John Shibuda : Hakuna Makutano ya Kifikra chaguzi za mitaa

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200
13 Oct 2019
Hakuna makutano ya kifikra baina ya Ofisi mbili kuu, yaani Ofisi ya Rais Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inayosimamia uchaguzi wa serikali za mitaa na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo inasimamia masuala ya siasa, hayo yamesemwa na Mzee John Shibuda na hivyo anasema kuna pahala pana mushkeli mkubwa katika matayarisho na mipango kuelekwa uchaguzi wa serikali za mitaa.

John Shibuda anasema hoja nzuri za wadau wa siasa kama vyama vya siasa zilipuuzwa na serikali na ndiyo tunaona hali hii ya kusuasua katika kujiandikisha.

Wakati taifa likielekea wiki ya kilele cha maadhimisho ya kifo cha baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere pia tunaelekea katika hitimisho la wiki ya uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mtaa. Zoezi hilo limeonekana kulega lega kwa baadhi ya maeneo. Je, kuna tatizo mahali? Tunajadili hayo kiundani katika MIZANI YA WIKI inayoongozwa na Nurdin Selemani akiwa na mkuu wa wilaya ya kinondoni, Daniel Mchongolwa, mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa John Shibuda, mhadhiri wa idara ya sayansi ya siasa ya chuo kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda.
Source: Azam TV
 
Oktoba 2019

Mhe. Suleiman Jafo waziri Ofisi ya Rais anayesimamia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) abainisha taarifa za ripoti na takwimu zaonesha mwamko kuelekea kujiandikisha ni mdogo

 
April 2019
Bungeni Dodoma

Tume ya Uchaguzi haiwezi kusimamia uchaguzi wa mitaa - Waziri Mkuu asema. Waziri Mkuu ndiy kiongozi wa shughuli za serikali ktk Bunge la Tanzania wakati akijibu hoja za baadhi ya wabunge kuwa vipi waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa apewe jukumu la kusimamia uchaguzi wa kidemokrasia moja kwa moja wakati Tume ya Uchaguzi ipo kisheria.

 
Ngoja Waendelee kutafuta Mwanga wakati wanaye papo hapo walipo na Wanamjua kuwa ni Jiwe.
CCM ina Utawala wa hovyo kupita kiasi. Lakini ndiyo hivyo bado hatujitabui Watanzania.
 
Back
Top Bottom