Joseph Selasin, Mbunge wa Rombo, anaandika

Joseph Selasin, Mbunge wa Rombo, anaandika

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,450
Reaction score
32,290
Kwa Mhe Rais wetu, Rais Mtukufu na wa wanyonge wote Tanzania.
Salaam.
Jana nilikuangalia na kukusikiliza kwa makini ulipokuwa wanatoa neno baada ya kuwaapisha Majaji uliowateua wiki hii. Niliona pia ulipomsimamisha CAG na kumuuliza kama kuna pesa trillioni 1.5 alizogundua kwamba zimeibiwa na akakujibu hakuna.
Pia nilikusikia ukisema umeisoma taarifa ya CAG mwanzo hadi mwisho.
Haraka nilikimbilia kitabu changu ambacho nami nimekisoma mwanzo mpaka mwisho.
Nilipofungua ukurasa wa 34 niligundua haya:-

1. CAG Anasema, kwa mwaka wa fedha 2016/17 Serikali ilipanga kukusanya mapato yenye dhamani ya Shilingi Trillioni 29.5

2. Mapato halisi yaliyokusanywa ni Shilingi Trillioni 25.3

3. Serikali ilitumia shilingi Trillion 23.8

4. Trillioni 25.3 ukitoa Trillion 23.8 ni Trillion 1.5 ambazo ndizo anazotaka apewe maelezo.

Mtukufu Rais CAG hajasema pesa zimeibiwa. Wala ktk hatua hii hawezi kusema hivyo. Anachosema fedha hizo, matumizi yake hayaonekani na hazipo popote. Inawezekana kweli zimeibiwa, zimetumika kwa uzembe bila kufuata sheria au zipo mahali fulani.

Kwa taratibu za kibunge Maafisa Masuuli(accounting officers) wanatakiwa wampelekee ushahidi wa matumizi yake au ziliko ktk Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali yaani PAC mbele ya CAG ili hoja hii ifungwe. Kama wakishindwa kuifunga PAC na CAG sasa wanaweza kuomba msaada wa Polisi na au Takukuru kutafuta wezi au wabadhirifu.

Mhe Rais bila shaka umesoma pia ktk ripoti kwamba Serikali ktk ujumla wake imepata HATI CHAFU.
Wakati ukipokea taarifa hii Ikulu uliagiza Mkurugenzi wa Mji wa Kigoma Ujiji na wa Pangani watumbuliwe kutokana na maeneo yao kupata hati chafu.

Mhe unasubiri nini kumtumbua Katibu Mkuu hazina kwa kuisababishia Serikali yako kupata Hati chafu? Mbona kila mara unaapa kuwa mtu wa haki na jana uliwaagiza Majaji wakatende haki kwa Watanzania hasa wanyonge?

Mheshimiwa Serikali yako imepata doa kubwa. Vyombo vya dola haviwezi kulizuia kwa kuwatisha wanaoandika. Hizi ni fedha za maskini wote unaowatetea wauza maandazi, mitumba, mchicha na wengine wakubwa.

Ninakushauri baadala ya kuwatisha wanaohoji, waagize watendaji wa Serikali yako, wapeleke maelezo ya kutosha yenye ushahidi kwa CAG. Vinginevyo hatutaacha kukuuliza kila mara ZIKO WAPI PESA ZETU SHILINGI TRILLION 1.5

Jana Naibu waziri wa fedha alisema uongo Bungeni akidai sehemu ya fedha hizo Billioni 200 Serikali ya Muungano iliisaidia Serikali ya Zanzibar kukusanya mapato yake huku Bara.

