- Source #1
- View Source #1
Taarifa kutoka ukurasa wa Instagram wa Habari 24 zimechapisha habari yenye ujumbe kwamba John Mrema, ambaye ni kada wa chama cha CHAUMA, ameomba kurejea CHADEMA.
Katika chapisho hilo, ujumbe ufuatao umeonekana: “Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zinaeleza kuwa aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje pamoja na Mkurugenzi wa Uenezi wa CHADEMA, na baadaye kuhamia CHAUMA, John Mrema, anapanga kurejea CHADEMA.”
je uhalisia wa dai hilo upo vipi?

- Tunachokijua
- John Mrema ni mwanasiasa na mwanachama wa Chama Cha Ukombozi wa Umma akiwa na nafasi ya Mkurugenzi wa mawasiliano. John Mrema pia amewahi kuwa mwanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Madai
Kupitia mitandao ya kijamii chanzo kimoja kijulikanacho kama Habari 24, kilichapisha taarifa ikiambatana na grafiki inayosomeka "Mrema aomba kurudi CHADEMA"
Uhalisia wa Taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli. Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa taarifa hiyo haikuchapishwa na vyanzo vingine vyenye kuaminika.
John Mrema pia kupitia ukurasa wake rasmi wa X amekanusha taarifa hizo kwa kueleza hana mpango huo na ana furaha kwenye chama alicho sasa (CHAUMMA).
Mrema aliandika
"Wapuuzeni wanaosambaza uvumi huu, hakuna nilichoacha CHADEMA,nilipo nina faraja na matumaini ya kusonga mbele .Kama kwa kuzusha kunawapa faraja basi waendelee na huo uzushi wao . Mimi ni CHAUMA na niko imara sana"