John Mnyika juu ya hotuba ya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John Mnyika juu ya hotuba ya Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 3, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Aprili Mosi 2011 Rais Jakaya Kikwete alilihutubia taifa na kuzungumzia masuala matatu: shughuli ya kutembelea Wizara na Idara za serikali, taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Katiba Mpya.


  Katika hotuba hiyo Rais Kikwete alizungumzia kuhusu hali ya umeme nchini na gharama za kuunganisha umeme kama sehemu ya mambo aliyoyatolea maelekezo wakati wa ziara yake katika Wizara ya Nishati na Madini.
  Katika hotuba hiyo Rais Kikwete amekiri kwamba serikali yake haina suluhisho lolote la umeme wa dharura kwa ajili ya kupunguza mgawo wa umeme katika kipindi cha sasa mpaka Julai zaidi ya kutegemea kudra ya mvua kuendelea kunyesha.

  Katika hali hiyo Rais alipaswa kuwawajibisha wote waliochelewesha maandalizi ya kukabiliana na dharura ambayo yalijulikana toka mwaka 2008 na Rais Kikwete amekuwa akiyatolea maelezo na maelekezo toka wakati huo bila kusimamia kikamilifu utekelezaji.
  Aidha kauli ya Rais Kikwete kwamba mchakato wa kukodi mitambo ya kufua umeme wa megawati 260 uko kwenye hatua ya zabuni kutangazwa imedhihirisha uzembe kwa upande wa serikali kwa kuwa toka mwezi Februari kauli hiyo hiyo imekuwa ikijirudia hali ambayo inaashiria kwamba mpango huo hautakamilika mwezi Julai mwaka 2011 kama inavyodaiwa.
  Uamuzi wa kukodi mitambo hiyo ulifikiwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri cha tarehe 15 Februari 2011 ambacho Rais Kikwete alikuwa mwenyekiti wake, Rais baada ya kikao hicho alipaswa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa maazimio husika badala ya kusubiri mpaka kutoa maagizo mengine kwenye ziara ya wizarani mwezi Machi mwishoni. Hali hii itapelekea taifa kulipia baadaye mitambo ambayo haitatumika kikamilifu katika kipindi chote cha dharura kama ilivyotokea katika kashfa ya Richmond/Dowans.


  Kadhalika kauli ya Rais Kikwete imedhihirisha kuwa serikali yake imeshikilia msimamo wa kukodi mitambo ambayo itatumika kwa kipindi cha miezi sita pekee kwa gharama za zaidi ya bilioni 400 badala ya kuweka mkazo katika kununua mitambo kama ambavyo imeshauriwa na wadau mbalimbali. Ni muhimu kwa Wizara husika kuueleza umma kiwango cha fedha ambacho kitatumika katika mpango huu ambacho kimsingi kitazidi kuongeza mzigo wa madeni kwa TANESCO.
  Pia, serikali ieleze maandalizi ambayo yamekwishafanyika mpaka hivi sasa kukabiliana na tatizo la upatikanaji, usafirishaji na uhifadhi wa mafuta mazito (HFO) ambayo yatahitajika kwa kiwango kikubwa katika kuendesha mitambo hiyo katika mikoa itakayowekwa mitambo hiyo. Jambo hili ni muhimu kwa kuwa katika mazingira ya sasa serikali inashindwa kukabiliana vya kutosha na mahitaji ya mafuta mazito kwa mitambo ya megawati 100 ya IPTL iliyopo Dar es salaam ambayo hutumia takribani bilioni 15 kwa mwezi kwa mafuta pekee.
  Kwa upande mwingine, naunga mkono kauli ya Rais ya kuwataka TANESCO kuangalia kwa haraka namna ya kupunguza gharama kubwa za kuwaunganishia umeme wateja jambo ambalo nimekuwa nikitoa mwito kwa serikali kulifanya toka mwaka 2010.


