John Pombe Magufuli faces cash crisis

Kokola

Senior Member
Joined
Sep 5, 2015
Posts
135
Reaction score
78
Wakuu nimesoma hii online je ni kweli..?

======================


Source: thecitizen
 
Wadanganyika ktk ubora wetu.... unapewa jiwe unatoa dhahabu ndio uzuzu aliosema hayati JKN
 
CCM ni ileile.

Ukawa tutaisoma namba.
 
Guys...hii issue ya financial crisis ni uzushi mtupu. Juzi hapa zaidi ya billioni 15 na ushee imepelekwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu. Na kana kwamba hiyo haitoshi, trillion 1.7 imekusanywa na TRA kwa mwezi wa huu wa kumi tu.
 
Guys...hii issue ya financial crisis ni uzushi mtupu. Juzi hapa zaidi ya billioni 15 na ushee imepelekwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu. Na kana kwamba hiyo haitoshi, trillion 1.7 imekusanywa na TRA kwa mwezi wa huu wa kumi tu.

Kuna salio au pocket to mouth??!!!!!!
 
Guys...hii issue ya financial crisis ni uzushi mtupu. Juzi hapa zaidi ya billioni 15 na ushee imepelekwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu. Na kana kwamba hiyo haitoshi, trillion 1.7 imekusanywa na TRA kwa mwezi wa huu wa kumi tu.

wewe ni sawa na mbuni anayeficha kichwa chake ndani ya udongo while kiwiliwili chote kinaonekana.
kapu jeupe pee.
 
Tanzania haiwezi kundelea ikiwa mikononi mwa ccm ni porojo mwanzo mwisho, aliyeondoka ccm aliyepo ccm na hakuna pesa, angechukua upinzania tungesema amekomba kumkomoa kama Nigeria, hii kwa wa watanzania wenye akili bila kujali siasa watajua wanaumia, kwani kodi zitawandama bila serekali kuangalia uhalisia wa unacholipia, bei zitapanda nahaya hayaangalii chama.
Watanzania waamke wapinge vitu kama hivi bila kujali vyama, na vizuri kila mwenye kadi ya chama cha siasa aichane ili asiwe mtumwa wa hicho chama, ila ampigie kura ambaye akiwa madarakani alimtete ili kupata elimu bora kwa bei nafuu, kulipa kodi stahiki, huduma ya fya bora, kuinua uchumi, na usalama wake mwenyewe nk.
 

fisiem bongolala wanakata mauno tu 'ccm ni ile ile"
 
Naona wazee wa mita 200 bado mnaweweseka, deraya 700 bado zipo, leteni tu fujo muone!
Kwa akili zenu fupi mnadhani zoezi la uchaguzi sio costful! hakuna nchi inayofanya uchaguzi ikabaki financially stable katika miezi miwili hadi mitatu ya mwanzo
 
Ambane jumanne Kimweri aka jk arudishe fweza
 
Habari za Asubuhi GT's,


Nimeona magazeti ya Leo yakipambwa na taarifa za Mkurugenzi mkuu kushughulikia wakwepa kodi.


Naomba pia kuipongeza TRA kwa makusanyo mazuri. Baada ya pongezi hizo naomba kuendelea.


Awali ya yote kama nilivyosema hapo juu nimefurahi na taarifa Yake ya makusanyo na kuwa wako kwenye asilimia zaidi ya 90 ya malengo waliyojiwekea.


Kupitia taarifa hiyo naomba kuchangia yafuatayo ili tuendelee kuboresha zaidi ukusanywaji wa kodi ktk nchi yetu.


Ukusanywaji sahihi wa kodi utaondoa bajeti tegemezi na tutaweza kutoa huduma za jamii kwa wakati hasa tutakapobana matumizi yasiyo ya lazima.


1. JE MALENGO WALIYOJIWEKEA (Targets) YAKO SAHIHI??
Nauliza hivi baada ya ripoti kuwa na excellence performance wakati yeye mwenyewe anasema sasa amepewa rungu atashughulika wakwepa kodi hasa wakubwa.


Ina maana hii ripoti Yake hao wakwepa kodi wakubwa makadirio yao hayakuwekwa kwenye targets?


2. Je hao wakwepa kodi wakubwa (defaulters) ni kina nani? Mbona taarifa Yake haikuwataja???


3. Je hadi sasa kodi ambayo imekwepwa kwa maana kuwa iko due na haikukusanywa ni Tshs ngapi???


4. Je ana mikakati gani ya kukusanya hayo madeni ya hao defaulters? Nilitegemea kwenye ripoti Yake angetoa ultimatum kuwa baada ya mwezi wawe wote wamelipa hayo madeni vinginevyo sheria ichukue mkondo wake.


5. Atoe level ya compliance regional wise.


6. Tunataka kuona realistic targets katika ukusanyaji wa kodi. Sio kuweka low targets halafu watu wanajisifia tumevuka malengo wakati malalamiko ya watu kukwepa kodi ni kila mkoa.


7. Wakati wa kuweka malengo watenganishe kodi inayotokana na mishahara (PAYE) na hiyo ya wafanya biashara ili tuone magnitude ya ukusanyaji katika kila eneo.


8. Taarifa za walipa kodi na defaulters zisiwe siri Kama kuna nia ya kweli ya kuboresha mfumo wetu wa kodi.


Naomba wadau wengine muongezee hoja ili kusaidia suala zima la ukusanyaji kodi ktk nchi yetu.


Mwisho ni ushauri kwako wewe usiyelipa kodi ujue huduma mbovu ktk jamii na Vifo vinavyotokana na kukosekana fedha vinakuhusu.


Hizo damu ziko mikononi mwako. Kwenda kwako misikitini au Kanisani ni bure bora ulale nyumbani.


Pia mfanyakazi yoyote wa TRA anayeshiriki ktk uovu huo. Basi mikono Yake imejaa damu za watu waliokufa sababu ya kukosa huduma mbalimbali za jamii ambapo pesa hizo wewe unahusika kuzipoteza.


Kila mtu asafishe MIKONO Yake tuendelee na kazi kwa kasi ya UWAJIBIKAJI; UFUATILIAJI; na UADILIFU.


Karibuni kwa michango zaidi. Tanzania ni yetu sote na sisi ndio tunaoamua mustakabali wa nchi yetu.


Queen Esther

Wakuu nimesoma hii online je ni kweli..?

======================



Source: thecitizen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…