Joka Jeusi Kwa sasa yupo katika anguko la kiuchumi

Jokajeusi

JF-Expert Member
Jun 1, 2018
6,305
10,582
Mpo poa wakuu.

Wiki hii imekuwa wiki ya majanga sana kwangu. Nimejikuta nikiwa na presha huku tumbo likiwaka moto. Mimi ni mfanyabiashara mdogo. Najishuhulisha na biashara ya saloon ya kiume, biashara ya nguo na Bodaboda.

Picha linaanza siku ya jumatatu ambayo nilipigwa faini ya elfu hamsini kwenye kibiashara changu cha nguo chenye mchanganyiko na vipodozi. Faini yenyewe ni kutokuwa na Leseni. Nilibembeleza lakini nilikaziwa mwanzo mwisho licha ya kujieleza kuwa mimi ni kijana mdogo niliyemaliza chuo mwaka jana(2017) hivyo mtaji wnagu bado ni mdogo. Lakini maneno yangu yalikuwa batili. Niliwapa huku roho yangu ikiniuma na nikilaani ijapokuwa kweli mimi ndiye mkosaji. Kimbembe ilikuwa kesho yake ambapo nilipigwa na butwaa nilipokutwa duka langu la nguo limevunjwa na kuibiwa. Hali niliyoisikia mwilini mwangu haielezeki. Nadhani wafanyabiashara na watu wazima mnanielewa hasa ukizingatia kipindi hiki kilivyokigumu.

Boda boda yangu jana nililetewa taarifa imeibiwa. Nilichokifanya hapa ni kumuweka sero dereva mpaka muaafaka utakapopatikana.

Asikuambie mtu usiku mzima sikulala, nilifikiria mtaji wangu wa nguo ulivyopotea na sikujua nitaurudisha vipi. Habari ya boda boda nayo ndio ilinipasua kichwa.

Kilichonifanya niandike mada hii.

Jana alhamisi nikiwa ofisini kwangu nilishuhudia ajali ya moja mbaya sana. Gari iligongana na bodaboda na dereva alivunjika mguu. Watu walijaa kama ujuavyo watanzania.

Baada ya ajali ile moyo wangu ulipoa, ulitulia na huzuni iliisha. Niliomba msamaha Mungu kwa kumlaumu kuhusu watu walioniibia dukani kwangu na boda boda yangu. "Je ingekuwa ndio mimi nimepata ajali na kuvunjika miguu ingekuwaje?" Nilijiuliza. Na hapo ndipo nilipojifunza kuwa mshukuru Mungu kwa kila jambo haijalishi unapitia wakati gani. Wapo wenzako wanapitia vipindi vigumu zaidi kuliko wewe.

Kwa sasa nimepoa, Wito wangu kwa vijana wenzangu, haijalishi maisha ni magumu kiasi gani. Haijalishi unapitia mangapi yenye kuumiza. Mshukuru Mungu kwa kila jambo ikiwa umepewa pumzi na afya njema.

Joka Jeusi Kwa sasa yupo katika anguko la kiuchumi.
Karibuni
 
Cheti Chake je?
 
Pole sana mkuu, kwetu tunasemaga ''Bishanga a'bashaija'' ikiwa na maana ya 'Huwakuta wanaume'. Hivyo piga moyo konde maisha yasonge.
 
Pole sana mkuu,By the way andiko lako limenikumbusha kitu kimoja kilichowa nitokea.Kwa sasa hivi huwa aridhika tu na maisha regardless maana soometimes.Ni kumshukuru Mungu kwa kila jambo

Kweli chifu, naanza kuwa mtu mzima kwa kweli
 
Kuna siku nitaandika kuhusiana na kushukuru kwa kila jambo! Hakika likupatalo wewe kuna mwingine a nahisi angekuwa na kama hilo lako kwake ingekuwa afadhali. Ndo maana wimbo wa "ni salama rohoni mwangu" has always been my fav. Song....hongera kwa kutambua hilo na pole sana kwa yote yalokukuta.
 
Ahsante sana Mkuu
 
Back
Top Bottom