Wote tunajiuliza vyanzo vya mapato ya ZNZ huku bara ni vipi? Hebu atutajie tuvijue na je! utaratibu huo ulikuwa wa 2016/17 peke yake tangu uhuru au ulikuwepo Taifa lisijue?
Mheshimiwa naona nakuchosha lakini nataka kusema neno la mwisho.
Inawezekana unadanganywa sana na waliokuzunguka na kwamba hawakuambii mambo mengi kwa faida yao. Wanapenda tu kukuambia yale wanayogundua unapenda kuyasikia na wanaogipa kukukosoa kutokana na ukali wako. Panua wigo wasikilize hata wale ambao hupendi kuwasikia hutakosa jambo lenye faida. Asante.
Joseph RS
 
Nilikuwa sijajua hiyo trillion 1.5 inayosemwa, sasa Mh. Selasini amenielewesha vizuri na nimeelewa! Kweli watoe majibu bwana kama wamekosea magazijuto warudie tena! Mwaka huu jiwe lazima afe kwa pressure, siku 2 tu Zitto kambana mpaka Jana anatoka hadharani akiwa afya mgogoro!!
 
Wapinzani/vibaraka naona mmejifunza jinsi ya kuishauri na kuihoji Serikali iliyopo madarakani...ni jambo linalostahili pongezi. Bwana Selasini unaanza kupevuka kisiasa.
 
Jumlisha toa za fedha acha kabisa
Hawa wa accounting bhana 1+1 abadani haiwezi kuwa 2
Maneno rahisi kabisa haya kama like swali maarufu sana 'onesha vyeti'
 
Kwa wenzetu statement kama hii ni 'madini' adimu lakini kwa TZ ni 'rubish' na sio ajabu mwandishi akahojiwa kwa uchochezi!
 
Nilikuwa sijajua hiyo trillion 1.5 inayosemwa, sasa Mh. Selasini enielewesha vizuri na nimeelewa! Kweli watoe majibu bwana kama wamekosea magazijuto warudie tena! Mwaka huu jiwe lazima afe kwa pressure, siku 2 tu Zitto kambana mpaka Jana anatoka hadharani akiwa afya mgogoro!!
Nimependa comment yako. Isije ikawa hata hao wanaowatisha wenzao hawajaelewa kama wewe ulivyokuwa hujaelewa au hata hawajasoma kabisa hiyo ripoti , learning is a process lakini hii principle inakuwa ngumu kwa wanaokariri.
 
Huyu CAG. naye vip mbona anakuwa muoga muoga
Kwani kuna sehemu alisema zimeibiwa ?

Yeye anataka Maelezo zipo wapi
Akisema zimeibiwa akienda mahakamani uthibitisho atatoa ?
 
Nimependa comment yako. Isije ikawa hata hao wanaowatisha wenzao hawajaelewa kama wewe ulivyokuwa hujaelewa au hata hawajasoma kabisa hiyo ripoti , learning is a process lakini hii principle inakuwa ngumu kwa wanaokariri.
Aah! Ni wepi hao wanaokariri?
 
Lakini mheshimiwa rais ndo mtu sahihi kujibu hoja ya CAG? Ila hilo alilouliza mheshimiwa Selasini tunahitaji majibu. Hili la CAG awaachie wahusika wajibu vinginevyo atachoka sana. Hivi atajibu mangapi mbona kero ziko nyingi sana?
 
Hivi mamsahib alipokuwa ananiambia kuna uber zinaendeshwa na watu wasiojulikana maana yake wanatafutwa wale wanaowashwawashwa wakunwe huko wanakowashwa? Nilikuwa sijaelewa. Kwani huyo supika naye vipi mbona anachelewa kuiunda hiyo tume,? Wajameni mtakatifu hawezi kufanya dhambi hata mara moja wako wengine tu
 
Wapinzani/vibaraka naona mmejifunza jinsi ya kuishauri na kuihoji Serikali iliyopo madarakani...ni jambo linalostahili pongezi. Bwana Selasini unaanza kupevuka kisiasa.
Hakuna shule inayofundisha namna ya kuihoji serikali hasa isiyozingatia maadili kama hii. Unaweza kuihoji whichever way.
 
Back
Top Bottom