Joining instruction Lufilyo sec school hii hapa

Spellan

JF-Expert Member
Jun 15, 2011
307
14
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
HALMASHAURI YA BUSOKELO,
SHULE YA SEKONDARI LUFILYO,
S.L.P 362,
TUKUYU.
SIMU NA. 0784424024 / 0767119911.
Kumb. Na. SSL/MNF/FV-14/……….
Mzazi/Mlezi wa Mwanafunzi………………………………………………………
S.L.P …………………………………..
…………………………………………..
YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI LUFILYO KIDATO CHA TANO (V) HALMASHAURI YA BUSOKELO –JULAI 2014.
Ninafurahi kukuarifu kuwa umechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule ya Sekondari Lufilyo mwaka 2014 kwa masomo ya …………………… Shule ipo umbali wa kilomita 58 Mashariki mwa mji wa Tukuyu na Kilomita 16 Kusini Mashariki kutoka Halmashauri ya Busokelo ambako ni makao makuu ya wilaya ya Busokelo.Usafiri kutoka mji wa Tukuyu kwenda shule ya sekondari Lufilyo unapatikana karibu na mkabara na stendi ya Tukuyu kituo kinaitwa uwanjani kwa nauli ya Tsh 5000/= kuanzia muda wa saa nne asubuhi mpaka saa nane na nusu mchana.
Muhula wa kwanza wa masomo utaanza tarehe………21/07/2014………………………… unatakiwa kuripoti shuleni, utakapofika unatakiwa kuripoti kwa mwalimu wa zamu.
Kauli mbiu ya Shule ni “ELIMU NI NURU” (EDUCATION IS LIGHT) .
1.0 MAMBO YA MUHIMU YA KUZINGATIA
1.1 SARE YA SHULE NA MAVAZI MENGINEYO
1.1.1 WAVULANA
Sare ya shule ni Suruali mbili (2) au zaidi nyeusi zenye malinda mawili na zisibane (sio vimodo) na koti lake la suti rangi nyeusi sawa na kitambaa cha suruali, Shati mbili(2) au zaidi nyeupe za mikono mirefu pamoja na tai ndefu nyeusi. Jozi mbili za viatu vya ngozi rangi nyeusi vya kufunga na kamba visivyo vya mchongoko na jozi mbili za Soksi nyeusi ndefu zisizo na maandishi na Mkanda mweusi kiunoni. Kwa wanaosoma Sayansi aje na koti jeupe kwa ajili ya Practical maabara.
Shuka mbili rangi ya bluu, blanketi, chandarua, muamvuli, Tochi kwa tahadhari na Godoro la futi mbili na nusu kwa sita. TShirt mbili au zaidi za kora (fom six) rangi ya Dark Blue na ufito mweupe kwenye kora na mikononi za kuvaa baada ya masomo ( nembo itawekwa shuleni). Pia Fulana mbili na bukta zisizo na maandishi wala picha, raba jozi moja kwa ajili ya michezo. Mahitaji ya bwenini- Aje na Ndoo ndogo mbili, fagio chelewa, soft broom, mopa, jembe na mpini wake na fyekeo/kwanja. Pia sahani, kikombe, bakuri na kijiko vya chakula pamoja na sanduku(tranka.)
Utapaswa kuja na daftari kubwa(counter book) zisizopungua saba(7), Folder file moja, Rimu moja (photocopy paper A4 nyeupe)
Ili upokelewe ni lazima uje na cheti cha kuzaliwa, cheti cha matokeo kidato cha nne na leaving certificate.
1.1.2 WASICHANA
Sare ya shule ni Sketi mbili (2) nyeusi zenye malinda kati ya 8 hadi 12 zenye urefu unaogusa viatu na koti lake la suti rangi nyeusi sawa na kitambaa cha sketi, Shati mbili(2) rangi Right blue za mikono mirefu pamoja na tai ndefu nyeusi. Jozi mbili za viatu vya ngozi rangi nyeusi vya kufunga na kamba visivyo na kisigino kirefu, jozi mbili za Soksi nyeupendefu zisizo na maandishi, nywele fupi. Kwa wanaosoma Sayansi waje na koti jeupe kwa ajili ya Practical maabara.
Shuka mbili rangi ya pinki, blanketi, chandarua, muamvuli, Tochi kwa tahadhari na Godoro la futi mbili na nusu kwa sita.
Shamba dress(2) rangi ya zambarau(pupple)ni gauni mshono wa solo lenye lainingi. Taulo moja kubwa na kitenge kimoja tu.TShirt mbili au zaidi za kora (fom six) rangi ya Dark Blue zenye ufito mweupe kwenye kora na mikononi za kuvaa baada ya masomo ( nembo itawekwa shuleni). Pia Fulana mbili na bukta zisizo na maandishi wala picha, raba jozi moja kwa ajili ya michezo. Mahitaji ya bwenini- aje na Ndoo ndogo mbili, fagio chelewa, soft broom, mopa, jembe na mpini wake na fyekeo/kwanja. Pia sahani, kikombe, bakuri na kijiko vya chakula pamoja na sanduku(tranka).
Utapaswa kuja na daftari kubwa(counter book) zisizopungua saba(7), Folder file moja, Rimu moja (photocopy paper A4 nyeupe)
Ili upokelewe ni lazima uje na cheti cha kuzaliwa, cheti cha matokeo kidato cha nne na leaving certificate.
NB: Kwa Wote Ni Marufuku kuja na mavazi mengine tofauti na yaliyotajwa hapo juu( ya nyumbani). Ni marufuku kuja na simu, ukishikwa utafukuzwa shule. Pia marufuku kuja na kutumia vyombo vya umeme kama pasi, heater, jiko n.k. Vipodozi kama wanja, ina, rangi kucha, poda n.k haviruhusiwi kabisa.
1.2 ADA NA MICHANGO YA SHULE
Ada ya shule kwa mwaka ni shilingi elfu sabini (70,000) unaweza lipa Tsh. 35,000/= katika muhula wa kwanza na wa pili ukamalizia Tsh. 35,000/= au ukalipa fedha yote Tsh 70,000 kwa mkupuo.
Michango inayotakiwa kulipwa na mzazi ni ifuatayo :
i. Tsh 5,000/- kwa ajili ya tahadhali, ii. Tsh 5,000/- kwa ajili ya kitambulisho,
iii. Tsh. 10,000/- gharama ya umeme, iv. Tsh 5,000/- Ulinzi, v. Tsh 10,000/- ajili ya Taaluma.
vi. Ukarabati Tsh. 10,000/ vii. Mahafali kwa mwaka Tsh 10,000/- vii. Mchango wa dawati Tsh 30,000/- . Pia pesa ya matibabu Tsh 10,000 aje nayo mkononi kama hana kadi ya bima ya afya.
NB; Fedha zote zilipwe kwenye akaunti ya shule isipokuwa fedha ya mchango wa dawati, Ukarabati, mahafali na matibabu ni lazima aje nazo shuleni atazilipa kwa maelekezo.
Akaunti ya shule ni Na. 6142300218 NMB – TUKUYU
2.0 SHERIA NA KANUNI ZA SHULE
Shule hii inaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya Elimu ya mwaka 1978. Aidha inazingatia miongozo yote inayotolewa na wizara yenye dhamana ya Elimu nchini. Hivyo unatakiwa kuzingatia mambo ya msingi ambayo yatafafanuliwa kwa maandishi na utapewa nakala yako mara baada ya kuripoti shuleni.

