka tumjue
   
 14. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Hivi huwa unafuatilia mijadala au unakurupuka tu. Selasini anaumia kwa kuficha
  jina kigogo wa TAMISEMI anaye mlinda mwizi wa maduhuli ya serikali yaliyopelekwa
  ktk Halmashauri ya Kondoa.

  Kwa ufupi huo nao ni UFISADI na mambo ya kulindana ni sera ya CCM na ndiyo
  imeifikisha nchi hapa tulipo.
   
 15. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2011
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Chadema huwa hawana utaratibu wa kumuonea haya mwizi. Selasini unachafua hali ya hewa, tafadhali sahihisha makosa yako haraka.

  Unataka kutuambia kuwa staili ya JK ya kuwasamehe wezi kwa kuwaomba warudishe pesa walizoiba ilifanikiwa? Umenichefua!!!
   
 16. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mimi nafikiri huyo Mhalifu atajulikana tu; tuvute subira ili tupate kujua jinsi watu wanavyotumia mamlaka yao vibaya.
   
Loading...