figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 26,660
- 59,082
Makamu mwenyeki CHADEMA Bara Heche, ataongea na Wanahabari leo.
Pia ataelezeza kinagaubaga kilichotokea na kinachoendea na kitakachoendelea.
Nitakuwepo mbele kabisa.
View: https://www.youtube.com/watch?v=R7XKhHM8iJg
Makamu Mwenyekiti, CHADEMA, JOHN HECHE
John Heche ameeleza kuwa hawatokubali kesi ya Tundu Lissu iendeshwe gizani. Amesema hata Mandela alipohukumiwa wafuasi wake waliruhusiwa kwenda.
Amesisistiza hawatoacha kwenda mahakamani hata kama watawaua wote, na watakwenda kwa amani ili kufuatilia kesi ya Mwenyekiti wao, Tundu Lissu.
Amesema kuwa polisi walipowakamata walianza kuzungushwa na gari la polisi maeneo mbalimbali ikiwemo Ununio baadaye wakapelekwa Mbweni kisha wakahamishwa kutoka kwenye gari ya polisi wakapandishwa kwenye gari binafsi.
Heche amesema matukio wanayofanyiwa hayawakatishi tamaa na amewataka wana Chadema kuendelea na mapambano bila kukata tamaa.
Naibu katibu mkuu CHADEMA bara Amnani Golugwa
"Jumla ya majeruhi mpaka jana usiku tuliwapeleka hospitali na wakapata matibabu walikuwa ni majeruhi 21 na nitawataja majina yao na hali zao, walipigwa na kutupwa Mabwepande porini msituni, ndio msitu ambao baadhi ya watu ambao tunawafahamu waliuawa na wakatupwa katika msitu huo akiwemo aliyekuwa mjumbe wa sekretarieti yetu marehemu Ali Kibao aliuawa na akatupwa maeneo yaleyale, watu hawa waliokamatwa walitekwa na jeshi la polisi wakaingizwa kwenye magari, wakatupwa maeneo yalele mambo haya yamefanywa na Jeshi la polisi"
"Waliokatwa ni makamu mwenyekiti wa chama chetu Zanzibar Said Mzee yeye alikamatwa kwenye gari akapigwa, hawa polisi walikuwa wanapiga marungu kwenye migongo, walikua wanageuzwa hivi halafu kwenye katikati ya uti wa mgongo marungu yanapigwa, ilikuwa ni kitendo cha unyama uliopitiliza. Said mzee alipigwa mwili mzima. Ali Juma Naibu katibu mkuu wa chama chetu nae alipigwa marungu kwenye uti wa mgongo, amevunjwa mguu ana POP mguu wa kulia na amevunjwa mkono. Mkurugenzi wetu wa fedha CPA Titto Kitalika yuko katika hali mbaya sana ni moja kati ya watu waliojeruhiwa na leo ameshindwa kuja hapa amevunjwa mguu na mkono, amepigwa mbavu."
"Ngudu Lucas Ngoto, huyu ni mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Serengeti amevunjwa mguu, John Pambalu mkurugenzi wa mafunzo na oganaizesheni naye yupo katika hali mbaya sana ameshindwa kuja hapa leo, amevunjwa mguu na kupigwa marungu kweye uti wa mgongo na kwenye mbavu. Peter Alex yeye alikuwa anapigwa kwenye nyayo."
“Tuna mwanachama wetu ambaye ni mjumbe wa baraza kuu Bi Hilda Newton kama ofisi zetu za chama hatuna taarifa zozote zilizo rasmi zinazoonyesha kwamba hilda Newton yuko wapi.”
