John Mnyika: Taarifa kuhusu Uongo wa waziri Muhongo

John Mnyika: Taarifa kuhusu Uongo wa waziri Muhongo

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ametoa kauli za uongo kwa nyakati mbalimbali mwaka 2012 na 2013 ndani na nje ya Bunge kuhusu utafiti na uendelezaji wa gesi asilia.

1)Waziri Muhongo alijibu uongo kwamba hafanyi kazi kwa vyombo vya habari.

Waziri Muhongo alijibu uongo kwamba hafanyi kazi kwa vyombo vya habari nilipohoji kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge ya kuanzia Novemba 2011 ya kushughulikia ufisadi uliothibitika katika mapato ya mauzo ya gesi na udhaifu mwingine uliobanishwa.

2) Kamati ya TPDC kupitia mikataba mibovu na ripoti kutumika kuendelea mbele.

Aidha, Waziri Muhongo aliahidi uongo alipounda alipounda kamati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) na kuahidi

kwamba kamati hiyo itafanya mapitio ya mikataba na kuandaa ripoti itakayowezesha mikataba mibovu ya utafiti wa mafuta na gesi asili kufanyiwa marekebisho. Hata hivyo, Wizara ya Nishati na Madini baadaye iliyoa taarifa kwamba matokeo ya ripoti hiyo hayatatumika kwa ajili ya mikataba iliyopita bali mikataba ijayo.
Pia, Waziri Muhongo aliahidi kwamba kungekuwa na uwazi kuhusu ripoti hiyo; hata hivyo mara baada ya kamati kumkabidhi ripoti ameamua kuifanya kuwa sini hata baada ya kuomba kupewa nakala ya ripoti hiyo kwa mujibu wa masharti ya sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge.

3)
kuhusu zabuni ya nne ya kunadi vitalu vya utafiti wa gesi asilia
Katika kauli itayofuata nitaeleza uongo wa Waziri Muhongo kuhusu zabuni ya nne ya kunadi vitalu vya utafiti wa gesi asilia ambao ameueleza kwa nyakati mbalimbali bungeni, katika Kongamano juu ya Rasilimali lililoandaliwa na UDASA katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na kupitia taarifa kwa umma ilivyotolewa kwenye vyombo vya habari tarehe 30 Disemba 2013.

Mwaka huu wa 2014 nitatoa kwa umma maelezo ya uongo wa Waziri Muhongo mfululizo kuanzia sasa mpaka atakapoomba radhi kwa umma na kuchukua hatua zinazostahili kuhakikisha maslahi ya nchi na matakwa ya wananchi yanazingatiwa kuhusu utafiti na uendelezaji wa gesi asilia.

lmetolewa na:
John Mnyika (Mb)
6/1/2014
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

Source: John Mnyika: Kauli kuhusu uongo wa Waziri Prof. Muhongo - wavuti.com

Mnyika endelea kujenga hadhi uliyonayokwawanchi jimboni kwako, usitumike vibaya, Muhongo ni makini alichosema sikauli za kisiasa ni za kitaalamu, majungu acha, jamii wanajua wewe ni mwanasiasa, Muhongo anajua anachofanya, mwache afanyekazi jamani!!"
 
Hivi mnyika hana mshipa wa aibu haya mambo ya kutunga atatunga mpaka lini wamemtungia uongo zitto hawajatosheka wanaendelea kudandia wengine.
 
Prof. Muhongo ni mababaishaji na mzigo mkubwa kwa Watanzania. Tangu aingie Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ni janga la kitaifa. Ukiangalia sekta zote mbili(Nishati na Madini) uwekezaji umekwama, hali ya umeme ni tete, uwekezaji katika utafutaji wa mafuta na gesi nao umekwama (ni wale tuu wa zamani ndiyo bado wanaendelea) uwekezaji katika nishati mbadala umekwama. Hakuna sera ya kuendeleza nishati ya joto ardhi, Uendelezaji wa makaa ya mawe umekwama. Morale ya wafanyakazi iko chini kuliko wakati wote.

