SIKU chache baada ya msanii wa kizazi kipya, Ali Kiba, kudai kuwa anamchukulia mwanamitindo Jokate Mwegelo kama rafiki yake, mrembo huyo ameibuka na kusema huenda aliteleza kutoa kauli hiyo.
Jokate alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki hii alipokuwa anahojiwa kwenye kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds Tv, ambapo mrembo huyo alisema kauli hizo huenda zimetolewa kimakosa.
“Sifikirii sana maana mimi ni mtu ‘positive’ nataka niamini hawakumaanisha, sasa sijui waliteleza au walikosea,” alisema mrembo huyo aliyewahi kushika nafasi ya pili kwenye shindano la Miss Tanzania mwaka 2006.
Mrembo huyo alikwenda mbali kwa kusema: “Unajua katika maisha huwezi kumlazimisha mtu kuona thamani yako, wanasema tenda wema nenda zako mengine ni matokeo na sipendi kulizungumzia sana maana siku hizi watu wanapenda sana kuokota maneno wanayatengeneza wanavyojua wao.”
Kiba na mama yake walimkana Jokate kwenye sherehe ya kumpongeza msanii huyo baada ya kurudi kutoka Afrika Kusini na tuzo ya MTV.
Tuzo hiyo ambayo awali alitangazwa Wiz Kid kwamba ndiye aliyeshinda lakini baadaye uongozi wa MTV wakakiri mshindi halali alikuwa ni Ali Kiba na kuahidi kumpa tuzo yake nchini Afrika Kusini.