John Mnyika: Nimemtembelea Lissu asubuhi, yuko salama, ana amani na anatuasa tusikae kimya

Kama huelewi hata hili, hutaelewa chochote duniani hapa. Nikutoe hofu, wala usihangaike kuwaza kwa kuwa hata Mnyinka na Tundulisu, hawakulenga ujumbe huu kwako. Unajua JF kuna jumbe nyingi na kila ujumbe unalenga wadau halisi.

Watu wasiona ufahamu wa kiasi hiki, hapa si mahala pako. Wewe subiri mkondo wa maji ukupeleke kokote kule maji yatakapoelekea. Nikutakie chakula chema.
Yaaan tupige mikelele tu barabarani au vp?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemtembelea Lissu asubuhi yuko salama na ana amani. Ujumbe wake mkuu kwetu ni TUSINYAMAZE!!!
Mbunge WA Jimbo LA Kibamba John Mnyika

Nadhani sitokuwa na la kuwashauri tena Marafiki zangu wa Kisiasa akina CHADEMA kwani personally nimeshajaribu kuwaasa / kuwashauri jinsi ya kufanya Siasa zenu vizuri hasa nyakati hii ya Tano ( 5 ) tuliyonayo sasa ili muweze kuyaepuka hayo mnayokumbana nayo na hata huyo Lissu ( Mtani wangu wa Kinyiramba ) nimewashawahi kumtahadharisha sehemu mbalimbali katika maandiko yangu ila kama kawaida Yenu Watu wa CHADEMA mkipewa ushauri mzuri tu na sisi Marafiki zenu wa CCM mnadhani tunawasanifu.

Nauona mwisho mbaya sana wa Kisiasa na Uanaharakati wa Mheshimiwa Tundu Lissu. Lissu siku zote amekuwa akiwashinda hao waliomkamata na mara nyingi sana amekuwa akijigamba kuwa hawamuwezi kwani anajua Kona zote za Kisheria lakini hapo hapo akasahau kwamba siku zote anayekukimbiza halafu anakukosa huwa anajiuliza mara mbili mbili ni kwanini anakukosa au ni wapi anakosea na pindi akishakujulia basi mwisho wake huwa ni mbaya sana Kwako Wewe mkimbizwaji na kutimiza ila kauli ya Mwingereza isemayo " The One who laugh later laughs better ".
 
Yaaan tupige mikelele tu barabarani au vp?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna tofauti kati ya "Shouting" na "Talking"
Hiyo unayosema wewe bila shaka ni "Shouting" au kule Elimu ya Upili mwalimu akiingia darasani alikuwa anasema "Murmiling"...Unaongeeeaaaa tu na kupiga mikelele with no legal basis

Lissu anataka watu "Waongeee",msingi wa kuongea ni kujadili,kufikiri,kuhoji,kukosoa na hata kupinga.Huu ni uhuru wa asili,ambao hata shetani amepewa na Mungu,ndio maana alipata uhuru hata wa kuongea na Yesu na kumpa majaribu ya kujitupa mnarani ili ampe milki ya dunia,abadili jiwe kuwa mkate.Sio kwamba mwenye himaya yake Mungu hakuwepo,bali alitaka kutoa tu ule mnaita "Natural Freedom"

Lissu hajasema mpayuke,amesema muongee...Ongeeni!!Kama vile wewe unavyopata nafasi ya kuongea hapa kwa njia ya maandishi na ID fake,wakati Lissu anaongea kwa maandishi na kwa mdomo kwa ID halisi
 
Nimemtembelea Lissu asubuhi yuko salama na ana amani. Ujumbe wake mkuu kwetu ni TUSINYAMAZE!!!
Mbunge WA Jimbo LA Kibamba John Mnyika
Si yupo sawa, anachotaka tupige kelele kwa lipi?
Ainisheni.
Alisema haogopi, kesho mtasikia kagoma kula. Huyu jamaa msanii kweli.
Ati anajiita nguli, Nguli hujafanikiwa hata mission hata moja, anazani wa tanzania ni wa miyehuko ya wahenga. Muwekeni sero kama miezi 3 hivi .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom