Joseph Mbilinyi (SUGU) awasha moto Serena Hotel kwenye birthday yake, Rais Samia ahudhuria

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,641
218,091
Mh Sugu ameandaa Tamasha kubwa la Muziki siku ya Leo ndani ya Serena Hotel, huku akishirikiana na wanamuziki wenzake Wakongwe, Akiwemo Komando Jay Dee.

Sasa cha kushangaza ni aina ya watu waliohudhuria Tamasha hilo kabambe , wengi ni wanasiasa wa kiwango cha juu na wazungu , wale wenzangu wa kugongea fegi mpaka sasa sijawaona.

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Subpost%201%20-%20Usiku%20wa%20Sugu%20Serena%20Hotel%20(%20562%20X%20750%20).jpg
===
Rais Samia
Leo tumekutanika hapa kwenye sherehe hii ya kusherekea miaka 30 ya kuwa msanii na miaka 50 ya kuwa Duniani, nikupongeze sana. Wewe ni mtu mwwnye majina mengi, Sugu, Mr two, ...... lakini mimi sitakuita Sugu maana umenyooka, titer hayo ni majina ya vijana watakuita vijana mimi nitakuita Joseph. Nakuita Joseph kwa kuwa mimi ni mama na wewe ni mtoto nimekuzaa.

Nimesikia hapa unaimba wimbo nimesikia tu neno Kilimanjaro basi najua ujumbe ni Kilimanjaro na pia nimeona watu wengine wanaimba hapa hadi Mkuu wangu wa Wilaya nikajiuliza huyu Mkuu wangu wa Wilaya anafanya kazi zangu saa ngapi? Lakini najua atakua na muda wa kujibalance na simvunji moyo bali namtia moyo kuwa aendelee.

Nikushukuru kwa kuandaa sherehee hii, qakati nimepata mwaliko wala sikusita, alikuwa kanipa tarehe ya kwanza ambayo nilikuwa na shughuli, nikamwambia nitakuletea mwakilishi na kama unataka niwepo basi sogeza mbele, akasema mama nasogeza, na leo nimefika hapa kama mgeni rasmi.

Nimekuja japa kwa sababu kadhaa, sababu ya kwanza ni kuwa mimi ni mama kwa Joseph, Joseph ni mwanangu na mama kufurahia mafanikio ya mwanae hiyo ni fahari kwa mama kuona mafanikio ya mwanaye.

Na sababu niyingine ni kuwa nimevutiwa na uamuzi wa Joseph kujiandikia kitabu, na ameniomba nikizundue kitabu kichachoitwa FROM THE STREET TO THE PARLIAMENT nami leo nakizindua, kitabu hiki japo sijakisoma lakini najua kitakuwa na simulizi nyingi sana zinazomuhusu Joseph. Ukimuona Joseph unaweza sema ni kijana Mtukututu lakini sio mtukutu. Nimekuwa naye tangu Bungeni namfahamu Joseph nakumbuka aliwahi muudhi Spika wa bunge ikaamuriwa atolewe nje basi ile shika mguu mkono huku wanamtoa nje unaweza sema huyu ni machachari na mtukutu na vile wanamuita sugu ila si mtukutu.
 
Mh Sugu ameandaa Tamasha kubwa la Muziki siku ya Leo ndani ya Serena Hotel , huku akishirikiana na wanamuziki wenzake Wakongwe , Akiwemo Komando Jay Dee.

Sasa cha kushangaza ni aina ya watu waliohudhuria Tamasha hilo kabambe , wengi ni wanasiasa wa kiwango cha juu na wazungu , wale wenzangu wa kugongea fegi mpaka sasa sijawaona .

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

View attachment 2246165
Huyo Rwaitama nikafikiri ni Shaka salli wa VOA
 
Mh Sugu ameandaa Tamasha kubwa la Muziki siku ya Leo ndani ya Serena Hotel , huku akishirikiana na wanamuziki wenzake Wakongwe , Akiwemo Komando Jay Dee.

Sasa cha kushangaza ni aina ya watu waliohudhuria Tamasha hilo kabambe , wengi ni wanasiasa wa kiwango cha juu na wazungu , wale wenzangu wa kugongea fegi mpaka sasa sijawaona .

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

View attachment 2246165
Ndio Birthday yake au? Maana nilimsikia akisema Mh.Rais atahudhuria.
 
Back
Top Bottom