Watu wasitafute majibu ya haraka haraka, tuangalie hali halisi katika sekta husika. Prof. Muhongo ni tatizo kubwa katika kuinua uchumi wetu.
 
mnyika ametumwa na mengi huyu si bure mengi anajifanya kada wa ccm huku anaishabikia chadema kisirisiri. wachaga ni matapeli sana
Umeonesha udhaifu wako hatujadili kabila la mtu bali tabia yake naona unatumia sera za ccm(udini)
 
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ametoa kauli za uongo kwa nyakati mbalimbali mwaka 2012 na 2013 ndani na nje ya Bunge kuhusu utafiti na uendelezaji wa gesi asilia.

1)Waziri Muhongo alijibu uongo kwamba hafanyi kazi kwa vyombo vya habari.

Waziri Muhongo alijibu uongo kwamba hafanyi kazi kwa vyombo vya habari nilipohoji kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge ya kuanzia Novemba 2011 ya kushughulikia ufisadi uliothibitika katika mapato ya mauzo ya gesi na udhaifu mwingine uliobanishwa.

2) Kamati ya TPDC kupitia mikataba mibovu na ripoti kutumika kuendelea mbele.

Aidha, Waziri Muhongo aliahidi uongo alipounda alipounda kamati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) na kuahidi

kwamba kamati hiyo itafanya mapitio ya mikataba na kuandaa ripoti itakayowezesha mikataba mibovu ya utafiti wa mafuta na gesi asili kufanyiwa marekebisho. Hata hivyo, Wizara ya Nishati na Madini baadaye iliyoa taarifa kwamba matokeo ya ripoti hiyo hayatatumika kwa ajili ya mikataba iliyopita bali mikataba ijayo.
Pia, Waziri Muhongo aliahidi kwamba kungekuwa na uwazi kuhusu ripoti hiyo; hata hivyo mara baada ya kamati kumkabidhi ripoti ameamua kuifanya kuwa sini hata baada ya kuomba kupewa nakala ya ripoti hiyo kwa mujibu wa masharti ya sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge.

3)
kuhusu zabuni ya nne ya kunadi vitalu vya utafiti wa gesi asilia
Katika kauli itayofuata nitaeleza uongo wa Waziri Muhongo kuhusu zabuni ya nne ya kunadi vitalu vya utafiti wa gesi asilia ambao ameueleza kwa nyakati mbalimbali bungeni, katika Kongamano juu ya Rasilimali lililoandaliwa na UDASA katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na kupitia taarifa kwa umma ilivyotolewa kwenye vyombo vya habari tarehe 30 Disemba 2013.

Mwaka huu wa 2014 nitatoa kwa umma maelezo ya uongo wa Waziri Muhongo mfululizo kuanzia sasa mpaka atakapoomba radhi kwa umma na kuchukua hatua zinazostahili kuhakikisha maslahi ya nchi na matakwa ya wananchi yanazingatiwa kuhusu utafiti na uendelezaji wa gesi asilia.

lmetolewa na:
John Mnyika (Mb)
6/1/2014
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

Source: John Mnyika: Kauli kuhusu uongo wa Waziri Prof. Muhongo - wavuti.com

Bwana Mnyika labda kama unahoja nyingine........lakini Pamoja na tuhuma zako kwa Prof. mara nyingi wananchi tuliamini maneno yenu sababu mnaongea sana, ila siku zile kwenye Kongaano la UDASA.....hoja zako na baadhi ya wenzako zilikuwa hafifu na zisizo na takwimu, Kwa kifupi mlitia aibu na siasa zenu za mipasho zilizo jaa personal attack (majitaka) badala ya hoja. Eti utatowa ''tuhuma mfululizo hadi waziri aombe msamaha'' unaendeleza majitaka badala ya hoja............wewe ni waziri Kivuli wa nishati na ni mbunge, kama ni vikao vya kamati na taarifa za umilikaji na gharama za uchimbaji wa gesi unazijuwa......badala ya kuja na data wewe ni propaganda za uzushi, sio kwamba sisi wananchi tusio bungeni hatuuwi haya mambo. Hili ndio tatizo la siasa za ukanjajanja!
 
