John Heche na kamati za bunge

Tatizo lako ni kumfanya ZZK mungu wako. Kwako wewe ZZK ni super Genius! Hizo tunaziita ni Akili za Kilaza aliyeshindikana. Hauamini nje ya ZZK, ume delegate kichwa chako kwake,tutegemee nini? Una maana gani kuwa hakuna wa kumfikia hata robo ZZK? Kwenye USALITI,UONGO NA UZANDIKI SAWA,HAKUNA WA KUMFIKIA, ila ZZK ni Binadamu mwenye upeo wa Kawaida tu. Kwa mujibu wa Parliamentary Watch, ni Mnyika na Lisu walioongoza kwa Hoja NYINGI ZENYE MANUFAA KWA TAIFA. Hawa ndio waliotisha Bungeni kwa michango yao na kuitendea wema nafasi yao bungeni. Kingine, Zzk na nyie wafuasi wake, msiwanyooshee vidole UKAWA kwa ZZK kuondolewa PAC, hilo analijua tangu siku ile Tulia Ackson alipochaguliwa kuwa Naibu Speaker. Ajiandae kukabiliana nae au kumkimbia.
 
Ritz kwa mara ya kwanza leo umeongea ukweli bila kupendelea, hongera mkuu
 
Hajapanga Ndugai....alikuwa India kwa matibabu na hali yake sasa imeimarika...lakini tujuwe yote ni ya ALLAH.Haitazidi wala kupungua sekunde muda ukifika.
 
Hivi kumbe kunawabunge wengine ni bora zaidi ya wengine na lazima wajioangie wanapotaka wao
 
Heche kachanganyikiwa tu,hao wabunge wa ukawa wapo robo ya bunge ukiwajaza katika kamati mbili tu kamati zingine zitakosa wabunge wa upinzani.
 
Haya ndio matokeo ya kubadili gia angani. Unatoka kwenye gia kubwa ya kukuwezesha kulitawala bunge unaenda kwenye gia ndogo ya kuingia ikulu wakati njia unayopita inakutaka ulitawale bunge kwanza.

Sasa umekosa vyote unabaki kulalamika. Shame on you Ukawa
 
Ndivyo mnavyotaka kuwaaminisha watu kuwa walioteuliwa ni vilaza, thats so Pathetic! Jifunze kwenye game kila mchezaji kuna mahali anapo fit. Unapomweka Rooney golini tegemea mvua ya magoli. The same na unapomweka De Gea Foward, tegemea ukame wa magoli! Unapomweka Mlata Martha kwenye Kamati ya Nishati na Madini na kumfanya M/kiti wa kamati hiyo unakuwa umeitendea Haki Kamati husika? Unapomtupa Zzk kwenye Kamati ya Huduma za jamii,je, si kumpoteza? Lazima tukubali ni vema zile Kamati zitakazoongozwa na Wapinzani wakapendekeza squad yao wenyewe ili kila mchezaji acheze nafasi yake. Kamati zote za Bunge zimepangwa strategically,Bunge hili litashindwa mapema sana katika kuisimamia serikali. Huo ndo ukweli. Kingine, mapovu yamekutoka wewe,ukweli mchungu, ni Ukilaza ku delegate kichwa chako kwa ZZK! Jiamini, unaweza kuwa na akili zaidi ya ZZK!
 

Hivi si hao CHADEMA walikuwa wanajitapa kuwa mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na wabunge 100 wa CCM? Sasa haya malalamiko ya Heche yanatoka wapi?
 
Ukimtoa Jecha ,Lubuva,Ndugai ni mtu anaefuata kwa kumchukia.Kama wanajua magufuli na serikali yake ni watu wasafi,kwanini wanapanga kumlinda hivyo?Lakini kwa vichwa vilivyoingia bungeni wanapoteza muda tu.Nina tabiri katika uongozi wa Ndugai atafanya kila kinachowezekana bunge lisionyeshwe live.Subirini mtaona.....!
 
Hivi zito ni nani kwako labda tuanzie hapo make wewe bila zito haupo.
 
Huu upangaji wa kamati hata vijana wa Lumumba umewachanganya hawataki tu kusema.
 
kaka acha kujitawala kwa dhana. Ivi umeambiwa nani kawapanga hao wabunge kwenye kamati? Cdm hamuwakubali cuf? Maana PAC yupo mbunge wa tanga mjini binafsi namkubali. Mbona mnalia lia. Wewe ulitaka nani awepo pale. Sikubaliani na hizo fikra potofu za kila muda kuwaza -ve
 
Mkuu hayo maneno siyo yangu pitia uzi upya kwa makini ni kauli ya John Heche wa Chadema kaandika hayo kweny ukurasa wake wa Facebook na mitandao mingine.
 
Ndugai. Nimempa 5. The way alivyopanga. Hataki bunge lenye mihemko bali lenye utulivu na uwakilishi mzuri wa hoja zenye kulenga taifa sio masuala ya kijinga ya kuwa kichama
 
Badala ya kuendelea kulalama na kujiaminisha kuwa kazi itakuwa ngumu, wabunge wajipange kwa kufuatilia mambo, kutafiti na kutumia uwakilishi wao kusimamia serikalimndani ya Bunge. Kamati ni ngazi kuelekea kwenye forum halisi * Bunge* Waache hofu wajipange kuleta matokeo yanayotazamiwa.
 
Spika ana mamlaka ya kupanga vile anavyoona inafaa bila kuwashirikisha akina heche. Wao watulie. Rais wetu mpendwa yupo kizalendo zaidi na sio kichama. Kama wana mambo ya ku raise ya kitafaifa yatafanyiwa kazi ila wawasilishe kwa heshima na si mihemko ya kijinga jinga ya kutaka sifa za kimakundi. Watanzania tunataka maendeleo na sio vyama vyao. Kama anauchungu huyo heche aanze kuikataa posho kubwa anayochukua. Ivi haona kama anatunyonya sie wananchi walalahoi? Kana akina heche wote nchini wapo kitaifa na si matumbo yao basi walitangazie taifa kuachana na posho na STNG allowance
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…