Jonathan James mdukuzi maarufu (Hacker) katika historia ya Dunia

makindaOG

Member
Aug 15, 2020
11
13
Jonathan alizaliwa tarehe 12 mwezi Desemba mwaka wa 1983.

Alipata umaarufu alipohukumiwa kifungo akiwa na umri wa miaka 16 kwa makosa ya udukuzi aliyofanya akiwa na umri wa miaka 15.

Jonathan alidukua mifumo ya kompyuta katika wizara ya Ulinzi ya Marekani. Jonathan pia aliwahi kudukua mfumo wa Kompyuta wa NASA na kuiba programu yenye thamani ya dola milioni 1.7.

Je, aliwahi kuadhibiwa?

Jonathan alipatwa na hatia na kupewa kifungo cha miaka 10 bali alibahatika kupunguziwa kifungo hicho hadi miezi 6. Jonathan alipigwa marufuku ya kutumia kompyuta

Katika mwaka wa 2008 Jonathan alifariki kutokana na jeraha baada ya kujipiga risasi mwenyewe.

Subscribe now.
 
Bongo siku ya kukamatwa tu ungesikia "jambazi sugu auawa katika mapambano na jeshi ra porisi" mpaka ndugu waje kumtambua pamoja na wanafunzi wenzake, wengine tushasahau. Marekani ukiweza kuwadukulia mifumo yao ya ulinzi, wanafanya makubaliano na wewe na unatakiwa kuwafanyia kazi na unalipwa pesa ndefu na uraia juu wewe na familia yako. Afrika hata ukitengeneza chupa ya chai, TCIA, TISS, POLISI, TBS, EWURA, TANROADS, MDA, TARURA, TANESCO na wengine wengi wanabisha hodi mlangoni kutaka uwaoneshe kibali cha kufanya jaribio la kutengeneza kifungashio hatari cha kuhifadhia joto
 
Utakamatwa kwa kumiliki kifaa kinaweza kusababisha mlipuko.
 
Back
Top Bottom