John Mnyika: Taarifa kuhusu Uongo wa waziri Muhongo

Geeky

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2013
Posts
307
Reaction score
181

SSSS.jpg

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ametoa kauli za uongo kwa nyakati mbalimbali mwaka 2012 na 2013 ndani na nje ya Bunge kuhusu utafiti na uendelezaji wa gesi asilia.

1)Waziri
Muhongo alijibu uongo kwamba hafanyi kazi kwa vyombo vya habari.

Waziri Muhongo alijibu uongo kwamba hafanyi kazi kwa vyombo vya habari nilipohoji kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge ya kuanzia Novemba 2011 ya kushughulikia ufisadi uliothibitika katika mapato ya mauzo ya gesi na udhaifu mwingine uliobanishwa.

2) Kamati ya TPDC kupitia mikataba mibovu na ripoti kutumika kuendelea mbele.

Aidha, Waziri Muhongo aliahidi uongo alipounda alipounda kamati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) na kuahidi

kwamba kamati hiyo itafanya mapitio ya mikataba na kuandaa ripoti itakayowezesha mikataba mibovu ya utafiti wa mafuta na gesi asili kufanyiwa marekebisho. Hata hivyo, Wizara ya Nishati na Madini baadaye iliyoa taarifa kwamba matokeo ya ripoti hiyo hayatatumika kwa ajili ya mikataba iliyopita bali mikataba ijayo.
Pia, Waziri Muhongo aliahidi kwamba kungekuwa na uwazi kuhusu ripoti hiyo; hata hivyo mara baada ya kamati kumkabidhi ripoti ameamua kuifanya kuwa sini hata baada ya kuomba kupewa nakala ya ripoti hiyo kwa mujibu wa masharti ya sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge.

3)
kuhusu zabuni ya nne ya kunadi vitalu vya utafiti wa gesi asilia
Katika kauli itayofuata nitaeleza uongo wa Waziri Muhongo kuhusu zabuni ya nne ya kunadi vitalu vya utafiti wa gesi asilia ambao ameueleza kwa nyakati mbalimbali bungeni, katika Kongamano juu ya Rasilimali lililoandaliwa na UDASA katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na kupitia taarifa kwa umma ilivyotolewa kwenye vyombo vya habari tarehe 30 Disemba 2013.

Mwaka huu wa 2014 nitatoa kwa umma maelezo ya uongo wa Waziri Muhongo mfululizo kuanzia sasa mpaka atakapoomba radhi kwa umma na kuchukua hatua zinazostahili kuhakikisha maslahi ya nchi na matakwa ya wananchi yanazingatiwa kuhusu utafiti na uendelezaji wa gesi asilia.

lmetolewa na:
John Mnyika (Mb)

6/1/2014
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

Source: John Mnyika: Kauli kuhusu uongo wa Waziri Prof. Muhongo - wavuti.com
 
Taking down the tz oligarchy one tentacle at a time.
 
ametumwa na mengii.. mchaga mwenzake;
huna lolote bora ukae kimya!!
 
Sasa hii tanzania viongozi wake wamekuwa vigeugeu kila kona aaaaah
 
mengi !! anamezea mate gesi anafanya kila namna ili amiliki gesi kwa mgongo wa uzawa,huku migodi kama tanzanite africa!! ikimshinda kuiendesha,
wanasiasa msitumike vibaye ..
 
Muhongo ameweka siri hadharani sasa watu wanaanza kutumika kumpaka matope. Mnyika nenda kashughulikie tatizo la maji ubungo, acha kutumika hovyo.
 
mnyika ametumwa na mengi huyu si bure mengi anajifanya kada wa ccm huku anaishabikia chadema kisirisiri. wachaga ni matapeli sana

mbona anajulikana kitambooooooooo-si ndio maaana matukio ya CDM hupewa airt time ya kutosha ITV hasa katika hili sagga la ZITTO vs MBOWE, SLAA, LISSU na LEMA
 
Mnyika jieleze vizuri ili ueleweke.naona habari yako imejaa porojo tu.inaelekea ni janja ya kubadili upepo wa mgogoro unaovuma ndani ya chadema.siasa si uongo
 
Unatumika kabisa huna jipya

Kweli kabisa, anatumika. Mbona katika mawaziri wote ambao huwa mnagombana nao sijawahi kusikia mmegombana na mawaziri Wachagga au wenzetu ni malaika? Sijawahi kusikia, kuona katika Tv, redio na magazeti yenu mkiwashambulia Wachagga. Hii imekaaje? Ukabila mtupu kama wa CHADEMA!!!!
 
Mengi mchagga, Mnyika nae mchagga? Wajukuu zetu wakipigiwa hadithi jinsi tulivyoibiwa mchana kweupe na watu wachache mwanzo wa karne hii na watatushangaa sana, mfano mikataba 17 tulioisaini na china na mikataba mingine ambayo ni siri waziri huyu mzalendo haijui?
 
Mambo hayo nilitarajia yangetamkwa nawe hadharani ndani ya mjengo kwani ninafahamu kama ni kweli basi amelidanganya bunge tukufu na hilo ni kosa kubwa kwa serikali kusema uongo mjengoni kama vile mbunge akisema uongo.
Anzia kule bwana!!!
 
