Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Anaandika Wakili Msomi John Malya
Commissioner wa Police nchini Tanzania, aliepata kushika wadhifa wa Inspekta Jenerali wa Polisi kwa kipindi kifupi kuliko watangulizi wake wa hivi karibuni.
Ernest Mangu anaiacha ofisi ya IGP ikiwa ameihudumu kwa miaka 3 na miezi 4 na siku 28. Amekabiliana na changamoto nyingi za kikazi moja wapo ikiwa ni mauaji yanayoendelea mkoa wa pwani huko Kibiti;
Ameacha wadhifa wa IGP akiwa ametoa kauli moja thabiti hivi karibuni '...sio maelekezo ya Jeshi la Polisi kukamata waandishi wa habari wakati wanatimiza majukumu yao...' :
Hiyo ni kuali ya kitetezi ya haki ya kupata na kupasha habari!
Ameacha ofisi akiwa ameanza kuwa mlinzi wa masharti ya Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sababu ya kuachishwa wadhifa anaijua anaeteua na kutengua, na hana wajibu wa kutujuza wananchi wake. Anafanya hivyo kwa hisani na mapenzi yake.
Kiongozi mwingine alieondolewa hivi karibuni akiwa kwenye harakati za kulinda Masharti ya Ibara ya 18 ya Katiba yetu ni Nape Nnauye.