John Nyerere kuagwa leo, Msasani

John Nyerere kuagwa leo, Msasani

Asante

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2009
Posts
2,086
Reaction score
1,082
attachment.php


MAMIA ya wakazi wa Dar es Salaam leo wanatarajia kutoa heshima za mwisho kwa John Nyerere (58), ambaye ni mmoja wa watoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

John alifariki dunia juzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alikokuwa amelazwa.

Makongoro Nyerere ambaye ni mtoto mwingine wa Mwalimu Nyerere, alisema Dar es Salaam jana kuwa mwili wa John utasafirishwa kesho kwenda Mwanza na kisha kupelekwa kijijini kwao Butiama Mkoa wa Mara kwa maziko.

"Misa ya kumuombea John itafanyika hapa Msasani nyumbani kwa Mwalimu na kufuatiwa na utoaji wa heshima za mwisho," alisema Makongoro, ambaye ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

John alitumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na alishiriki Vita vya Kagera vya 1978 na 1979, vilivyolenga kumng'oa nduli Iddi Amin wa Uganda.

 
Ukoo nakupenda sanaa hatakamasijapata URITHI hapo. angekuwa nanii. kafa tumejazana diamond ama karimujeeholi
 
Mbona unakuwa mgumu kuelewa?
Jana uliambiwa kuwa huyu Yericko hana uhusiano wowote na familia ya Mwl Nyerere! Acha utoto ndugu.
Wewe ndio hujui, hao waliokuambia wanaitwa akina nani nyerere? Huyu ni mtoto wa mwalimu na jina lithibitisha.
 
Ndio namsikia leo.... hawa watoto wa mwalimu mbona wanajificha hivi.. RIP
 
Back
Top Bottom