  Natambua kwa Rais Kikwete amekubaliana na pendekezo la kuwaunganishia watu umeme na kuingiza gharama hizo katika bili ya umeme kidogo kidogo hata hivyo ni muhimu pendekezo hilo likaambatana pia na utaratibu ambapo wananchi wanapogharamia wenyewe vifaa kama nguzo za umeme basi gharama hizo warejeshewe kupitia punguzo katika malipo ya bili zao kama umeme uliolipiwa kabla kwa kuwa miundombinu hiyo hubaki kuwa mali ya TANESCO.
  Hatahivyo, pamoja na kutoa kauli kwa TANESCO Rais Kikwete alipaswa kuwaeleza watanzania namna serikali yake ilivyojipanga kuipunguzia mzigo wa madeni TANESCO kutokana na madeni ambayo serikali inadaiwa na pia mzigo mkubwa ambao TANESCO inaubeba kutokana na mikataba mibovu ya kifisadi ambayo serikali iliingia.
  Kuwepo kwa gharama kubwa ya kuunganisha umeme na bei ya umeme wenyewe ni matokeo ya mzigo wa madeni na ufisadi katika mikataba kubebeshwa wateja waliopo. Sekta ikiwemo umeme imegubikwa na rushwa na ufisadi mkubwa ukihusisha viongozi wa juu wa Serikali tangu mwaka 1991, wakati wa IPTL ambayo inaendelea kuitafuna nchi hadi leo. Pamoja na kashfa ya Dowans/Richmond mwaka 2006 serikali iliingia mkataba na Alstom Power Rentals kuzalisha umeme wa dharura Mkoani Mwanza na kampuni hiyo kulipwa bilioni takribani 40 bili kuzalisha umeme wowote.


  Hivyo natoa mwito kwa Serikali kupitia upya haraka mikataba ya umeme hapa nchini ambayo imeliingiza taifa katika fedheha na hasara kubwa, ikiwemo mikataba ya IPTL na Songas,Artimas,Tanpower Resources /Kiwira, ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kishera na kinidhamu patakapobainika uzembe au ufisadi wowote kwa wote wanaohusika, kwa mikataba iliyoisha lakini ambayo iliingiza nchi katika hasara kubwa kama sehemu ya mkakati wa kupunguza gharama za umeme nchini Tanzania.
  Nilitarajia pia Rais Kikwete angetumia hotuba hiyo kueleza kwa umma maelekezo ambayo ameyatoa kwa Wizara ya Nishati na Madini kuhusu sekta ndogo ya mafuta hususani yanayohusiana na ubora na bei ya mafuta ikiwemo mkakati wa kupunguza tozo na kodi ili kupunguza gharama ambazo zinaongeza ugumu mkubwa wa wananchi hivi sasa.
  Kwa ujumla, maagizo ambayo Rais Kikwete ameyatoa mengi ni yale yale ambayo amekuwa akiyatoa kwa nyakati mbalimbali kati ya mwaka 2006 mpaka 2010, hivyo wakati umefika sasa kwa Rais kusimamia kikamilifu utekelezaji wa masuala ambayo baraza la mawaziri ambalo yeye ni mwenyekiti wake ndicho chombo cha haraka zaidi kinachopaswa kuongeza ufanisi.
  Mfumo wa utawala unaotumiwa na Rais Kikwete wa kuzunguka (Management By Walking Around-MBWA) hauwezi kuleta tija ya kutosha ikiwa Rais Kikwete hataweka mkazo katika mifumo ya kiutawala inayozingatia malengo na
  matokeo (Management by Objectives and Results).


  John Mnyika (Mb)
  Waziri Kivuli-Nishati na Madini
   
 2. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ni kweli Mnyika hivi mpaka leo bado tuna ndoto za kukodisha mitambo tena? Kinachotushinda ni nini kununua mitambo yetu moja kwa moja? Ni masuala ambayo yanaleta maswali mengi kuliko majibu!
  Ni jambo la ajabu kweli kutumia 400bill kwa ajili ya kukodi mitambo wakati inawezekana mitambo hiyo isifike 400bill. Hii ni njia nyingine tena ya kuwaundia watu ulaji kiulaini kabisa. 400bill ni karibu 3/4 ya mapato ya mwezi mzima ya serikali, kisha matumizi yake yawe ni yenye kutilisha mashaka ni aibu.
  Mimi naona iliyopo ni watu kupinga mambo haya hadharani na rais ajue kuwa watu hawapendi ujinga tena. Kupinga kunaweza kuwa kuandamana au njia yoyote muafaka bora isihusishe umwagaji damu lakini yenye tija.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,904
  Trophy Points: 280
  Kuna shinikizo kubwa sana toka kwa fisadi Rostam kwenda kwa Kikwete kwamba ni lazima mitambo hiyo ikodishwe tena ili watengeneze ulaji na pia walipwe shilingi bilioni 94 pamoja na riba ya kucheleweshwa kwa malipo hayo ambayo yalitakiwa yafanyike January 2011. Haingii akilini kuona kwamba wameng'ang'ana kukodisha mitambo kwa pesa chungu nzima shilingi bilioni 400 bila kuangalia gharama za kununua mitambo mipya ambazo zinaweza kabisa kuwa chini ya shilingi bilioni 400. Hata kama zikifikia bilioni 400 bado ni rahisi mno kununua mitambo mipya kwa bei hiy kuliko kununua mitambo ambayo haijulikani imeshatumika kwa muda gani. Si ajabu ilipoingia Tanzania mwaka 2006 tauari ilikuwa imeshatumika katika nchi nyingine.
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Mnyika usitafute umaarufu kupitia kwa JMK yale maji marefu huyawezi, utazama buree kwa kutafuta sifa.
   
