John, stuka au utaachwa solemba pale Ubungo mataa!

John, stuka au utaachwa solemba pale Ubungo mataa!

gollocko

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
2,945
Reaction score
2,281
Watoto wa mjini wanasema ukizubaa,utaingizwa kingi.

Napenda kukupa tahadhali ewe mkuu John, unatakiwa ushtuke mapema kwani mambo yanavyokwenda utalala doro!

Mkuu hujiulizi, inakuwaje watu wateuliwe kushika nyazifa kubwa siku tatu kabla ya kukabidhiwa rungu? Tena yule wa mwisho aliteuliwa kuwa katibu tawala pale Lindi siku moja tu kabla hujaapishwa, mwingine ukapewa umwapishe kuwa mshauri wako wa mikataba yote utakayoingia, ikiwa ni masaa 18 tu toka upewe rungu, duh! Kwani hujui kule Kusini kuna nini kinatakiwa?

Haya sasa, leo unatenguwa uteuzi halafu unafanya uteuzi kwa mtu huyo huyo kuwa mbunge, siku hiyo hiyo mtu huyo anajitoa kutaka cheo kile na siku hiyo hiyo anataka kingine hivi ni kweli haya maamuzi ya kiswahili umeyatoa wewe jembe letu John au umebambikiwa?

Haya juzi uneenda kuikagua ile mashine pale hosipitalini, ikatengenezwa, siku tatu tu imeharibika. Tena, imeharibika moyo wake. Kwa kukufafanulia tu ni kuwa, ile mashine imeharibika kifaa kiitwacho (Redio frequence amplifier) ambacho ndio moyo wake, bila hicho hakuna hiyo mashine!! Kwa mujibu wa mtandao wa hiyo kampuni iliyopewa zabuni ya ya ukarabati kifaa hicho kinauzwa usd 97,000! Mil. 200 za madafu, upo mkuu?

Ukienda lesi tena unapigwa kivingine hujashtuka tu?

Mkuu John ngoja nikuache, usiposhtuka sasa, solemba pale Ubungo mataa inakuhusu !
 
Mkuu pokea saluti zangu. Nimfahamuvyo John si mtu wa utawala wala wa rasilimali watu. Sasa hapa ndiyo watamchezea sana kwa kuwa hana ujuzi wa kupanga wachezaji. Kuna watu wanataka wandelee kuongoza kwa remote control na ndicho kinachofanyika. Kumbuka John amewekwa pale na baba yake aliyemleta kwenye uongozi tangu alipoanzia unaibu waziri halafu sasa kwa 2015 dili ikachezwa na baba yake huyo huyo kwa kumaliza yale makundi mawili. Kwa suprise wale walioandaliwa na mfalme wakaanguka kwa technical knockout. Sasa jua John hakuwa katika hesabu ya Mfalme na niseme mfalme hampendi kabisa!!! Kwa mantiki hii mfalme ili kulinda himaya zake alizojijengea ni lazima kuhakikisha katika mihimili anaweka watu wake. Watch out JOHN. Amka simama, haraka sana.
 
Naona John bado anadhani wanaomchekea wanampenda, hajui wao pesa mbele.
 
Ni ngumu sana John kuikwepa mishale ya Vasco, ajiandae kupambana na wanafiki ndani ya chama chake tofauti na anavyofikiria kuwa wanafiki wanatumwa na viongozi waliokihama chama.
 
Bilion 2 toka hazina kwenda Muhimbili halafu ndani ya wiki mashine inakufa? Hii kali.
 
Zinduka toka usingizini John uwanyang'anye remote control vinginevyo siku si nyingi utakuwa butu kama kisu kisichokuwa na makali.
 
Ni ngumu sana John kuikwepa mishale ya Vasco, ajiandae kupambana na wanafiki ndani ya chama chake tofauti na anavyofikiria kuwa wanafiki wanatumwa na viongozi waliokihama chama.

Lazima awe mjanja kama sungura la sivyo, zitabaki hadithi zile zile za wasukuma wafikapo kariakoo kwa mara ya kwanza.
 
Ni ngumu sana John kuikwepa mishale ya Vasco, ajiandae kupambana na wanafiki ndani ya chama chake tofauti na anavyofikiria kuwa wanafiki wanatumwa na viongozi waliokihama chama.
Hakuwa mjinga alipo waonya tanesco na aliposema kuna watu mchana ni ccm jioni ukawa kwa background yake na watu wanavosema wanaomjua huwa ana visasi vibaya mno. kwa hiyo hata washika remote inabidi wawe makini coz hii ni catch me if you can
 
Masikinii John!!!....John kata kamba usimame mwenyewe kama ilivyokuwa kwenye kampeni....
 
Uzuri wa john huwa anajielewa mwenyewe. aliwahi kuzenguana na mrisho na peter waka retain barua zake za kujiuzuru. wanaweza waka mremote ila siku watakayo kosea botton au betri kuisha ndo mwisho wa sinema john is unpredictable lets wait time will tell

Duh! Major, mpaka wakosee burton si ndio atakuwa keshatumbukia topeni?
 
Heshima kwako kaka, umeeleweka vyema. Tumuombee mema John, me nasubiri atupe Waziri Mkuu hapo ndo nitajua nini kinaendelea hapa.
 
Back
Top Bottom