Golugwa ameeleza kuwa Hilda alikamatwa eneo la Kisutu na walitegemea kuwa taarifa ya jeshi la Polisi iliyotoka jana pengine ingekuwa na jina la mjumbe huyo
“Jana kwenye taarifa ambayo afande Muliro alitaja majina ya viongozi na wanachama ambao wapo kwenye mikono ya jeshi la Polisi. Na pia alitoa taarifa kuhusiana na mtu mmoja ameokotwa kwenye ufukwe wa Coco Beach taarifa ya Hilda Newton kuwa kwenye mikono ya polisi"
Lucas Ngoto, Mwenyekiti CHADEMA kanda ya Serengeti
"Unyama mkubwa tuliofanyiwa jana na watu ambao wanajiita ni polisi ila mimi kwa imani yangu sidhani kama ni polisi wanaweza kufanya yale matendo, mimi nilifika mahakamani asubuhi nikaomba kuingia kwa ajili ya kusikiliza kesi ya mwenyekiti, lingekuwa neno la ajabu na aibu kwamba mwenyekiti analetwa kwenye kesi, alafu ni haki yetu kuisikiliza alafu nisifike mahakamani, mimi binafsi nilikuwa nimeapa kufika mahakamani. nimefika wakaanza kusema leo hakuna mahakama haifanyi kazi polisi waliokuwa pale, wakati naondoka wakawa wanamshambulia dada Eliza nilipoenda kuwaambia na wenzangu Twaha na Pambalu, mbona mnamshambulia huyu dada na ni mwanamke wakatukamata hapohapo, tulikamatwa watu tisa na hatukuwasumbua, wamezunguka na sisi zaidi ya masaa manne, wakatupeleka huko ambako walienda kutupiga Ununio na tulikuta Difenda mbili ambazo zina askari wanaojiita polisi ambao kazi yao ilikuwa kupiga watu"
"Tulipofika kwenye vichaka wakamshusha dada Pendo wakaanza kumpiga, kuna askari mmoja alikuwa na nyota kama mbili akaanza kumpiga Pendo kama anaua nyoka na wengine wote tukaambiwa shuka kwenye gari vua viatu ficha uso, na kama unaweza kuomba Mungu omba Mungu, jikabidhi kwa Mungu, tukavua viatu tukalala chali tukaanza kupigwa kipigo cha Mbwa koko, kulikuwa na vijana wadogo kama vile hawapigi binadamu, walivyoona tumechoka wakatuacha hapo ununio na askari mkubwa mwenye nyota akawaambia watafutieni maji masafi waoge, wakatupeleka kwenye dimbwi moja lilikuwa na dimbwi moja la maji machafu wakatuambia ogeni humu, tukapelekwa mbweni chumba cha upelelezi na baada ya masaa matatu wakatupeleka Bagamoyo kwenye pori wakatuacha humo"
"Mimi nina maswali ya kujiuliza na naomba watanzania wote tujiulize maswali haya, kwanini pale wanapotesea watu, tulipoenda kupigwa ni eneo la jeshi? Kama hao watu wanaotupiga ni askari wa kawaida wanapata wapi kibali cha kwenda eneo la jeshi na kwenda kupiga watu, kwanini? Swali la pili, sisi tumeenda mahakamani na tumekamatwa na hatuna hata wembe wowote wa kumshambulia askari kwanini wanatukamata hawatupeleki vituo vya polisi wanaenda kutushambulia kwa kutupiga, na ukweli ni kwamba kama tungelijua tunaenda kupigwa na hatupelekwi kituo cha polisi afadhali tungefia pale Kisutu. tulijua tumekamatwa na polisi tunapelekwa mahakamani na kama kuna sheria za Tanzania tumezivunja, basi tunajua tunapelekwa mahakamani lakini matokeo yake tunaenda kupigwa, tumekosa nini?"
Katibu mkuu CHADEMA, John Mnyika
"kuanzia saa tatu asubuhi niliwekwa kizuizini ndani ya gari mpaka saa moja na nusu usiku, ni tukio ambalo nalitafsiri kwamba polisi waliniteka na kuniweka kizuizini ndani ya gari mpaka saa moja nanusu usiku, hawakunieleza nimefanya kosa gani saa moja nanusu nikawaambia kama ni kunishikila kwa ajili ya kwenda mahakama ya Kisutu, kwa vyovyote huu muda hakuna mahakama Kisutu, kwahiyo ni ama mniachie au mnipeleke mnifungulie mashtaka mnayoamini kwamba nimeyatenda.
Hitimisho likawa nipelekwe nikafunguliwe mashtaka, ndiyo nikapandishwa kituo cha polisi juu nikaanza kuandikishwa maelezo, nikagoma kuandika maelezo, kwa kuwaeleza kwamba niko tayari kutoa maelezo mahakamani, kwahiyo wakaandika tu tuhuma wanayonituhumu nikatuhumiwa kwa makosa ya kuhamasisha na kula njama ya kufanya maandamano, na baada ya hapo wakaniachia niondoke"
"Matukio haya kwa Pattern yake pamoja na kuwa mzigo wote unaliendea jeshi la polisi kwa sababu jeshi la polisi na vyombo vyake ndilo ambalo lilikuwa mstari wa mbele siku ya jana kwenye kamatakamata kwenye vipigo, kwenye matukio yote. Lakini ukiyatazama kiundani matukio ya jana kivyovyote vile hayakufanywa kwa amri na mamlaka ya jeshi la polisi peke yake.
Pattern ya matukio ya jana na ya jana yake, kuanzia namna ksesi ilivyotoka kwenye kuendeshwa na mahakama ya kawaida kwenda kwenye mahakama ya mtandao, inaonyesha kuna ushiriki wa idara ya usalama wa taifa, inaonesha kuna ushiriki wa serikali moja kwa moja. Niwaombe watanzania chuki, hasira, uchungu juu ya haya yote ambayo tumetendewa na wananchi wametendewa zielekezwe kwa serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Haiwezekani matukio yakafanyika katika taifa, Rais asiwe anafahamu au kuhusika katika hili jambo lote"
"Kanusho la polisi kuwa hayuko kituo cha polisi Central itakuwa ni kanusho la uongo kwa kuwa alipelekwa kituo cha polisi Central jeshi la polisi kupitia kwa mkuu wa jeshi la polisi lieleze ni sababu zipi zinafanya mpaka sasa Hilda Newton aendelee kushikiliwa, na aachiwe mara moja kama wanaodaiwa kutuhumiwa wa matukio yote ya jana"