 5. g

  gepema Member

  #5
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kukodi mitambo kwa 400b wakati tutatumia kwa muda mfupi tu ni uchizi,why not implementing bigger projects like stiglers or kiwira? Jk and your govt are total failure!! Phew
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Watu wa Ubungo hawakufanya makosa kumpeleka Mnyika bungeni. Natamani wabunge wengine wa upinzani wangekuwa kama hivi, even if it means they have to be a bit on the cerebral side. I would rather take cerebral Mnyika than airhead Mtema.
   
 7. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  big up, mawaziri kivuli wengine wajibie hoja za jk katika maeneo yao.
   
 8. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hehehe,
  Nimecheka sana, ati jamaa anazunguka zunguka, anabwaka bwaka tu, teheheheeeee
  MBWA nayo!:smile-big:
   
 9. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #9
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  We ndio unatafuta sifa. Mnyika mwenzio mbunge we mropokaji tu, maji marefu yapi!?
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  NGUVU YA UMMA Itumike kupinga ufisadi huo, siku ikifika hiyo mitambo tujulisheni tuwashe moto, tumechoka bana
   
 11. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kati ya hao wawili wa kumzamisha mwenzaka nani?
   
 12. S

  Salimia JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Same goes to you na wengine wanaomwandama JK, mwenzenu Rais, ninyi mnakesha humu mnaropoka!
   
 13. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Tatizo watu mnaweka mapenzi yenu ya vyama badala ya kujadili mambo mazito ya nchi kwa maslahi ya umma,tunahitaji kuweka ushabiki pembeni tujadili hoja siyo kuleta maneno ya mipasho kumtetea JK hata ambapo hastahili kutetewa! Amkeni watanganyika na mchukue hatua!
   
 14. m

  malimamalima Member

  #14
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kula 5...
   
 15. m

  malimamalima Member

  #15
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watanzania bwana...kazi kweli kweli...
   
 16. O

  Old ManIF Senior Member

  #16
  Apr 4, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kungekuwa na nia ya kweli ya kumaliza tatizo hili la umeme hapa TZ lingekuwa limeisha na tumesahau. Tanesco wangekuwa wana mitambo yao mipya na ya kisasa wakizalisha umeme. Lakini kwa vile hili tatizo la umeme kwa mafisadi ni mradi wa kujitengenezea mabilioni ya fedha na kujitajirisha kwa utajiri haramu na wakufuru halitaisha atleast kwa awamu hii ya uongozi ambayo kwayo kukumbatia mafisadi na ufisadi ni moja ya sifa ya kujivunia.
   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #17
  Apr 4, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  What's your point!
   
 18. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #18
  Apr 4, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  majimshindo hana point, pointless. Mnyika mmoja sawa na wabunge 80 wa ccm
   
 19. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #19
  Apr 4, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,039
  Likes Received: 8,532
  Trophy Points: 280
  acha kuropoka kama tahira please ama ushabwia.
  Mnyika could be right though sema michangiaji mingine humu inatia hasira.
  Mmojawapo we pompo KEEP KWAYAT kama huna point
   
 20. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Huna muelekeo wa Maendeleo kila hoja nzuri lazima uipinge na za ujinga unazitetea China ungeshanyongwa. Na Akili zako kama za Joseph Makamba.
   
Loading...