PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,202
- 8,787
Wanajamvi,
Jioni hii tumepata barua ya Joining instructions ya mtoto tunaeishi nae ndani, tukaamua tukusanyike familia yote tusome wote kwa pamoja ili tujue tutajifunga vipi mkanda kumwezesha mtoto aende kidato cha Tano huko Sanya Juu Sec.
Basi mtoto wetu mdogo mjanja sana amepewa barua hiyo aisome kwa sauti, huku anayeenda shule akiwa na kalkuleta ya kukokotoa majumlisho. Tumeenda vizuri vipengele vyote vya hela vikaisha.
Tulipofika kwenye kipengele C ndipo tulipokumbana na mfadhaiko wa aina yake, ambapo heading imeandikwa hivi; MAMBO YATAKAYOMFUKUZISHA SHULE MWANAFUNZI.
1.Kulawiti, Kulawitiwa, Kufanya Ushoga na Kufanya Uasherati.
Furaha yetu yote imeingia dosari kwa kipengele hicho maana imetupa picha kuwa huenda shule hiyo imeshamiri na matendo hayo ndiyo maana ikawekwa No1!
Ukiacha hayo mawazo yetu, watoto nao, hasa huyo msomaji wameanza kuuliza kwa shauku maana ya maneno hayo, kitendo kilichotupa wakati mgumu sana, hadi tumeomba nyumba yetu ipigwe tsunami dakika hiyohiyo na wote tusipone!
Hebu wazazi wenzangu niambieni, je na nyie huko joining instr. z watoto wenu zina vitu vya namna hiyo?