1.Jamani Muhongo ni Muongo acheni uongo muongo anaongopa sana.

2.Wanaojadili ukabila Mwalimu alituambia ni wendawazimu hvyo tusiwajadili wendawazimu
Muhongo tatizo lake jina linafanya kazi atatuongopea mpaka tukome kumfahamu ila tusimlaumu jina tatizo
 
Kweli kabisa, anatumika. Mbona katika mawaziri wote ambao huwa mnagombana nao sijawahi kusikia mmegombana na mawaziri Wachagga au wenzetu ni malaika? Sijawahi kusikia, kuona katika Tv, redio na magazeti yenu mkiwashambulia Wachagga. Hii imekaaje? Ukabila mtupu kama wa CHADEMA!!!!

Wewe ndiye bure kabisa.

Mramba sio mchaga? Nani alipiga kelele mpaka akapigwa chini na kufunguliwa mashtaka?

Cyril Chami sio Mchaga? Nani alimbebea bango mpaka akaachia ngazi kwenye uwaziri?

Acha kufikiri kwa kutumia ma------!!!!!

Tiba
 
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ametoa kauli za uongo kwa nyakati mbalimbali mwaka 2012 na 2013 ndani na nje ya Bunge kuhusu utafiti na uendelezaji wa gesi asilia.

1)Waziri Muhongo alijibu uongo kwamba hafanyi kazi kwa vyombo vya habari.

Waziri Muhongo alijibu uongo kwamba hafanyi kazi kwa vyombo vya habari nilipohoji kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge ya kuanzia Novemba 2011 ya kushughulikia ufisadi uliothibitika katika mapato ya mauzo ya gesi na udhaifu mwingine uliobanishwa.

2) Kamati ya TPDC kupitia mikataba mibovu na ripoti kutumika kuendelea mbele.

Aidha, Waziri Muhongo aliahidi uongo alipounda alipounda kamati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) na kuahidi

kwamba kamati hiyo itafanya mapitio ya mikataba na kuandaa ripoti itakayowezesha mikataba mibovu ya utafiti wa mafuta na gesi asili kufanyiwa marekebisho. Hata hivyo, Wizara ya Nishati na Madini baadaye iliyoa taarifa kwamba matokeo ya ripoti hiyo hayatatumika kwa ajili ya mikataba iliyopita bali mikataba ijayo.
Pia, Waziri Muhongo aliahidi kwamba kungekuwa na uwazi kuhusu ripoti hiyo; hata hivyo mara baada ya kamati kumkabidhi ripoti ameamua kuifanya kuwa sini hata baada ya kuomba kupewa nakala ya ripoti hiyo kwa mujibu wa masharti ya sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge.

3)
kuhusu zabuni ya nne ya kunadi vitalu vya utafiti wa gesi asilia
Katika kauli itayofuata nitaeleza uongo wa Waziri Muhongo kuhusu zabuni ya nne ya kunadi vitalu vya utafiti wa gesi asilia ambao ameueleza kwa nyakati mbalimbali bungeni, katika Kongamano juu ya Rasilimali lililoandaliwa na UDASA katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na kupitia taarifa kwa umma ilivyotolewa kwenye vyombo vya habari tarehe 30 Disemba 2013.

Mwaka huu wa 2014 nitatoa kwa umma maelezo ya uongo wa Waziri Muhongo mfululizo kuanzia sasa mpaka atakapoomba radhi kwa umma na kuchukua hatua zinazostahili kuhakikisha maslahi ya nchi na matakwa ya wananchi yanazingatiwa kuhusu utafiti na uendelezaji wa gesi asilia.

lmetolewa na:
John Mnyika (Mb)
6/1/2014
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

Source: John Mnyika: Kauli kuhusu uongo wa Waziri Prof. Muhongo - wavuti.com

Mengi at work! Yale yale ya Zitto.
 
Mnyika pole sana, kutumika kubaya, umejisahau kuwa huo uongo ndio anauhubiri huyo mtu wako siku zote, ulichobadili ni kuupa sura ya bungeni.

Pili, wabunge hamuaminiki tena kwani mmetumika mara nyingi na wenye maslahi yao binafsi, mlimtetea Mhando hadi kulazimisha kuitwa kwa Waziri Muhongo mbele ya Kamati ya Uongozi, Spika Makinda akaona mbali ataumbuka akapiga chini, aliwasaidia sana kwani naye angeumbuka baada ya madudu ya Mhando kuibuliwa na Raia Mwema.

Mmetumika kwenye Oparesheni tokomeza ikaonekana haifai, nyuma ya pazia tunaelewa wapo majangili, mbona hatuwasikii mkiwajibishana kuhusu mauaji ya wakulima wasio na hatia yanayofanywa na wafugaji.

Kijana, unajimaliza, Watanzania sasa tuyaelewa mengi ukiwemo uchafu wenu. Huyo mzee mnayempigania, iweje siku zote anaonewa yeye tuuuuuuuu!
 
Back
Top Bottom