Joseph Kabila aahirisha Uchaguzi, asema serikali haina hela

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Augustin Matata Ponyo, amesema uchaguzi hautaweza kufanyika mwishoni mwa mwaka huu, kwa sababu serikali haina fedha za kuugharimia. Uchaguzi huo ni pamoja na ule wa urais, ambapo Rais Joseph Kabila atakuwa kikatiba amemaliza muhula wake wa pili na wa mwisho.

Miongoni mwa sababu zilizotajwa ni kushuka kwa bei za madini kama vile dhahabu, shaba na mali nyingi za asili katika soko la dunia.

Chanzo: DW Radio
 
Hawezi toka hapo Mpaka Mungu amuite kuungana na "Malaika" wengine huko mbinguni...

Ref:Mugabe
 
d.r.c inaweza ikawa ndio nchi tajiri kwa rasilimali kuliko hata nchi yoyote duniani, wana eneo kubwa sana lenye mto mkubwa, misitu, madini ya shaba,almasi,dhahabu,shaba etc, wanyama, maziwa na vivutio kibao, leo hii hawana hata hela ya kufanya uchaguzi!!!!???
waafrica kweli hawawezi kujitawala, wape bunduki na watabaki kuuwana tu!
 
Since day one ilifahamika uchaguzi unaofuata utatakiwa kufanyika lini; how comes maandalizi hayakufanyika? Baadhi ya viongozi Afrika hawastahili hata kuitwa viongozi.
 
halafu agombee, ashindwe
Mkuu, yeye ndiye kashikilia mpini atahakikisha anashinda si unajua tena tawala za Kiafrika - baadhi ya nchi xinaonekana kupania kurudisha tawala za kifalme taratibu taratibu, kuja kufikia mwaka 2040 karibu Bara lote litakuwa limejaa viraka viraka vya tawala za kifalme.
 
Mkuu, yeye ndiye kashikilia mpini atahakikisha anashinda si unajua tena tawala za Kiafrika - baadhi ya nchi xinaonekana kupania kurudisha tawala za kifalme taratibu taratibu, kuja kufikia mwaka 2040 karibu Bara lote litakuwa limejaa viraka viraka vya tawala za kifalme.
kweli,
 
Yuko sahihi, hamna haja ya kupoteza hela kwenye chaguzi za Kiafrika maana ni usanii mtupu.
 
Kama ni kweli waziri mkuu amesema hayo basi anamaanisha hivyo na ndio hakutakuwa na uchaguzi tena mpaka baada ya miaka mitano mingine. Hayo ni mawazo ya mkulu mwenyewe Joseph Kabila.

Kabila ametajwa na jarida la Forbes la mwezi Juni mwaka 2014 kwamba alikuwa ana utajiri wa kiasi cha dolali 15 billion na pia mdogo wake bwana Soloumane yeye amekwishajinyakulia kiasi cha dolali 300 milioni.

Hizi fedha zote zimehifadhiwa nje ya Congo DRC na hakuna anaeweza kuzifikia,

Anaweza kufanya moja ya mambo mawili, kwanza kuruhusu ipigwe kura ya maoni kama Rwanda ambapo ataruhusiwa kuendelea zaidi kutawala.

Au atafuta uchaguzi ulipo sasa na badala yake uchaguzi wa raisi utafanyika kwenye majimbo ambapo madiwani na wabunge watapiga kura/

Hizi zote ni njia za kifisadi.
 
kaamua kusigina demokrasia

Yap, katika watu wanaopinga kwa nguvu zote hili neno demokrasia ni Joseph Kabila.

Huwa mara nyingi anasema hapati tafsiri sahihi ya neno hili kwa Kiswahili.

Yeye anapendelea nchi za Afrika ziwe na mfumo wa demokrasia yake zenyewe na sio za kuiga kutoka mataifa ya Ulaya na Marekani.
 
Dah! Africa kunavituko, Subiri wamtandike shaba, ndio wafusiwake wajue kuwa walicho mshauri ni ujinga.
 
Back
Top Bottom