mnyika ametumwa na mengi huyu si bure mengi anajifanya kada wa ccm huku anaishabikia chadema kisirisiri. wachaga ni matapeli sana

Jadili HOJA sio kabila la mtoa hoja.
Kwanza John Mnyika sio mchaga.
Je! Muhongo sio muongo? Hakuwadanganya Watz kuwa umeme utashuka bei na badala yake umepanda mara dufu?

Issue hii ya kupanda kwa umeme ni janga ambalo ccm hawatapona 2015.

Mnapewa hoja ya maana mnakuja na kejeli za kitoto kama vile hamuathiriwi na hujuma zinazofanywa na hawa Mawaziri MIZIGO.
 
Hata kwa haya yenye maslahi mapana kwa wananchi wa Tanzania bado mnaleta propaganda za Lumumba!?... Nani kawaloga?
 
Kuna ukweli katika taarifa hii haswa hiyo ya mikataba inayopitiwa na TPDC...kuna kasoro nyingi sana ambazo Wizara ya Nishati imezifanya na bahati mbaya zimejumuishwa kwenye mikataba.

Hii nchi yetu inaingizwa kwenye lindi la umasikini kwa kuwa kuna watu wachache wasioweza kutumia vizuri madaraka waliyokabidhiwa.
 
JM kwa suala la gesi nakushauri ukae kimya na utaonekana unachemka, ila nitakuunga mkono kwa suala kupanda kwa gharama za umeme na matatizo ya maji Ubungo na kama si Dar yote, tena nitakusaidia na kukuunga mkono kwa 100% Prof.Maghembe ni Mzigo that is all, heri ya Muhongo kuliko Ngereja au Karamagi,Msabaha na Kikwete mwenyewe
 
Kuna ukweli katika taarifa hii haswa hiyo ya mikataba inayopitiwa na TPDC...kuna kasoro nyingi sana ambazo Wizara ya Nishati imezifanya na bahati mbaya zimejumuishwa kwenye mikataba.

Hii nchi yetu inaingizwa kwenye lindi la umasikini kwa kuwa kuna watu wachache wasioweza kutumia vizuri madaraka waliyokabidhiwa.

Tatizo mafumbo ni mengi sana, kwa nini usifunguke vizuri ili tujue hizo kasoro?
 
Hata kwa haya yenye maslahi mapana kwa wananchi wa Tanzania bado mnaleta propaganda za Lumumba!?... Nani kawaloga?
Fanya utafiti wako uone, kwa kawaida Mnyika akiweka bandiko humu, kila mmoja anasapoti na hao Lumumba huwa hawatii mguu katika uzi wa namna hiyo. Je leo kimetokea nini?
 
Nyie endelezeni dhana ya ukabila kila siku ili kuthibibitisha wosia wa Baba wa Taifa.
Badala ya kutafuta hoja za msingi kuipinginga haja ya Mnyika; jibu rahisi ni UKABILA! Mkereketwa; duanzi@puruma
 
Last edited by a moderator:
haya ndio tunayotaka kusikia sio habari ya zitto hongera mnyika wewe ni kijana mzalendo
 
mnyika ametumwa na mengi huyu si bure mengi anajifanya kada wa ccm huku anaishabikia chadema kisirisiri. wachaga ni matapeli sana

WAUNGWANA na kwa heshima kuu naomba niulize 'Mengi ameingiaje katika hoja hii ya Mnyika?"
Mnyika ametumia maneno makali kabisa kuwa atauanika UONGO wa Waziri,kwa nini tusisubiri tuone ushahidi wake kwanza kabla ta kuanza kuivuruga habari kamili?
Tunaliharibu jukwaa sana,habari kama hii tumchagize Mnyika aweke ushahidi na pia tukumbuke kuwa bila opposition mambo mengi yangekuwa siri na tusingeyajua.
Pamoja na udhaifu wote ni lazima tuipe oppsition support kwa mustakabali mwema wa Taifa.
Mmesikia kwenye Halmashauri kuna mchwa,dawa ya mchwa ni kuingiza opposoition kwenye halmashauri ili angalau mchwa kama ni kula wale usiku tu na mchana waogope kinyume na ilivyo sasa.
 
