TANZIA John Mwankenja auawa kwa risasi

Poleni Watanzania wote kwa mtanzania mwenzetu. Poleni familia ya wafiwa.

Chama Cha Mapinduzi kimempoteza mmoja wa wapiganaji wake makini, pole sana Mh. J.K (M/Kiti) na Ndugu W.Mukama (Katibu Mkuu) kwa msiba huu mkuu na wana-CCM wote nchini. Poleni pia wananchi na wakazi wa Rungwe kwa kumpoteza M/Kiti wa Halmashauri yenu...hakika hili ni pigo kubwa kwa Rungwe na Taifa kwa Ujumla.

Mungu, ailaze mahali pema peponi Roho ya John Mwankenja. Amina:A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose:
 
Poleni sana wafiwa........Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu........
Umalafyale Abhatule......
 
Kama kwali ameuawa kwa sababu za kisiasa basi HALI MBAYA TANGANYIKA.

RIP malafyale Mwankenja
 
Ya Kolimba yalikuwa mauaji? Watendeeni haki waliofariki. Vinginevyo hata akina Chacha Wangwe, Mwalimu, yoote tutaita ni mauaji.
Wewe unaishi tanzania ipi unajua chanzo chake kifo cha Kolimba siyo ajali wala cha kawaida(natural death) yale ni mauaji tena ya mchana kweupe.
 
Ndugu zangu kwa kuingiza siasa katika mambo ya uhalifu hamuisadii jamii yenu kwani kwa kufanya hivyo mnafanya wachunguzi wa tukio waelekeze nguvu zao sehemu nyingine mbali na wale waliohusika na uhalifu; hiyo inaweza kuwa ni njama ya wahalifu to divert attention from the real culprits ili wasikamatwe!
 
Kuna maswali ya msingi kuna nini katika Halmashauri?Isije ikawa kaponzwa na misimamo yake kuhusiana na mambo fulani na mara nyingi ni mijifedha au miradi yenye utata!mimi sisemi konspirasi hapa lakini nataka kusema inakuaje hasa mtu anapigwa risasi nyumbani kwake.ni kuuawa tu sawa.kwanini?nakumbuka muda fulani aliwekewa ulinzi. Naanza hivi hii halmashauri ina kipato gani?inategemea nini.kulikuwa na kitu gan i mezani kwa mheshimiwa huyu?
haya yangu manenolakini
 
adui yako mpende, usilipe kisasi kwa kisasi. Mungu aifariji familia ya marehemu.amen!!!!!!!
 

Ni kwanini aliwekewa ulinzi wakati huo, Unaweza kutuambia kaka?
nadhani polisi wa anzie hapo!
 
poleni wafiwa na wanarungwe kwa ujumla. mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina.

POLENI SANA NDUGUZETU WA RUNGWE!!! Lkn mauaji ya namna hii si ya kufmbia macho!!!! Hali inatukumbusha yaliyotokea kwa Jaji Mwaikasu!!!!

USALAMA WA RAIA NI MAMLAKA YA NANI!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…