John Mnyika ndani ya Kikao cha Kamati kuu kinachoendelea

John Mnyika ndani ya Kikao cha Kamati kuu kinachoendelea

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716
11811500_10153538021187938_3900723245743735649_n.jpg unnamed.jpg
MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika, ameibuka jijini Dar es Salaam na kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu (CC) ya chama chake. Anaandika Saed Kubenea … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya kikao cha CC kinachofanyika katika hoteli ya Bahari Beach zinasema, Mnyika amehudhuria mkutano huo na kueleza kuwa kutoonekana kwake, kumetokana na matatizo ya familia.

Mnyika ambaye ni naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amekuwa haonekani tangu Edward Lowassa alipojiunga na chama chake, Jumapili iliyopita.

Mbali na Mnyika, katibu mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, hajaonekana katika ofisi za chama hicho, tangu Lowassa ajiunge na Chadema; jambo ambalo limezua taharuki kwamba huenda amejiuzulu wazifa wake.

Dk. Slaa ambaye alishiriki vikao vyote muhimu na majadiliano vilivyomkaribisha Lowassa ndani ya Chadema, anadaiwa kuzuiwa na mkewe, Josephine Mushumbuzi, kushughulika na chama hicho.

Mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amethibitisha Mnyika kuhudhuria mkutano huo.

Amesema, "…Mnyika yupo ndani ya ukumbi wa mkutano. Anashiriki kikao cha kamati kuu. Waliokuwa wanadhani chama chetu kimepata mpasuko kutokana na ujio wa Lowassa, walikuwa wanajidanganya."

Lissu amesema, ndani ya Chadema wako wamoja, yote yaliyotokea yalikuwa mapambano yanayotokana na ukomavu wa kidemokrasia uliyopo.
 
John John Mnyika,leo katika kikao cha Secretarieti ya Kamati Kuu amejitokeza ndani ya ukumbi,huku akionekana mwenye utulivu wa akili na sura alilakiwa na baadhi ya Wazee wa ImageUploadedByJamiiForums1438516324.573781.jpg

Baada ya Kikao hiki,sisi kama wadau na wapenzi wa Chadema tunaomba ndugu JJ Mnyika uweze kuongea na waandishi wa habari kuondoa sintofahamu iliyojengeka kwa wananchi na hasa wafuasi na wapenzi wa Chadema
 
wape vidonge vyao! na watavinywa mwaka huu!
 
Picha ya zamani sana hii mnyilka ameapa kuwa hawezi rejea ukahawani
 
Hii migogoro ni fake lengo ni kumsahaulisha magupombe
 
Ikigundulika sio ya leo Moderator haki itendeke kwa mleta mada.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: 7ve
nafurah kusikia hlo bado babu yangu kipenzi cha watania japo nisikie saut yake tu basi
 
Back
Top Bottom