“KARIBU SANA SHULE YA SEKONDARI LUFILYO”

MKUU WA SHULE
 
Hizo fedha zingine kwanini hazingii kwenye akaunti ya shule? Hapa naanza kuona harufu ya ufisadi. Halafu shule mbona ina ukoloni mwingi sana, mara sijui bukta fulana mbili, sasa si wanaigeuza shule kuwa gereza hawa dah!
 
da joining nimeionaaaaaaaaaa asante xana kwa maana nilikuwa nahangaikaaa kuipata ahaaaaaaaaaa #lufiland

:A S 11::A S wink::llama::hail::hungry::cool2::mad::couch2::bange::shock:
 
Hizo fedha zingine kwanini hazingii kwenye akaunti ya shule? Hapa naanza kuona harufu ya ufisadi. Halafu shule mbona ina ukoloni mwingi sana, mara sijui bukta fulana mbili, sasa si wanaigeuza shule kuwa gereza hawa dah!

hahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahatwende hvyo hvyo tu mzeiyah
 
Lufilyooooo,nmepiga hapo advance ni shule tulivu kwa kusoma........mazingira yake ni tulivu,chin ya mkuu wa shule majuto mkosa sura tem
 
Hivi kumbe serikali haipeleki shuleni hela za kulipia umeme? Maana nimeona kwenye hii shule ya Lufilyo kila mwanafunzi anatakiwa kwenda na sh 10000 za umeme!

Ya mafagio, kwenda na (chelewa na dekio etc) yananishangaza mpaka najisikia kutetemeka!
 
Cjui kwa sasa enz zetu tulikuwa tuna2mia pasi had heater afu hakukuwa na madem,darasan ilikuwa ni uamuz wako kuingia,walimu walikuwa hamna,msuli yatima ndio ulihusika sana
 
Back
Top Bottom