Kama kuna mtu ndani ya CHADEMA mwenye uwezo wa kuwa Rais na kuleta mabadiliko ya kweli, basi ni John Heche.
Anaongea mambo ya msingi sana hoja zake ni za kisiasa, zenye uzito, na zinawagusa wananchi moja kwa moja. Lakini changamoto yake kubwa ni kuwa yupo pahala pasipo, yaani mazingira aliyonayo sasa yanamzuia kung'ara ipasavyo.
Kutokana na hilo, mara nyingine analazimika kuzungumza kwa kufuata upepo wa kisiasa, badala ya kusimamia ukweli wake. Hata hivyo, akipata nafasi ya kutulia na kuongea kwa uhuru, anaibomoa CCM kwa hoja nzito kabisa.
Kwa upande mwingine, kama kuna mtu ambaye ameathiri maisha ya watu wengi kwa namna mbaya kisiasa, basi ni Tundu Lissu. Amevunja matumaini ya watu wengi waliomwamini. Kwa hiyo, kama siasa ni safari ya matumaini, basi kwa wengi bora wahame njia hiyo.
John Heche, jiunge na Zitto Kabwe. Kuna kitu ndani yangu kinaniambia nyie wawili mkishikamana, mnaweza kushinda uchaguzi.