Nilikuwepo kwenye Kongamano hilo UDSM. Muhongo alimgaragaza Mzee Mengi mpaka nikamuonea huruma. Baada ya kugaragazwa na kongamano likiwa limeisha na wakati huo Muhongo keshaondoka ukumbini pale Nkrumah hall, Mzee Mengi akaitisha tena kajikongamano kinyemela bila Muhongo kuwepo, MIONGONI MWA WALIOKUWEPO KWENYE HIGH TABLE YA KAJIKONGAMANO HAKO ALIKUWEPO TUNDU LISSU NA MNYIKA PAMOJA NA MZEE MENGI.

NI DHAHIRI MNYIKA ANATUMIKA KATIKA ISHU HII, ITAKUWA NI KOSA KWA MZEE MENGI KULIGEUZA HILI KUWA AJENDA YA KISIASA NA VIONGOZI WA CHADEMA KUKUBALI KUTUMIKA KATIKA HILI. NI BORA CHADEMA WAKAJA NA SERA YAO, KULIKO KIONGOZI MMOJA MMOJA KAMA MNYIKA KUTUMIKA NA MZEE MENGI
 
mengi !! anamezea mate gesi anafanya kila namna ili amiliki gesi kwa mgongo wa uzawa,huku migodi kama tanzanite africa!! ikimshinda kuiendesha,
wanasiasa msitumike vibaye ..

Acha ulimbukeni kwa hiyo mengi ndo chanzo cha umeme kupanda bei, mgao wa umeme unaoendelea kimya kimya na propaganda za kudanganya watu umeme unasambazwa vijijini wakati hiyo 12% ya Tz wanaotumia umeme ni wa mashakamashaka na wa mgao
 
Nilikuwepo kwenye Kongamano hilo UDSM. Muhongo alimgaragaza Mzee Mengi mpaka nikamuonea huruma. Baada ya kugaragazwa na kongamano likiwa limeisha na wakati huo Muhongo keshaondoka ukumbini pale Nkrumah hall, Mzee Mengi akaitisha tena kajikongamano kinyemela bila Muhongo kuwepo, MIONGONI MWA WALIOKUWEPO KWENYE HIGH TABLE YA KAJIKONGAMANO HAKO ALIKUWEPO TUNDU LISSU NA MNYIKA PAMOJA NA MZEE MENGI.

NI DHAHIRI MNYIKA ANATUMIKA KATIKA ISHU HII, ITAKUWA NI KOSA KWA MZEE MENGI KULIGEUZA HILI KUWA AJENDA YA KISIASA NA VIONGOZI WA CHADEMA KUKUBALI KUTUMIKA KATIKA HILI. NI BORA CHADEMA WAKAJA NA SERA YAO, KULIKO KIONGOZI MMOJA MMOJA KAMA MNYIKA KUTUMIKA NA MZEE MENGI

Mbona ukweli ukiongelewa mnakuja na majibu mepesi ya kumtetea muhongo, kweli ni muongo mpaka sasa kuna mgao wa umeme na alisema utakuwa historia,na mambo mengi tu au mnasubiri mpaka kamati ya bunge iundwe kuchunguza ndio mje kusema wizara na waziri wote wabovu acheni kutumika mnakuwa wepesi kusema mnyika anatumika wakati nyie ndio mnatumika mnakataa ukweli wakati kila kitu kiko wazi. Kutoa takwimu zilizokuwa za uongo hakumfanyi mtu kuonekana mjanja. Waziri wa serikali anadanganya alafu mnasema yuko sawa
 
Back
Top Bottom