Joseph Mbilinyi (SUGU) awasha moto Serena Hotel kwenye birthday yake, Rais Samia ahudhuria

Mh Sugu ameandaa Tamasha kubwa la Muziki siku ya Leo ndani ya Serena Hotel, huku akishirikiana na wanamuziki wenzake Wakongwe, Akiwemo Komando Jay Dee.

Sasa cha kushangaza ni aina ya watu waliohudhuria Tamasha hilo kabambe , wengi ni wanasiasa wa kiwango cha juu na wazungu , wale wenzangu wa kugongea fegi mpaka sasa sijawaona.

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

View attachment 2246165
===
Rais Samia
Leo tumekutanika hapa kwenye sherehe hii ya kusherekea miaka 30 ya kuwa msanii na miaka 50 ya kuwa Duniani, nikupongeze sana. Wewe ni mtu mwwnye majina mengi, Sugu, Mr two, ...... lakini mimi sitakuita Sugu maana umenyooka, titer hayo ni majina ya vijana watakuita vijana mimi nitakuita Joseph. Nakuita Joseph kwa kuwa mimi ni mama na wewe ni mtoto nimekuzaa.

Nimesikia hapa unaimba wimbo nimesikia tu neno Kilimanjaro basi najua ujumbe ni Kilimanjaro na pia nimeona watu wengine wanaimba hapa hadi Mkuu wangu wa Wilaya nikajiuliza huyu Mkuu wangu wa Wilaya anafanya kazi zangu saa ngapi? Lakini najua atakua na muda wa kujibalance na simvunji moyo bali namtia moyo kuwa aendelee.

Nikushukuru kwa kuandaa sherehee hii, qakati nimepata mwaliko wala sikusita, alikuwa kanipa tarehe ya kwanza ambayo nilikuwa na shughuli, nikamwambia nitakuletea mwakilishi na kama unataka niwepo basi sogeza mbele, akasema mama nasogeza, na leo nimefika hapa kama mgeni rasmi.

Nimekuja japa kwa sababu kadhaa, sababu ya kwanza ni kuwa mimi ni mama kwa Joseph, Joseph ni mwanangu na mama kufurahia mafanikio ya mwanae hiyo ni fahari kwa mama kuona mafanikio ya mwanaye.

Na sababu niyingine ni kuwa nimevutiwa na uamuzi wa Joseph kujiandikia kitabu, na ameniomba nikizundue kitabu kichachoitwa FROM THE STREAT TO THE PARLIAMENT nami leo nakizindua, kitabu hiki japo sijakisoma lakini najua kitakuwa na simulizi nyingi sana zinazomuhusu Joseph. Ukimuona Joseph unaweza sema ni kijana Mtukututu lakini sio mtukutu. Nimekuwa naye tangu Bungeni namfahamu Joseph nakumbuka aliwahi muudhi Spika wa bunge ikaamuriwa atolewe nje basi ile shika mguu mkono huku wanamtoa nje unaweza sema huyu ni machachari na mtukutu na vile wanamuita sugu ila si mtukutu.
Sawa James Mbowe.
 
Na mimi naungana na Sugu kumshukuru raisi, yule mwingine alikataa siyo tu kumtibu Lissu bali ata asiombewe kwa Mungu
Kwani maombi lazima mpige mikelele kwa pamoja, mkiomba mmoja mmoja mungu hasikii ama Magufuli aliingia hadi mioyoni mwenu akazuia maombi yasifike kwa mungu?
 
Wengi wao ni WAJINGA NA MALIMBUKENI mara wapatapo pesa!

Just imagine lei Msanii anayejiita Baba Levo anashindana na mjinga mwenzake kupiga danadana kwa furushi la milioni kumi kama mpira!

Kesho akiugua Kifaduro unadhani akiomba msaada atasaidiwa?

Wengine wamepata maisha kwa usanii wao, hata kama wakiomba msaada ama kusaidiwa na serikali ama jamii yao si mbaya...ila kwa ujinga huu wa Baba Levo au Daz Baba wasahau!
Waacheni watu waishi Maisha yao.
 
Mjumbe wa Kamati kuu ya CHADEMA Joseph Mbilinyi aka Sugu amemshukuru sana Rais Samia kwa kukubali kumtibu Joseph Haule aka Prof Jay kupitia serikali yake.

Prof Jay ni mjumbe wa Kamati kuu ya CHADEMA pia

Sugu ametoa shukrani hizo mbele ya Rais Samia katika ukumbi wa Serena le
ASANTE kwa Shukurani kwa RAIS WETU

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Hawa wasanii sijui pesa wanapeleka wapi jay tangu kitambo na ubunge juu hawezi kujitibia na mkewake anamiliki shule lakini bado tu

USSR
Unajua gharama za kutibu Figo Mkuu ? ,We unasema Prof Jay,Mobutu sese sell tu wakati wa mwisho wa uhai wake ili reportiwa Ana wakati mgumu kulipa bills
Na hapo kawa Rais Miaka zaidi ya 31 na Ana majumba na Mali nyingi lakini cash ilikata
 
Hawa wasanii sijui pesa wanapeleka wapi jay tangu kitambo na ubunge juu hawezi kujitibia na mkewake anamiliki shule lakini bado tu

USSR
Kuna muda ukibaki kimya inakupa heshima zaidi kuliko kubwabwaja tu,
Unajua gharama ya matibabu ya Joseph kwa siku? Unajua ni muda gani amekuwa kitandani?
Ukipata majibu, unaweza futa comment yako ili kulinda heshima uliyo nayo..
Nikukumbushe ugonjwa ni liability wala sio investment
 
Back
Top Bottom